• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Bibi Restuta Tibalila Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Bukoba Akifungua Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Mkoani Kagera

Posted on: May 4th, 2018

Waandishi wa Habari Wakumbushwa Kuzama Chini Kwenye Jamii Kuandika Habari za Wananchi Zenye Vyanzo Sahihi

Waandishi wa Habari Mkoani Kagera wakumbushwa kwenda kwa wnanchi katika ngazi za chini kabisa hasa vijijini kuona matatizo ya wananchi na kuyaibua kwa kuandika habari zao zitakazolenga kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao na kuwatoa sehemu moja na kupiga hatua ya maendeleo kuliko kuandika habari za mijini tu ambazo zimezoeleka.

Hayo yalisemwa na Bibi Restuta Tibalila Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukoba alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Bukoba  Mhe. Deodatus Kinawilo katika ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya  Habari ambayo huadhimishwa  kila mwaka Mei 3 ambapo  Waandishi wa Habari Mkoani Kagera walijumuika na wenzao Duniani kuadhimisha siku hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Bukoba Coop Manispaa ya Bukoba .

Katika hotuba yake Mkuu wa Wilaya ya Bukoba iliyosomwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya alivipongeza vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari Mkoani Kagera kwa kuchangia sehemu kubwa ya maendeleo ya mkoa kwa kuandika habari ambazo zinaelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali yanayolenga kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na mkoa kwa ujumla.

Vilevile Mkuu wa Wilaya Bukoba katika hotuba yake aliwashukuru wamiliki wa vyombo vya Habari kuendelea kufanya uwekezaji katika Vyombo vya Habari na masuala ya habari kama kuanzisha Redio za Kijamii na magazeti ambapo vinachangia sehemu kubwa kwa wananchi kupata habari mbalimbali zinazohusu mkoa wao na kwa wakati.

Aidha, Mkuu wa Wilaya katika hotuba yake aliwahakikishia Waandishi wa Habari kuwa Serikali Mkoani Kagera itaendelea kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari ili vitimize wajibu wake pia Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu  ili wananchi ambao ni walaji wapate habari sahihi na zenye uhakika.

Katika Maadhimisho hayo yaliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Kagera pia walialikwa wadau mbalimbali ambao walishirikiana na waandishi wa Habari na Wamiliki wa Vyombo vya Habari kujadili na kuchambua mada isemayo  “Uhuru wa Habari ni Chachu ya Uwajibikaji kwa maendeleo ya Mkoa.”

Wadau wakichangia mada hiyo waliwashauri Waandishi wa Habari kuhakikisha wanaandika habari zenye vyanzo vyenye uhakika na zenye maslahi mapana na jamii ili kubadili mtazamo wa jamii kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine ya maendeleo.

Pia  Waandishi wa Habari walishauriwa kuhakikisha wanazama chini katika jamii kuandika habari za wananchi wa kawaida au kuandaa vipindi ambavyo vinawagusa wananchi wa chini kabisa ambao wangependa kuona mabadiliko chanya katika maisha yao kwa kuelimishwa kupitia vyombo vya habari.

Chanagamoto kubwa waliopewa waandishi wa Habari ni kujiendeleza kielimu ili kuhakikisha wanankuwa na ufahamu wa kutosha na masuala mbalimbali ambayo wanayaandika au kuandaa vipindi juu ya masuala hayo pia kuendana na matakwa ya Sheria ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016.

Kwasasa Mkoa wa Kagera unavyo vituo vya  redio vipatavyo tisa, Kasibante, Fadeco, Karagwe, Shinuz, KCR, Vision, Kwizera, Bukoba na redio Mbiu. Pamoja na Redio nyingine nyingi ambazo zinasikika katika Mkoa wa Kagera zikirusha matangazo yake kutoka nje ya mkoa.

Pamoja na Redio kuna magazeti, mitandao ya kijamii, Cable TV, ambavyo vinautangaza mkoa wetu wa Kagera na kuwapasha wananchi wake kupitia Waandishi wa habari ambao wametapakaa mkoa mzima wakiandika habari mbalimbali za michezo, kuichumi, kijamii, Elimu, Utalii, Uwekezaji na nyinginezo nyingi.

Siku ya Mei 3 ilitangazwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya  Habari Duniani. Siku ya Uhuru wa Vyombo vya  Habari Duniani huongeza ufahamu wa umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari na kuikumbusha Serikali wajibu wake wa kuheshimu na kuhakikisha haki ya uhuru wa kujieleza inaheshimika  chini ya Ibara ya 19 ya Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu la 1948. Pia katika Siku hiyo Hukumbukwa Waandishi waliotangulia Mbele za Haki.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.