• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Kagera Wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa (Hayupo Pichani) Katika Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoani Kagera.

Posted on: March 8th, 2018

Mkuu wa Mkoa Kagera Aagiza Mkandarasi Kukamatwa na Kufikishwa Ofisini Kwake Akiwa na Pingu Mikononi Baada ya Kuitia Serikali Hasara

Mkuu wa Mkoa wa Kagera aagiza  Mkandarasi wa Kampuni ya MECCO aliyeshinda zabuni  ya ujenzi wa barabara zenye thamani ya shilingi bilioni saba na kukataa kusaini mkataba wa kuanza ujenzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kukamatwa  na kufikishwa  Ofisini kwake akiwa na pingu mikononi ili kutoa sababu za kuitia Serikali hasara.

Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu alitoa agizo hilo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa kwenye kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika Mkoani Kagera Machi 8, 2018 ambapo katika kuwasilisha hoja Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Chief Karumuna  kumuomba Mkuu Mkoa kumchukulia hatua Mkandarasi huyo baada ya kugoma kusaini mkataba wakati alishinda zabuni ya ujenzi wa barabara hizo.

Chief Karumuna alisema kuwa Manispaa ya Bukoba imepata hasara baada ya Mkandarasi kukataa kusaini mkataba wa kuanza ujenzi wa barabara zenye thamani ya shilingi bilioni saba na zabuni kutangazwa tena upya, pia alisistiza kuwa fedha hizo zilitolewa na Benki ya Dunia na utekelezaji wa miradi yake ni wa kipindi maalumu kwa hiyo Mkandarasi huyo amechelewesha muda wa utekelezaji.

Katika kikao hicho ambacho Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti aliwasistiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini TARURA Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanatengeneza barabara za mipakani ili kuimarsha ulinzi na usalaama wa mkoa na na chi kwa ujmla. Barabara hizo ni Bubale-Missenyi Runch- Kakunyu  Kilomita 32.5, Bubale – Kamwema Kilomita 17.8  Wilayani missenyi na barabara ya Nyabishenge-Nyakanoni-Ibanda Game Reserve kilomita 15 Wilayani Kyerwa.

Vilevile Meneja wa Wakala wa Umeme na Ufundi (TEMESA) Mkoa wa Kagera ameagizwa na kikao hicho kusitisha mara moja tozo ya shilingi 80,000/= ya ukaguzi wa magari ya Serikali pale yanapotakiwa kukaguliwa ili yakatengenezwe baada ya wajumbe kuwasilisha sheria kikaoni inayoelekeza kuwa magari ya Serikali yanatakiwa kukaguliwa bure. Hadi Mkuu wa mkoa atakapopata walaka unaoruhusu kutoza magari ya Serikali.

Mkoa wa Kagera unahudumia barabara zenye mtandao wenye jumla ya kilomita 7,505.42 kati ya hizo, kilometa 675.46 ni barabara za lami, kilometa 2,791.56 barabara za changarawe na kilometa 4,038.96 zikiwa in barabara za udongo.

Mkoa wa Kagera kwa mwaka wa fedha 2017/18 uliidhinishiwa shilingi Bilioni 10,710.05 kwajili ya matengenezo ya kazi za barabara na ujenzi wa madaraja. Pia mkoa umeidhinishiwa shilingi bilioni 14,180.937 kwa ajili ya matengenezo ya Barabara Kuu na Barabara za Mkoa kwa mwaka wa fedha 2017/18

Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Mkoani Kagera Mkuu wa Mkoa wa Kagera amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka kumkamata na kumpeleka ofisini kwake kijana anayemtesa mama yake mzazi kwa kutaka kumnyanganya shamba lake na mama huyo ameshinda kijana huyo mara mbili Mahakamani.

“Mtafute kijana huyo na kumleta kwangu nijue ana matatizo gani ili tumsaidie maana atamuua mama yake, hana uchungu na mama yake mzazi. Mama huyoaliwasilisha kilio chake katika mkutano wa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. Lukuvi Wilayani Karagwe lakini kijana huyo bado anaendelea kumsumbua mama yake mzazi.” Alifafanua Mkuu wa Mkoa Kijuu.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.