• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Hatuna Changamoto ya Fedha za Malipo ya Awali Kwa Wakulima wa Kahawa Napita Kuona Msimu Unaendeleaje – RC Gaguti

Posted on: September 3rd, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti afanya ziara katika wilaya tatu kukagua msimu wa kahawa wa 2019/2020 unavyoendelea hasa lengo kuu likiwa ni kuona wakulima kama wanalipwa fedha zao kwa wakati bila ucheleweshwaji na kama kuna changamoto zozote ziweze kutatuliwa.

Septemba 3, 2019 Mhe. Gaguti akiwa katika Chama cha Msingi Muungano na Nkwenda Wilayani Kyerwa akiongea na wananchi na wakulima wa kahawa alisema kuwa taarifa alizonazo na anazozipokea kila siku ni kuwa Vyama Vikuu vya Ushirika vya KDCU LTD na KCU 1990 LTD havidaiwi na Vyama vya Msingi kwa hiyo hakuna sababu ya malipo ya kwanza kwa wakulima kucheleweshwa.

“Ukiondoa wakulima ambao walipeleka kahawa zao kwenye vyama vya msingi ndani ya siku saba hadi kumi kufikia leo tarehe 3 Septemba, 2019 wakulima wote hakuna anayedai kwani fedha zipo za kuwalipa, taarifa nilizonazo hakuna mkulima yeyote anayedai fedha za mwezi wa saba mwisho wa kulipa ilikuwa ni tarehe 23.08.2019.” Alifafanua Mkuu wa Mkoa Gaguti

Katika Vyama vya Msingi  vya Muungano, Nkwenda Wilayani Kyerwa na Kamahungu Wilayani karagwe akiongea na wakulima Mhe. Gaguti alitoa nafasi kwa wakulima wanaovidai Vyama vya Msingi malipo ya kwanza ya muda mrefu kujitokeza ili ajue tatizo ni nini. Katika mikutano hiyo wakulima waliojitokeza ni wale ambao walipeleka kahawa zao kwenye vyama vya msingi mwishoni mwa mwezi wa Agosti, 2019 na malipo yao tayari yapo kwa taratibu za kulipwa tangu tarehe 3/08/2019.

Aidha, Mhe. Gaguti alimchukulia hatua za kinidhamu mkulima  mmoja wa Chama Msingi  Kamahungu Wilayani Karagwe kwa kumdanganya kuwa anadai chama hicho fedha zake tangu mwezi Julai 2019 ambapo alipohakiki katika vitabu vya chama hicho alikuta kuwa si kweli mkulima yule aliuza kahawa yake mwezi Julai bali  mwishoni mwa mwezi Agosti 2019.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa bado hajaridhishwa na matumizi ya ushuru unaokatwa kwenye kahawa ya wakulima na Vyama vya Msingi ambapo alisema kuwa tayari analifanyia kazi suala hilo kuona ushuru huo unapunguzwa na mkulima anapata fedha zaidi maana fedha hiyo inatumika bila ridhaa ya wakulima wa Vyama vya Msingi bali viongozi vinatumia fedha hizo na kutoa taarifa kwa wakulima jambo ambalo si sawa.

Katika suala hilo Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa angependa kuona fedha za ushuru zinaboresha kwanza Vyama vya Msingi kuliko kwenda kwenye matumizi mengine. Fedha hizi zingeweza kununulia mizani ya kidigitali ambayo itaondoa utata katika upimaji wa kahawa ya mkulima, pili fedha hiyo inunue vifaa vya kupima unyevunyevu katika kahawa ili mkulima asiendelee kukatwa kilo moja ya unyevu kwenye kahawa yake.

“Hili tunalifanyia kazi na nitaunda timu ya wataalam ili kuhakikisha changamoto zote hizo katika zao la kahawa linapatiwa ufumbuzi na mkulima kuneemeka na jasho lake.” Alisistiza Mkuu wa Mkoa Gaguti. Katika Wilaya ya Missenyi Mhe. Gaguti alitembelea vitalu vya kuzalisha miche ya kahawa ambapo lengo ni kuinua uzalishaji katika Wilaya hiyo.

Katika msimu wa mwaka huu wa kahawa wa 2019/2020 tayari Vyama Vikuu vya Ushirika vya KCU 1990 LTD na KDCU LTD mkoani Kagera vimekusanya zaidi ya kilo milioni 35 sawa na asilimia 75 ya kahawa inayotarajiwa kukusanywa katika msimu mzima na zaidi ya shilingi bilioni 35 tayari zimelipwa kwa wakulima. Aidha, makisio ya ukusanyaji katika msimu huu ni kukusanya kilo milioni 52

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.