- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa yawasili Mkoani Kagera Machi 14, kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu katika sekta za Afya, Elimu na Miundombinu.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Justine Razaro Nyamoga Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mkoani Iringa akiongea na Mkuu wa Mkoa Hajjat Fatma A. Mwassa ofisini kwake alisema lengo la ziara ya Kamati ni kukagua utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu katika Mkoa wa Kagera iliyopitishiwa fedha na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ilitarajiwa kukagua utekelezaji wa mradi wa Ujenzi wa Ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa utakaogharimu shilingi Bilioni 4.2, Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Biija iliyopo Wilayani Muleba wenye gharama ya shilingi milioni 584.2 na mradi ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Amali (ufundi) wilayani Muleba wenye gharama ya shilingi milioni 584.2
Akiwakaribisha wajumbe wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge mkoani Kagera Mkuu wa Mkoa Mwassa alitoa shukrani kwa Waheshimiwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukubali kupitisha bajeti ya fedha za kutekeleza miradi mikubwa katika mkoa wa Kagera ambayo sasa inakwenda kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi.
Naye Mheshimiwa Zainabu A. Katimba Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa aliyeambatana na Kamati hiyo ya Kudumu kwa niaba ya Serikali alisema Serikali ipo tayari kupokea maelekezo yote yatakayotolewa na Kamati hiyo ya Kudumu mara baada ya ukaguzi ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ikiwa na viwango vinavyoendana na thamani ya fedha iliyotolewa kwa ajili ya utekelezaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa