- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MADINI
Madini Yapatikanayo Mkoani Kagera
Mkoa wa Kagera una madini yafuatayo kama yalivyo tofautishwa kutokana na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010:
Utafiti wa Madini Katika Mkoa
Baada ya Serikali kupitisha Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Kanuni zake za mwaka 2010, ndipo Watanzania wengi waliona fursa ya uwekezaji katika madini Mkoani Kagera. Mkoa wa Kagera kuna jumla ya lesseni 56, zilizo tolewa hadi kufikia mwezi Septemba 2017.
Leseni za Madini Zilizopo Katika Mkoa
Aina za leseni za uchimbaji zilizopo Mkoani Kagera ni kama ifuatavyo:-
SML (Special Mining Licence) Leseni hii kubwa ya uchimbaji wa madini inamilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kupitia kampuni yake tanzu ya STAMIGOLD Leseni hiyo yenye namba SML 157/2003 ipo Wilayani Bihalamulo.
PL (Prospecting Licence) Hizi ni leseni kubwa za utafiti nz leseni hai za utafiti zilizopo katika Mkoa huu ni 56 ambazo ni hai. Leseni hizi hizi zinafanya utafiti wa madini ya aina mbalimbali katika Mkoa wa Kagera.
PML (Primary Mining Licence) Leseni hizi ni za utafiti na uchimbaji mdogo wa madini,katika a Mkoa huu kuna jumla ya leseni 467 za utafiti na uchimbaji mdogo wa madini ya aina mbalimbali zikiwemo,Bati, Dhahabu,Madini ujenzi na Kaolin.
Retention Licence (RL) Leseni hii ipo moja na inamilikiwa na Kampuni ya Kabanga Nickel. Leseni hii yenye namba RL 0001/2009 inashikilia eneo ambalo limefanyiwa utafiti wa madini ya nickel katika Wilaya ya Ngara. Hadi sasa tayari wamemaliza miaka mitano ya kipindi cha kwanza na wameomba na kupewa kwa upya kipindi kingine cha miaka mitano hadi 2019. Bado kampuni hii haijaanza shuguri za uzalishaji na Sababu kuu ni kushuka kwa bei ya madini ya Nickel katika soko la Dunia.Na chagamoto ya Miudombinu, ikiwemo umeme wa uhakika.
Uchimbaji na Uzalishaji wa Madini Mkoani
Madini yanayochimbwa na mchimbaji mkubwa ni dhahabu. Madini haya yanachimbwa na kampuni ya Stamigold Company Ltd Gold Mine huko Biharamulo. Madini mengine yana chimbwa na wachimbaji wadogo ni pamoja na Bati, Kaolin na madini ujenzi (mchanga, kokoto).
Uzalishaji wa Dhahabu
Uzalishaji wa dhahabu katika Mkoa wa Kagera, umekuwa ukifanyika katika leseni namba SML 157/2003. Leseni hii ilikuwa inamilikiwa na kampuni ya Barrick Tulawaka Mine na sasa inamilikiwa na Shirika la Umma STAMICO kupitia kampuni yake ya STAMIGOLD Company Ltd .Madini ya dhahabu yanachimbwa pia na wachimbaji wadogo maeneo ya Busini, Mavota na Kalukwete Wilayani Biharamulo.
Uzalishaji wa Bati Ghafi (Tin)
Hadi sasa hakuna mchimbaji mkubwa wa madini haya. Hivyo madini haya yanachimbwa na wachimbaji wadogo wadogo Wilayani Kyerwa katika Mkoa huu wa Kagera. Katika kipindi cha mwaka 2011/12 hadi 2016/ 2017 jumla ya tani 590.65 za bati ghafi zenye thamani ya shilingi 6,552,647,500 zilizalishwa na kulipiwa mapato ya serikali (mrabaha) wa jumla ya shilingi 256,140,673 na Marahaba shilingi 95,095,347.
Uzalishaji wa Madini ya Kaolin
Katika Mkoa wa Kagera, madini haya yanazalishwa katika Wilaya ya Biharamulo pekee na mchimbaji mdogo. Uzalishaji wa madini haya unategemea uhitaji wake sokoni kwani hadi sasa yamekuwa yakitumika katika shughuli za ujenzi wa nyumba tu. Katika kipindi cha mwaka 2012/13 hadi 2016/17 jumla ya tani 9,138.49 za Kaolin zenye thamani ya shilingi 575,152,666.67/= zilizalishwa na kuchangia pato la serikali (Mrahaba) wa Tsh. 17,254,580/=
Uzalishaji wa Madini ya Ujenzi
Uzalishaji wa madini ujenzi umekuwa ukiathiriwa na msimu wa mvua. Kwa takwimu zilizopo, misimu ya mvua uzalishaji hupungua kwani watu wengi wanakuwa hawafanyi shughuli za ujenzi hivyo kupelekea madini haya kuwa na uhitaji mdogo ukilinganisha na kipindi cha kiangazi. Katika kipindi cha mwaka 2012/13 hadi 2016/17 jumla ya tani 145,878.5 za madini ya ujenzi (Kokoto, Mchanga, Morum) zenye thamani ya Tsh. 1,491,070,000 zilizalishwa na kuchangia mapato (Mrahaba) Tsh. 44,732,100.
Biashara ya Madini
Leseni za biashara ya Madini zilizotolewa Mkoa wa Kagera ni;-
Leseni ndogo ya ununuzi na uuzaji madini (Brokers Licence).
Leseni hizi hutolewa kwa Watanzania tu, na inamtaka mhusika kununua madini kutoka kwa mchimbaji mwenye leseni ya uchimbaji na kumuuzia mwenye leseni kubwa ya ununuzi (Dealer licence). Hadi kufikia sasa, Ofisi ya Madini imepokea jumla ya maombi 27 ya leseni hizi.
Leseni kubwa ya ununuzi na uuzaji wa madini (Dealer Licence).
Leseni hii hutolewa kwa Mtanzania au raia wa kigeni mwenye ubia na Mtanzania. Katika ubia huo, Mtanzania anatakiwa awe na ubia usiopungua 25%. Hadi sasa kuna jumla ya maombi manne (5) ya leseni hizi yaliyowasilishwa. Leseni hii humuwezesha mmiliki kuuza madini yaliyonunuliwa nje ya nchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa