• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Zahanati ya Nyanga Manispaa ya Bukoba Iliyopatiwa Msaada wa Vifaa Tiba vya Shilingi Milioni 5 na Benki ya NMB Mkoa wa Kagera

Imewekwa : May 25th, 2018

Benki ya NMB Yatoa Misaada ya Shilingi Milioni Ishirini Kuboresha Huduma za Jamii Mkoani Kagera

Na: Sylvester Raphael

Benki ya NMB Mkoani Kagera yatoa misaada ya Shilingi Milioni 20,000,000/=  ya Vifaa Tiba na Samani kwa ajili ya Shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Manispaa ya Bukoba ili kuboresha huduma za Jamii katika Halmashauri hizo.

Misaada hiyo imetolewa mapema leo Mei 25, 2018 katika Zahanati ya Nyanga Manispaa ya Bukoba ambapo katika Zahanati hiyo Benki ya NMB Mkoa wa Kagera ilitoa Vitanda 6, Magodaro 6, Vitanda viwili vya kujifungulia Wajawazito na Boksi moja la vifaa vya vinavyotumika wakati wa kujifungua akinamama, vifaa tiba hivyo vikiwa na thamani ya shilingi milioni 5,000,000/=.

Aidha, Benki hiyo ilitoa Madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 10,000,000/= katika shule za Msingi Kyaitoke na Kitwe kila shule madawati 50. Pia Shule ya Sekondari Bukara ilipokea viti 60 na meza 60 vyenye thamani ya shilingi milioni 5,000,000/= kutoka katika Benki hiyo na kukamilisha jumla ya shilingi milioni 20,000,000/=.

Akikabidhi misaada hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meneja wa Kanda ya Ziwa Bw. Abraham Augustine alisema kuwa Benki ya NMB imeamua makusudi kujikita katika kuhudumia jamii hasa katika Sekta za Elimu na Afya ili kuigusa jamii ya Watanzania moja kwa moja.

Bw. Augustine aliongeza kuwa katika mwaka huu 2018 Benki hiyo imetenga shilingi Bilioni 1 kwaajili ya kuihudumia jamii na tayari misaada mbalimbali imeishatolewa katika Sekta za Elimu na Afya yenye thamani ya shilingi Milioni 100 na mkoa wa Kagera tayari umenufanika.

Bw. Augustine alimalizia kwa kusema kuwa Benk ya NMB inarudisha faida inayoipata kwa wananchi kutokana na biashara wanayoifanya ili kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na faida hiyo hasa kupitia huduma za kijamii katika Sekta za Elimu na Afya.

Mara baada ya kupokea misaada hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu M. Kijuu aliishukura sana Benki ya NMB kwa kurudisha faida kwa wananchi kupitia kutoa misaada ya kuboresha huduma za jamii kama Afya na Elimu

Mhe. Kijuu alitoa wito kwa Taasisi na Mashirika mbalimbali ya Serikali na yasiyokuwa ya Seriakli hasa Taasisi za Kibenki  kuiga mfano mzuri wa Benki ya NMB kwa kuiunga mkono Serikali katika juhudi zake za kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za kijamii kama shule na Sekta ya Afya ili wananchi wapate huduma bora.

Mkuu a Mkoa Kijuu alitolea mfano Sekta ya Elimu kuwa baada ya Serikali kutoa Sera ya Elimu bila malipo kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wazazi kuwaandikisha wanafunzi kwa wingi katika shule jambo ambalo linaifanya miundombinu iliyokuwepo hapo awali kuonekana kuwa ni michache kwahiyo Serikali kwa kishirikiana na wananchi na wadau wengine wote wanatakiwa kuiboresha miundombinu hiyo ili kukidhi uhuhitaji ili huduma bora itolewe.

Aidha, Mara baada ya kupokea msaada wa meza na viti meza kwaniaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Kashasha aliishukuru benki ya NMB na kusema kwamba msaada huo umewafikia kwa wakati muafaka ulipokuwa unahitajika.

Naye Mhe. Jimmy Kalugendo Naibu Meya wa Manispaa ya Bukoba alisema kuwa Vifaa Tiba vilivyotolewa na Benki ya NMB Katika zahanati ya Nyanga ni msaada mkubwa katika kituo hicho kwani vifa atiba hivyo vilikuwa vimekwamisha Zahanati kufunguliwa lakini sasa itafunguliwa na kuanza kutoa huduma bora kwa wananchi wa eneo hilo.

Mkoa wa Kagera unayo matawi 22 ya Benki ya NMB na tawi la mwisho kufunguliwa ni Tawi la Kabanga Wilayani Ngara na kuna uwezekano wa Tawi linguine kufunguliwa Kamachumu Wilayani Muleba ili kutoa huduma kwa wananchi wa Nshamba, Rubya na Kamachumu Kwenyewe.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa