• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

RC Gaguti Awataka Mawakili wa Kujitegemea Kuwa Wakweli Kwa Wateja Wao na Wananchi Kagera Wayaamini Maamuzi ya Mahakama

Posted on: February 1st, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti azindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini Mkoani Kagera kwa kupokea maandamano ya wadau mbalimbali wa Sheria wakiongozwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba  Mhe. Lucia Gamuya Kairo.

Katika hotuba yake ya uzinduzi Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa kilio chake kwa Mawakili hasa wale wa kujitegemea kuwa wakweli na kumtanguliza Mungu katika kutekeleza majukumu yao ya huduma kwa wananchi katika masuala ya kisheria.

“Kwa moyo wa dhati kabisa niwaombe Mawakili hasa wa kujitegemea muwe wakweli kwa wateja wenu, mwananchi anapokuja kwako na hoja yake msikilize kwa umakini ukiona hoja yake haina mashiko mbele ya sheria mwambie ukweli  kuwa hata akienda Mahakamani hawezi kushinda kesi hiyo kuliko kumdanganya na kupoteza muda na fedha zake Mahakamani. “ Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Pia Mkuu wa Mkoa gaguti aliwataka Mawakili hao kumtanguliza Mungu katika kazi zao ili wanapokuwa wanatoa msaada wa kisheria kwa wananchi wasiongozwe na tama za kibinadamu ili wateja wanaowatetea washinde mashauri yao kwa haki bila dhuruma au kupindisha haki.

Kwa upande wa wananchi Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa rai kwao hasa katika Mkoa wa Kagera kuwa nao wanapaswa kuridhika na maamuzi ya Makama pale yanapotolewa. “Unakuta kesi ilishaamuliwa mpaka Mahakama ya Rufani lakini mwananchi haridhiki akiona huko hakushinda anakuja kwa Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya kushinikiza kufuta hukumu jambo ambalo si sawa.”  Alisema Mhe. Gaguti.

Katika hatua nyingine Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba  Mhe. Lucia Gamuya Kairo alisema kuwa katika Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Mahakama itatembelea maeneo mbalimbali  mkoani Kagera kutoa msaada wa kisheria  kwa wananchi na maeneo hayo ni Magereza, Shule mbalimbali za Sekondari, na maeneo ya wazi kama soko kuu na kituo kikuu cha Mabasi Bukoba.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti alivitaka Vyombo vya Habari Mkoani Kagera hasa Redio za Kijamii kuitumia Wiki ya Sheria nchini iliyozinduliwa rasmi Mkoani Kagera  Februari 1, 2020 kurusha vipindi mubshara kutoka katika maeneo mbalimbali wadau wa Sheria watakakokuwa wanatoa misaada ya kisheria ili kutoa elimu kwa wananchi  walioko manyumbani.

Mwisho Mkuu wa Mkoa Gaguti akizungumzia Kaulimbiu ya Mwaka huu 2020 isemayo “Uwekezaji na Biashara: Wajibu wa Mahakama na Wadau kuweka Mazingira Wezeshi ya Uwekezaji.”  Aliwasisitiza wadau wote wa uwekezaji wanaopenda kuja kuwekeza katika mkoa wa Kagera kuhakikisha wanafuata na kukamilisha taratibu zote za kisheria ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima hapo mbeleni.

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria  imezinduliwa leo Februari  1, 2020 na kilele chake kitakuwa tarehe 6/02/2020. Ikumbukwe kuwa mkoa wa Kagera unahitaji watendaji wa kutosha katika masuala ya kisheria kutokana na wingi watu. Kagera ni mkoa wa tatu kwa  wingi wa watu ukiacha mikoa ya Dar es Saalam  na Mwanza kwa takwimu za mwaka 2019 ambazo zimetolewa hivi karibuni, Kagera kuna jumla ya watu 3,127,908 ukilinganisha na takwimu za mwaka 2012 watu 2,458,023.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.