- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Fursa za Uwekezaji Ufugaji
Mkoa wa Kagera una eneo lenye ukubwa wa takribani hekta 1,200,000 ambalo linafaa kwa shughuli za ufugaji. Kati ya eneo hilo eneo lenye ukubwa wa takribani hekta 400,000 pekee ndilo linalotumika kwa shughuli za ufugaji.
Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na Wizara na Mamlaka za Serikali za Mitaa unaendelea kubainisha maeneo yanayofaa kwa ajili ya ufugaji katika Halmashauri kwa kuzingatia hifadhi ya mazingira na uendelezaji wa malisho. Maeneo yaliyoainishwa katika Halmashauri kwa matumizi ya ufugaji ni kama ifuatavyo:
Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi ina eneo la Hekta 63,884.02. Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Hekta 31,927.19. Aidha, hivi karibuni mpango wa kubaini eneo lenye ukubwa wa Hekta 50,000 linalopendekezwa toka eneo la Mwisa II lililopo kati ya ranchi ya Kagoma na Ziwa Burigi katika Wilaya za Muleba na Karagwe umeanza.
Halmashauri ya wilaya ya Karagwe Hekta 154,000 pamoja na Hekta 2,000 katika Kata ya Kihanga zilizotolewa na Serikali kutoka eneo la NARCO katika ranchi ya Kitengule. Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Hekta 5,930. Halmshauri za wilaya za Biharamulo, Ngara na Kyerwa zimetenga maeneoambayo bado hayajabainishwa ukubwa wa maeneo hayo. Jumla ya maeneo yaliyotengwa na kupimwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Mkoani Kagera kwa ajili ya wafugaji ni Hekta 307,741.21
Kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya mifugo (ng’ombe, mbuzi n.k), mkoa unayo fursa kubwa ya kuanzisha kiwanda cha nyama na maziwa. Aidha, ipo fursa ya kuanzisha kiwanda cha usindikaji na uchakataji ng’ozi na utengenezaji wa bidhaa za ng’ozi kama vile viatu, mikoba, mikanda n.k
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa