• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Hifadhi ya Brigi-Chato Sasa Kumekucha ni Baada ya Mfalme wa Pori Kupokelewa na Familia Yake Kutawala Eneo Hilo

Posted on: February 7th, 2020
  • Je Wajua Kuwa Nusu ya Simba Wote Duniani Wapo Tanzania?

Brigi- Chato kumekucha sasa  Mfalme wa Pori  (Simba) na familia yake awasili katika hifadhi hiyo ya Taifa  ili kutawala eneo hilo muhimu la utalii katika ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa Tanzania. Ni ukoo mmoja wa simba 20 ukiwa na simba wazima 17 na simba watoto 3 wapokelewa  katika lango la Nyungwe Hifadhi ya Taifa ya Brigi-Chato Februari 6, 2020 na Mkuu wa Mkoa  wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti.

Katika Simba hao 20 Baba anaitwa Brigi na mama anaitwa Chato wakiwa na familia yao ya simba wengine 18 waliwasili Nyungwe katika Hifadhi ya Brigi-Chato majira ya saa 5:00 asubuhi wakisafirishwa kutoka katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara na dhumuni la kuwaleta simba hao ni kuhakikisha hifadhi ya Brigi- Chato inakuwa na wanyamapori  wote hasa wale wakubwa watano ili kuvutia zaidi utalii.

Kwaniaba  ya wananchi wa Mkoa wa Kagera na Geita mara baada ya kuwapokea Simba hao 20 wakiongozwa na baba Brigi na Mama Chato Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa neno  la kumshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kuamua  kuanzisha Hifadhi ya Taifa Brigi-Chato katika ukanda wa Kaskazini Magharibi  ili kufufu upya uchumi wa mikoa ya Kagera na Geita kupitia utalii.

“Sisi wananchi wa Kagera tunayo furaha sana kuwapokea Simba hawa kwani katika eneo hili uchumi wetu utakua kwa kasi, lakini nimshuru tena Mhe. Rais Magufuli  kwa maamuzi yake sahihi kuanzisha hifadhi hii kumesaidia sana, hakuna asiyejua kuwa miaka ya nyuma kulikuwa na hatari sana katika maeneo haya ya Brigi kwa majambazi kutumia hifadhi hii kuteka wananchi l pia kuendesha vitendo vya kiharamia lakini sasa hakuna tena.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwashukuru pia uongozi wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kuamua Hifadhi ya Serengeti itoe Simba 20 ili waletwe katika Hifadhi ya Taifa ya Brigi-Chato ambapo aliwahaidi yeye kwakushirikiana na wananchi wa mkoa wa Kagera watahakikisha kuwa hakutakuwepo na changamoto zozote zitakazojitokeza ambazo ziliwahi kujitokeza katika Hifadhi nyingine za Taifa.

Kamishina  wa Uhifadhi  Martin Loibooki ambaye ni  Mkuu wa Kanda ya Magharibi kwaniaba ya Kamishna Mkuu Dkt.  Allan Kijazi akieleza sababu za kuhamisha simba 20 kutoka Serengeti kuja Brigi-Chato alisema kuwa katika hali ya kawaida kuna wanyama wanaokula nyasi na kuna wanayama kama simba wanakula nyama au wanakula wanyama wezao na hilo linasaidia katika ekolojia ya wanyamapori .

Kamishna Loibooki alisema pia katika Hifadhi ya Taifa ya Brgi-Chato siyo mara ya kwanza hifadhi hiyo kuwa na Simba na ndiyo maana kuna maeneo katika hifadhi hiyo  yanajulikana kwa jina la Mllima wa Simba lakini kutokana na shughuli za kibinadamu na uvamizi wa hifadhi hizo simba waliweza kutoweka kwa kuuawa na binadamu ili wasidhurike na ndiyo maana simba wakatoweka.

Naye Dkt. Denis Itanda Mtafiti Mkuu wa wanyamapori aliyeongoza jopo la Madaktari na wataalam kuhakikisha simba 20 kwanza wanakamatwa kule Serngeti wananwekwa kwenye vitenga na kusafirishwa salama hadi katika Hifadhi ya Brigi-Chato alisema kuwa Tanzania ina (simba 15000 waliopo ndani ya mipaka ya Tanzania) nusu  ya Simba wote duniani jambo  ambalo ni la lakujivunia pia nchi ya pili kwa wingi wanyamapori  duniani.

Dkt, Denisi alisema kuwa Hifadhi ya Taifa  ya Serengeti  ndiyo hifadhi yenye Simba bora duniani na katika miaka mitano Simaba wameongezeka kwa kiwango kikubwa baada ya Serikali kuamua kupambana na ujangiri na uwindaji haramu katika hifadhi zote nchini na ndiyo maana Serikali imeamua kuhamisha Simba 20 kuja katika hifadhi za Brigi-Chato.

Simba hao 20 tayari wamewekewa vifaa maalum vya kuhakikisha kila mara walipo kama ni salama lakini pia vifaa hivyo vitasaidia kuwaongoza watalii kujua Simba hoa wapo wapi kwa siku husika ili wakawaone kirahisi.  Dkt. Denisi anasema kuwa mara baada ya simba 20 kufikishwa eneo wanalotakiwa kuachiwa watawekwa kwenye uzio na kuwa chini ya uangalizi wa wataaalam kwa wiki mbili na baadae watakuwa wanaachiwa wachache wachache.

Kwaniaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. More Msua Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori alimshukuru Mkuu wa Mkoa Kagera kukubali kuwapokea Simba hao pia alimhakikishia Mkuu wa Mkoa huyo kuwa Wizara imejipanga kuhakikisha Wanyamapori  wakubwa watao (The Big 5) wataletwa katika Hifadhi ya Taifa ya Brigi-Chato ili kuhakikisha watalii wanapofika ktika hifadhi hiyo wanawaona wanyama hao wote.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo  Saada Malunde akishiriki katika zoezi la kupokea simba 20 alisema wananchi wa Biharamulo wapo tayari kuwalinda wanyamapori hao kwa kushirikiana na TANAPA ili Hifadhi ya Brigi-Chato iweze kushamiri. Hifadhi ya Brigi- Chato ina ukubwa  wa kilometa za mraba 470.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.