• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya Ngara Laagizwa Kuwachukulia Hatua Wafujaji wa Fedha za Serikali

Posted on: July 26th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu aliagiza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kuchukua hatua zinazostahili kwa watumishi na wadau wote wa Halmashauri waliosababisha kwa namna yoyote ile Halmashauri kuwa na hoja za miaka ya nyuma ambazo majibu yake hayakumridhisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mkuu wa Mkoa Kijuu alitoa agizo hilo katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizoishia tarehe 30 Juni, 2017 ambapo kwa mwaka 2016/ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ngara ilipata hati safi.

Pamoja na Halmashauri hiyo kupata Hati Safi mwaka 2016/2017 Mkaguzi alionesha udhaifu wa kutozingatia Sheria na kanuni za Usimamizi wa Fedha, Manunuzi, Usimamizi wa watumishi, Usimamizi wa mali za Halmashauri, Usimamizi wa Mikataba na kutozingatia maagizo mbalimbali ya Serikali.

Katika ukaguzi wake Mkaguzi alionesha kuwa Menejimenti ya Halmashauri haitekelzi kikamilifu baadhi ya hoja za miaka ya nyuma na hivyo kuendelea kubakia bila kufungwa. Halmashauri ilikuwa na hoja za nyuma 108 ambapo kati yake 30 zilizotekelezwa kikamilifu na kufungwa, 38 ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji, hoja 9 hazijatekelezwa kabisa na hoja 31 ziliondolewa na Mkaguzi kwa sababu mbalimbali.

Aidha, katika utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Bunge yaliyotolewa tarehe 30/08/2017 Mkaguzi ameonesha kuwa agizo moja tu liko katika hatua za utekelezaji na maagizo mawili hayajatekelezwa. Miongoni mwa hoja za miaka ya nyuma zilizobakia bila kutekelezwa kikamilifu na kufungwa ni kama ifutavyo;

Moja, Mawakala kutowasilisha mapato yenye thamani ya shilingi 38,550,000 kulingana na mikataba yao (2012/2013) na shilingi 3,000,000 (2013/2014). Pili, Kutokamilisha utaratibu wa kufuta vitabu vya wazi vya mapato (open receipt book) 4 ambavyo havikuwasilishwa wakati wa ukaguzi (2012/2013). Tatu, Kutokamilisha utaratibu wa kufuta hasara ya mapato ya ndani ya shilingi 4,308,030 ambazo hazikuwekwa benki na mtumishi ambaye sasa ni marehemu (2012/2013).

Nne, Kutothibitika kurejeshwa Hazina mishahara isiyolipwa ya jumla ya shilingi 27,613,192 (2012/2013), shilingi 8,309,656 (2013/2014), shilingi 24,080,903 (2014/2015) na shilingi 47,011,670 (2015/2016). Tano, Kutochangia kikamilifu katika Mfuko wa Wanawake na Vijana na hivyo kubakia na deni la shilingi 42,501,143 kwa mwaka 2013/2014 na shilingi 53,757,770 mwaka 2014/2015.

Sita, Kutokamilika kwa maabara za sayansi katika shule za sekondari Mabawe na Ndomba zenye thamani ya shilingi 35,477,173 (2013/2014). Saba, Kutorejesha shilingi 2,260,000 (2014/2015) na shilingi 228,415,951 (2015/2016) zilizokopwa kutoka katika akaunti ya Amana.

Nane, Kutotumika kwa nyumba ya watumishi (2 in 1) katika zahanati ya Kabalenzi iliyogharimu shilingi 53,895,426 (2014/2015).

Tisa, Kutumika kwa kazi nyingine shilingi 75,000,000 zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa eneo la kuegesha malori BENACO (2015/2016). Kumi, Kutothibitika matumizi ya mafuta ya thamani ya shilingi 1,204,060/= katika vitabu vya magari (logbooks) (2015/2016). Na mwisho, Kutopatikana kwa hati za malipo zenye thamani ya shilingi 76,163,888 (2015/2016).

Pamoja na mapungufu mengine katika kuhitimisha kikao hicho Mkuu wa Mkoa Kijuu alitoa maagizo yafuatayo; Halmashauri zote za mkoa wa Kagera zihakikishe kuwa hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwa ajenda ya kudumu katika vikao mbalimbali vya Halmashauri za Wilaya.

Halmashauri za Wilaya zihakikishe zinatumia Mfumo wa Kielektroniki katika kukusanya mapato ya Halmashauri na kuhakikisha mifumo hiyo inatumika na kusimamiwa kiamilifu pia Halmashauri ziepuke kuwatumia Mawakal katika kukusanya mapato ya Serikali na kuwatumia Watumishi na fedha zinapokusanywa zisitumike bila kuwasilishwa benki.

Halmashauri za Wilaya ziwaalike Watendaji mbalimbali wa Serikali mfano TANESCO, TARURA, na wengine katika vikao mbalimbali vya Halimashauri kama Mabaraza ya Madiwani ili kupata taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Halmashauri husika.

Halmashauri zote za Mkoa wa Kagera zihakikishe zinatekeleza agizo la Serikali la kupeleka asilimia 10 ya mapato yake kwa vikundi vya Akinamama, Vijana na Walemavu na kuhakikisha vikundi hivyo vinasimamiwa na  vinakuza mitaji yake na kuondokana na umasikini.

Mwisho Mhe. Kijuu alitoa rai kwa wananchi wote wa mkoa wa Kagera hasa Halmashauri za Wilaya kuchangamkia fursa mpya ya utalii ambayo imeapatika sasa baada ya Serikali kuyatangaza Mapori ya Biharamulo, Burigi na Kimisi kuwa hifadhi za Taifa. Fursa hizo ni pamoja kujenga Mahoteli ya Kitalii, Kujifunza Uongozaji wa Watalii, Vituo mbalimbali vya Utamaduni vya Kitalii pamoja na mengineyo mengi.

 

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.