- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Shughuli za Sekta hii zimegawanyika katika sehemu ya Viwanda, Biashara/Masoko, kwa lengo la kuinua na kuongeza ufanisi kwa kuweka uhusiano mpana kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika uzalishaji nchini sambamba na kujenga uchumi endelevu, unaohimili ushindani katika masoko ya nje kama njia ya kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi nchini. Shughuli kuu zinazofanywa na sekta ya Biashara katika Sekretarieti ya Mkoa wa Kagera ni kama ifuatavyo:-
i. Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wadau wa maendeleo ya kiuchumi kuhusu masuala ya biashara, masoko, viwanda na uwekezaji katika mkoa.
ii. Kutoa elimu na mafunzo ya ujasiriamali kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, watu wananchi/watu binafsi, vikundi, makampuni pamoja na mashirika yanayohudumia jamii katika mkoa wa Kagera.
iii. Kuratibu utoaji wa leseni za biashara kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) Mkoani Kagera.
iv. Kuratibu shughuli za usajili wa majina ya biashara na makampuni kwa mujibu wa sheria ya usajili wa shughuli za biashara (Business Activities Registration Act-BARA namba 14 ya mwaka 2007) na sheria ya usajili wa makampuni namba 12 ya mwaka 2002 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2011- (Business Laws) Misclleneuos Amendments
v. Kujenga mazingira wezeshi na yenye kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika Mkoa wa Kagera.
vi. Kuratibu upatikanaji wa vibali mbalimbali vya uuzaji bidhaa nje ya nchi na uingizaji bidhaa.
vii. Kutoa ufafanuzi wa miongozo , sera, sheria na kanuni kwa wadau wa maendeleo ya kiuchumi kuhusu biashara, masoko, viwanda na uwekezaji katika Mkoa.
viii. Kuwaunganisha wakulima na wazalishaji na masoko ya bidhaa zao.
ix. Kuhamasisha wakulima/wajasiriamali na wazalishaji kuzalisha kwa wingi na kwa kuzingatia ubora na tija hatimaye kuongeza thamani. (Value Addition).
x. Kuhamasisha Watanzania kupenda bidhaa za Tanzania ili kukuza uchumi wa Tanzania.
xi. Kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika mkoa na kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika Mkoa wa Kagera
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa