- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Wilaya
- Halmashauri
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Sekta ya uvuvi ni moja ya Sekta muhimu katika kuwapatia Wananchi wengi wa Mkoa wa Kagera ajira, lishe bora mfano protini, kipato na hivyo kuchangia katika kumuondolea mwananchi umaskini. Shughuli za Uvuvi katika mkoa hufanyika kwa kiwango kikubwa katika Ziwa Victoria Wilaya ya Muleba , Bukoba na Missenyi. Wilaya za Ngara, Biharamulo, Kyerwa na Karagwe hazipakani na Ziwa Victoria hivyo Uvuvi hufanyika katika mto Kagera, Ngono na Ruvuvu , mabwawa na maziwa madogo madogo ya Burigi, Rwakajunju, Kamakala, Ikimba, Rushwa, Melula, Katwe, Liko, Karenge, Mitoma na Rumanyika. Samaki wanaovuliwa kwa wingi katika Ziwa Victoria ni pamoja na Sangara (Nile perch), dagaa, Sato na furu . Samaki wanaofugwa katika mabwawa ya kuchimba mkoa wa Kagera ni jamii ya Nile tilapia (O. niloticus, O. variabilis, Oesculentus na O. leucostictus) na Kambale mumi (Clarius gariepinus).
Sekta ya Uvuvi inatekeleza mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kudhibiti Uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira, kuendeleza ufugaji bora wa samaki, kudhibiti utoroshaji wa mazao ya samaki kwenda nchi jirani, kutoa elimu juu ya VVU/UKIMWI, usimamizi wa masoko na mialo ya samaki, kuhakiki viwango vya ubora na usalama wa mazao ya Uvuvi, kukusanya mapato ya Uvuvi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mitumbwi yote inasajiliwa ili kidhibiti mapato na uhalifu n.k . Juhudi hizi zinafanyika na kutekelezwa kwa kuzingatia Sera ya Uvuvi ya mwaka 1997, Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003, Mikakati na Kanuni zake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Anwani: S.L.P 299 BUKOBA
Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa