• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Hatimaye Kongamano la Wiki ya Uwekezaji Lafungwa Rasmi Kagera Kuwa Kitovu Cha Biashara Afrika Mashariki na Kati

Posted on: August 16th, 2019

Kongamano la Wiki ya Uwekezaji Kagera lafungwa rasmi na Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara  Mhandisi Stella Manyanya mara baada ya wanazuoni, wataalamu wa mambo ya uchumi, wafanyabiasha na wajasiliamali mbalimbali  kukaa kwa siku mbili mfurulizo kuchambua kwa kina fursa za uwekezeji mkoani  Kagera na kutoka na maazimio makuu sita ya kuufanya mkoa wa Kagera kukua kiuchumi.

Akifunga rasmi kongamano hilo Naibu Waziri Mhandisi Manyanya aliwakumbusha wanankagera wote sasa kuwa tayari kwa kila hali kuwapokea wawekezaji kwasababu mkakati wa kutangaza fursa uliondaliwa na uongozi wa Mkoa ukiongozwa na mkuu wa Mkoa katika Wiki ya Uwekezaji Kagera umefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana.

“Kama mkakati huu utatekelezwa vizuri na kwa umakini mkubwa utakuza zaidi pato la mwananchi wa Kagera pato la mkoa na taifa kwa ujumla, wakati ni huu wananchi sasa amkeni msiogope fursa zimebainishwa hasa katika kitabu cha mwongozo wa uwekezaji Kagera alichozindua juzi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.” Alisisitiza Naibu Waziri Mhandisi Manyanya.

Naibu Waziri Mhandisi Manyanya aliendelea kusisitiza kuwa Kagera  imefanikiwa kwani pamoja na fursa zilizopo za kuzungukwa na nchi jirani lakini pia gharama za kwenda huko ni ndogo sana ukilinganisha mfano kutoka Bukoba kwenda mkoani Ruvuma ni zaidi ya kilomita 2000 lakini ni nafuu kwenda nchi jirani ukitokea hapa Bukoba ambayo ni fursa ya gharama ndogo ya kusafiri au kusafirisha bidha.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti Mwenyekiti wa Wiki ya Uwekezaji Kagera akitoa taarifa fupi kwa Mgeni rasmi  Naibu Waziri Mhandisi Stella Manyanya kabla hajafunga rasmi Kongamano la Uwekezaji Kagera alisema kuwa dhumuni kubwa la Wiki hiyo lilikuwa ni chagizo la kuona fursa mbalimbali zilizopo mkoani Kagera kupitia sekta zote muhimu.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti alisema kuwa Wiki ya Uwekezaji Kagera imefnikiwa kwa kiwango kikubwa na iliandaliwa kwa sura kuu tatu kwanza maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wadau mbalimbali katika mkoa wa Kagera. Pili, kongamano ambalo lililowakusanya wanazuoni wabobezi kuchambua na kuchanganua fursa za uwekezaji na mwisho ni wadau wa uwekezaji kutembelea vivutio mbalimbali vya uwekezaji mkoani Kagera.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti aliwashukuru wananchi wote wa Kagera na wadau mbalimbali walioshiriki katika kufanikisha Wiki ya Uwekezaji bila kuvisahau vyombo vya habari mbalimbali vya ndani na nje ya mkoa lakini pia waandishi wa habari kwa kuitangaza Wiki ya Uwekezaji Kagera na kuwahabarisha wananchi juu ya nini kilikuwa kinafanyika katika wiki hiyo.

Mara baada ya Kongamano la Wiki ya Uwekezaji Kagera wadau wote waliafikia maazimio makuu sita ili kufanya ufuatiliaji kila baada ya miezi mitatu na kuhakikisha adhima ya uwekezaji Kagera inafikiwa; Kwanza; Taratibu zifanyike ili mkoa wa Kagera upewe hadhi ya kuwa “Special Economic Zone” (SEZ) kwasababu Kagera ni lango la kibihara kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Pili, Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zianzishe dawati la kuratibu utekelezaji wa mwongozo wa uwekezaji mkoa wa Kagera mwaka 2019. Tatu, Uwekezaji ufanyike katika mifumo rasmi ya ndani na mipakani (Rusumo, Kabanga, Mtukura na Murongo) ili kurahisisha biashara ndani ya mkoa na nchi jirani.

Nne, Mkoa kwa kushirikiana na umoja wa wafanyabiashara mkoani utakuwa na vikao vya mara kwa mara kuweka mikakati ya kuvutia mitaji na masoko toka ndani na nje ya nchi. Tano, Uongozi wa Mkoa uendelee na juhudi za kuimarisha stadi za fedha na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wafanyabiashara na wananchi juu ya umuhimu wa kushirikiana kupata mitaji na usimamizi wa fedha.

Mwisho wafanyabiashara wa Mkoani Kagera kufanya ziara katika nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Congo DRC, na Kenya ili kuona fursa za uwekezaji au biashara zilizopo katika nchi hizo ili kuona namna wanavyoweza kunufaika na fursa hizo kwa kupeleka bidhaa mbalimbali huko.  

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.