- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
Huduma za Madaktari Bingwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera zawafanya wananchi wengi wenye matatizo ya kiafya kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kagera kufurika katika Hospitali hiyo ili kupata huduma za Kibingwakutoka kw Madaktari Bingwa.
Katika uzinduzi rasmi wa utoaji wa huduma hizo za Kibingwa Novemba 6, 2018 Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera Dk. Felix I. Otieno alitoa taarifa kwa Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhandisi Richard Luyango ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba kuwa tangua zoezi lianze Novemba 5, 2018 siku ya Jumatatu tayari wagonjwa 858 walikuwa wamejiandikisha kuwaona Madaktari Bingwa wa magonjwa mbalimbali.
Aidha, Dk. Felix alisema kuwa tayari Madaktari Bingwa 27 walikuwa wamewasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwaajili ya kutoa huduma za kibingwa na siku ya kwanza ya Jumatatu Novemba 5, 2018 wagonjwa 429 walikuwa wamepatiwa huduma za Kibingwa katika vitengo vya kuhudumia magonjwa mbalimbali katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kuwaadaa baadhi ya wagonjwa kwajili ya upasuaji.
Akizindua rasmi zoezi la kutoa huduma za Kibingwa Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhandisi Richard Luyango ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Luyango aliwashukuru Madaktari bingwa 27 ambao tayari wamewasili katika Hospitali hiyo na kuanza kutoa huduma za Kibingwa na kusema kuwa huo ni uzalendo mkubwa waliuonesha wa kuwahudumia wananchi wa Kagera.
“Nawapongeza sana Madaktari Bingwa ambao mmefika hapa kuwahudumia wananchi wetu mmekuwa wazalendo kweli kweli kama mnavyowaona wananchi wetu hapa kuwa wanahitaji huduma zenu kwasababu ya matatizo ya kiafya waliyonayo. Wito wangu kwenu ninyi Madaktari Bingwa niwaombe muongeze siku mbili zaidi katika kutoa huduma kwani siku sita (tarehe 5 hadi 11 Novemba, 2018) hazitatosha ukiangalia wananchi waliohudhuria hapa.” Alisisitiza Mhandisi Luyango.
Pia Mhandisi Luyango aliwaomba wananchi ambao ni wagonjwa waliohudhuria katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kupata huduma za Kibingwa kuwa wavumilivu katika kupata huduma hizo kutokana na wingi wao na pia walitakiwa kusikiliza maelekezo wanayopewa na Wataalamu wa Afya ili kuwafikia Madaktari Bingwa kwajaili ya kupatiwa huduma.
Naye Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Projectus Rutabanzibwa aliwataka watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha katika kutoa huduma kwenye zoezi hilo na kusisitiza kuwa Serikali imetoa fedha nyingi kugharamia zoezi hilo kwa ajili ya kutoa Huduma za kibingwa kwa Wananchi wa Mkoa wa Kagera.
Kwa upande mwingine Daktari Bingwa Kiongozi wa timu ya Madaktari Bingwa wanaotao huduma za Kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera Dk. Samwel Rweyemamu ambaye ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo alisema timu yao ya Madaktari Bingwa inaendele vizuri na utoaji wa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera.
Dk. Rweyemamu alisema kuwa kwa upande wa magonjwa ya moyo siku ya kwanza Jumatatu Novemba 5, 2018 walikuwa wamehudumia wagonjwa watu wazima 60 lakini siku ya pili ya Jumanne Novemba 6, 2018 huduma za Kibingwa kwa upande wa magonjwa ya moyo zilikuwa zikitolewa kwa watoto ambao nao ni wengi. Aidha, Dk. Rweyemamu alisema tayari wagojwa 10 walikuwa wameshauriwa kwenda katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kutokana na matatizo yao kuwa makubwa zaidi.
Nao wananchi ambao wamefurika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera walikiri mbele ya Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Mhandisi Richard Luyango ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba kuwa wanaishukuru Serikali kwa kuwasogezea huduma za Kibingwa karibu. Pia krahisisha namna ya kuwaona Madaktari Bingwa ukilinganisha na kuwafuata katika vituo vyao vya kazi pamoja na gharama za malazi na chakula.
Katika kutekeleza zoezi hilo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ikishirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera wamejipanga vizuri kuhakikisha huduma za Kibingwa zinatolewa kwa uhakika ambapo wananchi wenye kadi za Bima Hawatozwi chochote bali wanalipia gharama zao kupitia kadi hizo lakini mfumo wa kukusanyia mapato unatumika kuhakikisha fedha ya Serikali inakusanywa kwa usahihi ili kukuza mapato ya Hospitali hiyo.
Ikiwa ni mara ya pili zoezi la huduma za Madaktari Bingwa kutolewa Mkoani Kagera mwaka 2017 jumla ya wagonjwa 3,146 walihudumiwa na mwaka huu 2018 huduma hizi zinalenga kuwahudumia wagonjwa 4,000 hadi 5,000 kwa magonjwa ya Uzazi na kizazi kwa wanawake, Magonjwa ya upasuaji kwa Ujumla, Magonjwa ya njia ya mikojo ikiwemo tezi Dume, Magonjwa ya pua, sikio na koromeo.
Magonjwa mengine yatakayoshughulikiwa na Madaktari Bingwa ni pamoja na Magonjwa ya mifupa, Magonjwa ya moyo, Magonjwa ya ndani ikiwemo sukari na figo, Magonjwa ya watoto, Magonjwa ya Afya ya kinywa na meno, Magonjwa ya macho, Magonjwa ya Ngozi, Magonjwa ya afya ya akili, na Saratani ya Mlango wa kizazi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.