- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkoa wa Kagera unakadiriwa kuwa na ng’ombe wapatao 554,380 wanaofugwa ambapo ng’ombe wa asili ni 534,299 na ng’ombe wa maziwa ni 20,081. Mbuzi wafugwao ni 639,449. Wanyama wengine ni kondoo 55,935, nguruwe; 57,747 na wanyama kazi kama vile punda 224 na farasi 18. Wengine ni bata 50,166; sungura; 17,525 na mbwa; 39,822.
Mifugo iliyopo kwenye Vitalu vya Wawekezaji kwenye Ranchi za Taifa (NARCO) ni ng’ombe 40,548 sawa na asilimia 7.3 ya ng’ombe wote waliopo Mkoani hapa; ambapo wafugaji wakubwa ni Agro Ranching ng’ombe 4,278, Kagera Sugar 4,005, NARCO Missenyi ranch 1,640, Wawekezaji kwenye vitalu chini ya NARCO (Kitengule 8,308, Missenyi 9,201, Kagoma 10,158, na Mabale 2,958). Hivyo ng’ombe wapatao 513,832 sawa na asilimia 92.7 wanapatikana katika maeneo mengine ya vijiji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa