- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
“Tangu nizaliwe nikue na nijitambue katika maisha yangu sikuwahi kuona natendewa wema kama siku ya leo na siku ya Jumamosi ya tarehe 29.12.2018, nimekuwa kama yule mlemavu (Kiwete) aliyemuona Yesu na kumuomba amsaidie naye Yesu alimwamuru asimame na kutembea.”
Hayo maneno ni ya Bw. Aron Bukuru Mlemavu mwenyeji wa Kaperanono Kata Nyabusozi Wilayani Biharamulo ambaye ni Mlemavu wa mguu mmoja wa kulia ambapo aliyasema maneno hayo baada ya kupokea mguu bandia na fedha taslimu shilingi 2,023,000/= kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti.
Bw. Aron Bukuru ni Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Nyabusozi Wilayani Biharamulo akiwa katika kikao cha ndani cha chama kilichofanyika Desemba 29, 2018 Wilayani Muleba chini ya Katibu Mkuu Taifa Dk. Bashiru Ally aliomba msaada wa kupatiwa mguu bandia mpya kwani aliokuwa nao ulikuwa umeisha muda wake na ulikuwa ukimuumiza na kumsababishia majereha.
Katibu Mkuu Taifa wa CCM Dk. Bashiru Ally aliendesha harambee katika kikao hicho na Bw. Aron alichangiwa kiasi cha Shilingi 2,723,000/= taslimu ambapo fedha hizo zilikabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti ili kuhakikisha Bw. Aron Bukuru anapata mguu bandia mpya na fedha itakayobaki imsaidie katika matumizi madogo madogo pia na kuweka akiba kwa ajili ya kununulia mguu bandia mwingine endapo huo aliopata ukiisha muda wake.
Baada ya Mkutano ule wa tarehe 29/12/2018 chini ya usimamizi wa Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti Bw. Aron alipelekwa katika Hospitali ya Kagondo Wilayani Muleba na kutengenezewa mguu bandia kwa gharama ya shilingi 600,000/= pia na kupewa shilingi 100,000/= kwa matumizi ya chakula akiwa hospitalini hapo na nauli ya kurudi Nyabusozi Wilayani Biharamulo.
Mara baada ya Mguu bandia kukamilika Januari 10, 2019 Mkuu wa Mkoa Gaguti alifika nyumbani kwa Bw. Aron Bukuku Kaperanono Nyabusozi Wilayani Biharamulo na kumkabidhi kiasi cha shilingi 2,023,000/= fedha iliyobaki baada ya mguu bandia kupatikana. Akikabidhi fedha hizo Mhe. Gaguti alisema kuwa alikuwa natekeleza jukumu aliloachiawa na Katibu Mkuu Taifa wa CCM Dk. Bashiru Ally.
Mwenyekti wa CCM Mkoa wa Kagera Mama Costancia Nyamwiza Buhiye akiongea na ndugu, jamaa na wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais John Pombe Magufuli ni Serikali inayowajali wananchi wake hasa wanyonge wa chini kabisa.
Naye Mama Jonesia Masabile mke wa Bw. Aron Bukuku akitoa shukrani zake kwa Mkuu wa Mkoa alisema kuwa anashukuru mmewe aliyotendewa kwani ilikuwa imefikia mahali mguu bandia aliokuwa nao ulikuwa ukimuumiza na kumchubua jambo ambali lilikuwa likimfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake kikamilifu hasa shughuli za kilimo.
Bw. Aron Bukuku alipata ajali ya gari Ushirombo mwaka 2006 wakati akitokea Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga na kupelekwa Hospitali ambapo ilipelekea mguu wake wa kulia kukatwa na kulazimika kutumia mguu bandia na tangu mwaka 2006 hadi 2018 amekuwa akitumia mguu bandia wa kulia na kila ukiisha muda wake anabadilisha na kununua mguu mwingine ambapo mguu bandia mmoja gharama yake ni kati ya shilingi laki tano hadi nane.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.