• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Usimamizi Ufuatiliaji na Ukaguzi
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Uwekezaji Viwanda na Biashara
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
        • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Kilimo


SEKTA YA KILIMO

Utekelezaji wa Malengo ya Kilimo Msimuwa Mwaka 2017/2018

Katika msimu wa kilimo 2017/2018  Mkoa ulijiwekea lengo la kulima na kutunza jumla ya hekta 679,393 za mazao mbalimbali ya chakula zilizotarajiwa kuzalisha jumla ya tani  2,592,695  za ndizi, tani 360,729 za nafaka, tani 170,053 za mikunde na tani 1,042,326 za mazao ya mizizi.

Aidha, Mkoa ulilenga kulima na kutunza eneo la hekta 92,081.5 za mazao mbalimbali ya biashara linalotarajiwa kuzalisha, tani 81,994 za kahawa maganda, tani 4,488.9 za pamba mbegu,  tani 383 za tumbaku, tani 3,645 za majani mabichi ya chai.

Hadi kufikia Mwezi Juni, 2018 Mkoa ulikuwa umelima na kutunza jumla ya hekta 673,974 za mazao mbalimbali ya chakula na kuzalisha jumla ya tani 2,379,901 za ndizi, tani 285,595 za nafaka, kati ya tani hizi, zao la mahindi limechangia uzalishaji wa tani 243,287, tani 122,406  za  mikunde, aidha, zaidi ya  tani  1,095,347 za mizizi zimezalishwa kati ya tani hizi, zao la mhogo limechangia uzalishaji wa tani 818,742.

Hata hivyo, uzalishaji wa mazao ya mizizi katika Mkoa wa Kagera kwenye Halmashauri zake ni endelevu kwa msimu wote wa Vuli (Septemba –Desemba) na Masika (Machi –Mei).

Mazao ya biashara, Mkoa umelima na kutunza  jumla ya hekta 129,151 za mazao mbalimbali ya biashara na  kuzalisha tani 156.5 za tumbaku, tani 2,249.983 za majani mabichi ya chai, zao la kahawa na pamba bado yanaendelea kuvunwa. 

Katika mazao ya kipaumbele kitaifa Mkoa wa Kagera unazalisha mazao ya kahawa, chai, pamba na tumbaku.

Mkoa wa Kagera ni moja ya Mikoa inayozalisha kwa wingi zao la kahawa hapa nchini ambapo wastani wa uzalishaji wa kahawa ya maganda kwa mwaka ni tani 50,000. Kutokana na takwimu za uzalishaji kahawa kitaifa, Mkoa wa Kagera unaongoza katika uzalishaji wa kahawa.

Zao la pili la biashara linalozalishwa Mkoani Kagera ni Chai inayolimwa katika Wilaya za Bukoba na Muleba. Wastani wa uzalishaji wa zao la chai kwa mwaka ni tani 1,000 hadi 1,500 kwenye eneo la hekta 1,132.

Zao la tatu ni pamba ambayo huzalishwa katika Wilaya za Biharamulo na Muleba. Wastani wa uzalishaji kwa mwaka ni tani 900 ambazo huzalishwa kwenye eneo la hekta 2,000. Idadi ya wakulima wanaojihusisha na kilimo cha pamba Mkoani Kagera ni takribani 5,700.

Zao la nne kwa umuhimu katika Mkoa wa Kagera ni Tumbaku ambayo huzalishwa katika wilaya ya Biharamulo kwenye eneo la hekta 237 na wastani wa mavuno kwa mwaka ni tani 230.

Mazao mengine ya biashara yanayolimwa Mkoani Kagera ni pamoja na vanilla na miwa. Wastani wa uzalishaji wa zao la vanilla ni tani 45 kwenye eneo la hekta 50 ambapo wakulima wanaojiuhusisha na kilimo cha vanilla ni takribani 6,000 wengi wao wakiwa chini ya usimamizi wa MAYAWA (Maendeleo ya Wakulima).


Mikakati ya Mkoa ya Kuendeleza zao la Kahawa Iliyopitishwa na Kikao cha Wadau Mkoani ni Kama Ifuatvyo:-

Kuongeza tija ya uzalishaji wa kahawa kutoka kilo 500 kwa hekta hadi kilo 2,000 kwa hekta za kahawa maganda kwa kuimarisha huduma za ugani, kuongeza na kuimarisha matumizi ya miche bora na pembejeo za kilimo na Kuimarisha udhibiti wa magendo ya kahawa.

  • Kuongeza maeneo ya uzalishaji wa kahawa na kufufua mashamba yaliyokanda kwa muda mrefu.
  • Kuimarisha uwezo wa vyama vya ushirika na usimamizi wa vyama vya ushirika ili viwe na uwezo wa kukusanya kahawa za wakulima na kuzitafutia soko la uhakika.
  • Kupambana na wizi pamoja na biashara ya magendo.
  • Kuhakikisha kila kata inayozalisha kahawa iwe na Afisa ugani.
  • Kumarisha ziara za uhamasishaji na utoaji elimu kwa wakulima.


Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la chai:

  • Kuhamasisha wananchi kuongeza uzalishaji wa chai kwa kufufua mashamba yaliyokanda.
  • Kuimarisha utendaji wa kiwanda cha chai Kagera ili kiwe na uwezo wa kuwalipa wakulima kwa wakati kwa kutafuta mbia mwenye mtaji wa kutosha.
  • Kuimarisha huduma za ugani katika kilimo cha chai.
  • Kuimarisha bei ya majani ya chai ili kuvutia wakulima kuzalisha chai kwa wingi.
  • Kuhakikisha chai inayozalishwa inaongezewa thamani ili mkulima aweze kupata bei ya soko tofauti na bei zinazopangwa na wadau kwa sasa.

 

Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la pamba:

  • Kuimarisha upatikanaji wa pembejeo bora za zao la pamba hususani mbegu na viuadudu.
  • Kuimarisha huduma za ugani kwa kuwajengea uwezo wataalamu wa kilimo ili waweze kutoa elimu sahihi kwa wakulima kupitia mashamba darasa.
  • Kuhamasisha wakulima kujiunga katika vikundi na vyama vya msingi vya mazao ili iwe rahisi kufikiwa na huduma za mikopo na huduma nyingine za ugani.
  • Kuimarisha ufuatiliaji na usimamizi wa zao la pamba kupitia viongozi wa ngazi zote.
  • Kuimarisha utoaji elimu juu ya kanuni bora za kilimo cha pamba.
  • Kuhamasisha wakulima kupanua maeneo ya kulima zao la pamba.


Mikakati ya Mkoa ya kuendeleza zao la tumbaku:

  • Kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za zao la pamba hususani mbegu, mbolea viuadudu na viuatilifu kwa wakati.
  • Kuimarisha huduma za ugani kwa kuwajengea uwezo wataalamu wa kilimo ili waweze kutoa elimu sahihi kwa wakulima kupitia mashamba darasa.
  • Kuhamasisha wakulima kujiunga katika vikundi na vyama vya msingi vya mazao ili iwe rahisi kufikiwa na huduma za mikopo na huduma nyingine za ugani.
  • Kuimarisha ufuatiliaji na usimamizi wa zao la tumbaku kupitia viongozi wa ngazi zote.


HALI YA CHAKULA

Mahitaji ya Chakula 

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Mkoa wa Kagera ulikuwa na Idadi ya wakazi wapatao 2,458,023. Ongezeko la watu kwa mwaka limepanda hadi kufikia wastani wa asilimia 3.2 kutoka wastani wa 3.1 mwaka 2002.  Makadirio ya mwaka 2017 Mkoa wa Kagera una idadi ya watu 2,879,231. Kwa uwiano wa mahitaji ya mtu mmoja kwa siku ambayo ni gramu 65 ya utomwili na gram 650 za vyakula vya wanga, Mkoa wa Kagera unahitaji tani 655,479 ya vyakula vya wanga na tani 65,547 ya vyakula vya utomwili kwa mwaka.

 

Uhakika wa Chakula Katika Mkoa wa Kagera

Hadi mwishoni mwa mwezi Juni, 2018 Wilaya zote zinazozalisha ndizi zilikuwa zimezalisha asilimia 92 ya lengo, sawa na tani 2,379,901 za ndizi ambazo ndiyo chakula kikuu kwa wananchi walio wengi katika Mkoa wa Kagera, hivyo kiasi hicho kinatosheleza mahitaji kwa kipindi husika na hata kuweza kuuzwa katika Mikoa ya jirani na nchi jirani.

 

Ugavi wa mazao mbalimbali kama ya nafaka, mizizi na mikunde ni mzuri kwenye masoko ya vijijini na  mjini kwa mwaka 2017/2018 na bei za mazao hayo zimekuwa za wastani, mfano wastani wa kilo moja ya mahindi kwasasa ni Tsh 350-550/= na ndizi mbichi kwa kilo tsh 500-1000/=. Vyakula aina ya mizizi (muhogo, na viazi) vinaendelea kuvunwa na kuimarisha hali ya upatikanaji wa chakula  katika ngazi ya Kaya.

Hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa ili kuimarisha usalama wa chakula katika Mkoa wa Kagera. Hatua hizo ni pamoja na Kuhamasisha matumizi  ya maghala ya kuhifadhia chakula, kuendelea kutoa elimu ya hifadhi ya vyakula kwa kutumia mifuko ya PICs, kuhamasisha wakulima kupanda mazao ya muda mfupi ikiwa ni pamoja na kusisitiza Matumizi ya mbolea na mbegu bora na za muda mfupi ambazo zinastahimili mvua chache na magonjwa kwa kushirikiana na Kituo cha utafiti Maruku. Kuwahamasisha wakulima kujiunga katika vikundi/ vyama vya msingi vya mazao (AMCOS) na  vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) ili waweze kupata mtaji.

Aidha, Katika kuendeleza Sekta ya kilimo, Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri imekuwa ikibuni Mipango mbalimbali ya Kisera na Kimkakati mfano Maonesho ya kilimo (Nanenane) Kimkoa, Lengo likiwa ni kubadilisha kilimo kutoka kilimo cha mazoea na kukifanya kiwe kilimo cha kibiashara na endelevu kutokana na teknolojia sahihi na mbalimbali wanazozipata kupitia maonesho hayo.


Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • Tazama zote

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa