• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karagwe Wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kagera (hayupo pichani) Kwa Umakini

Posted on: May 31st, 2018

Watumishi Wawili Halmashuri ya Wilaya ya Karagwe Wasimamishwa Kazi Kupisha Uchunguzi wa Upotevu Wa Zaidi ya Shilingi Milioni 500

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu leo Mei 31, 2018 awasimamisha kazi watendaji wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kufuatia utendaji usioridhisha wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kieletroniki na kusababisha upotevu wa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 500 katika Halmashauri hiyo.

Hatua hiyo imechukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera baada ya Katibu Tawala wa Mkoa CP Diwani Athuman kuunda tume ya uchunguzi wa upotevu wa fedha hizo kutokana na ripoti ya Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ambapo tume hiyo ilifanya kazi ya uchunguzi kwa siku nne tu na kubaini upotevu fedha cha shilingi 500,000,000/=

Uamuazi wa kuwasimamisha kazi watumishi wawili Afisa TEHAMA Bw. Beatus Nyarugenda na Mhasibu wa Mapato Bw. Innocent Kakulima ulitolewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu katika kikao cha Kamati ya Fedha cha Halmashauri hiyo ambapo alitoa maagizo kama ifutavyo;

Moja, Uchunguzi wa kina ufanyike kwa kila Maafisa walioomba na kuidhinisha marekebisho au miamala ya mapato ya ndani katika mfumo bila kuwa na kibali cha Afisa Masuuli na kiasi cha fedha kinachohusika katika eneo hilo ni Shilingi 427,027,430.49/=

Pili, Watumishi waliokusanya mapato na hawajapeleka benki fedha walizokusanya jumla ya Shilingi 127,094,900/= hadi tarehe 14 Aprili, 2018 waziwasilishe katika akaunti ya mapato ya Halmashauri ndani ya siku 7, na vielelezo vihakikiwe na Katibu Tawala wa Wilaya ya Karagwe na watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo sheria ichukue mkondo wake.

Tatu, Afisa TEHAMA Bw.Beatus Nyarugenda tume ilimbaini kuwa hakuwa makini kwa kukiuka usalama wa mtandao kwa kutoa haki kwa Afisa mmoja kukamilisha muamala mzima wa kufuta ama kubadili tarakimu za fedha katika mtandao. Mkuu wa Mkoa aliagiza utaratibu huo uachwe mara moja na Mkuu wa TEHAMA wa Mkoa kuhakikisha usalama wa mfumo unawekwa vizuri mara moja.

Nne, Mhasibu wa Mapato Bw. Innocent Kakulima tume ilimbaini kutokuwa na uthibitisho wa kupeleka benki shilingi 23,216,400/= fedha ambazo alizichukua kutoka kwa wakusanyaji. Aidha katika ufuatiliaji ilibainika kuwa katika Halmashauri ya Karagwe kuna vituo vya ukusanyaji (POS) 39, hivyo inahitajika uchunguzi zaidi ili kuwa na uhakika katika vituo vyote kama Mhasibu huyo hakukusanya fedha.

Baada ya maagizo hayo Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu alimwagiza Kamanda wa TAKUKURU Mkoa kupokea taarifa hiyo kwa ajili ya kuifanyia uchunguzi ambao utatoa majibu sahihi ya kushuka kwa mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe.

Aidha, wakati uchunguzi unafanyika Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu aliagiza Afisa TEHAMA Bw. Beatus Nyarugenda na aliyekuwa Mhasibu wa Mapato Bw. Innocent Kakulima wasimame kazi kupisha uchunguzi huo. Pia aliagiza kuwa wakati uchunguzi unaendelea watuhumiwa wengine watakaobainika kuwa wanaweza kuingilia uchunguzi wawapo maeneo yao ya kazi ajulishwe haraka ili nao wahusishwe kupisha uchunguzi.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu alihitimisha kwa kurudia kumuagiza Kamanda wa TAKUKURU Mkoa kufanya Uchunguzi na kuukamilisha haraka pia na kuzitahadharisha Halmashauri nyingine za Wilaya za Mkoa wa Kagera hususani Wakurugenzi Watendaji na Watumishi wengine kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa bila kujihusisha na vitendo vya kuyahujumu mapoto hasa mapato ya ndani ya Serikali.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.