• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba Mhe. Salvatory Bongole Akitoa Hotuba Yake Katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Mkoani Kagera

Posted on: February 1st, 2018

Mkoa wa Kagera Waadhimisha Kilele Cha Wiki ya Sheria Kwa Wadau Kuchambua Ufanisi wa Matumizi ya Tehama Katika Mahakama

Mkoa wa Kagera waadhimisha kilele cha wiki ya Sheria  kwa wadau mbalimbali kuchambua, kutoa ufafanuzi  na uelewa kwa wananchi juu ya kaulimbiu ya mwaka huu isemayo “Matumizi ya TEHAMA Katika Utoaji Haki kwa Wakati na Kuzingatia Maadili”

Akitoa salamu za Serikali Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu wakati wa kilele cha wiki ya Sheria katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba alisema kuwa ni Muhimu sana Mahakama kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuwafanya wananchi wasipoteze muda mwingi Mahakamani badala yake watumie muda huo kufanya shughuliza kiuchumi.

Mhe. Kijuu aliwaomba Viongozi  wa dini kuendelea kuhubiri amani katika nyumba za ibada ili wananchi waendelee  kuwa na upendo na kudumisha amani na kuacha vurugu za kupelekana Mahakamani  ili zibakie kesi au mashauri ya msingi tu na yashughulikiwe na kumalizika kwa wakati.

Pia  Mhe. Kijuu alitoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi  pia kuheshimu maamuzi ya Mahakama na waache tabia za kukata rufaa za kesi zilizoamuliwa kihalali jambo ambalo linazifanya Mahakama kuwa na msongamano wa kesi na kuchelewesha maamuzi kwa kesi ambazo tayari zilishaamuliwa.

Aidha, Jaji Mfawidhi wa Mahakama  Kuu Kanda ya Bukoba Mhe. Salvatory Bongole alisema kuwa Mpango Mkakati mkuu uliowekwa na  Mahakama wa mwaka 2016 hadi 2020 umejikita katika shabaha kuu sita za TEHAMA Katika Mahakama. Shabaha ya kwanza ni kufunga au ujenzi wa miundombinu ya TEHAMA katika Majengo ya Mahakama.

Pili ni kuwa na Mahakama ya Kielektroniki  (E-Judiciary), Tatu kuwa na mtoa huduma mmoja wa internet ambaye ataziunganisha Mahakama zote nchini, Nne ni kununua vifaa vya Video Conferencing pamoja na mobile recording system kwa Mahakama zilizochaguliwa, Tano kuanzisha mfumo wa kuratibu nyaraka za kielektroniki,  Sita kuanzisha mfumo utakaoratibu raslilimali za Mahakama.  Jaji Bongole alisema kuwa shabaha zote sita zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji kwa sasa.

Naye Mwanansheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Kagera Hashim Ngole alisema kuanzishwa kwa TEHAMA katika Mahakama kutaleta faida nyingi ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa kushughulikia mashauri mahakamani na kupunguza matumizi makubwa ya karatasi (Paper work), Kurahisisha utumaji wa taarifa kwa wakati na kwa kipindi maalum.

Mhe. Ngole pia alisema kuwa TEHAMA katika Mahakama itarahisisha utaratibu wa kurekodi mienendo ya mashauri Mahakamani kwa kumbukumbu sahihi za baadae kuliko ilivyo sasa. Pia Kuwafanya mashahidi wa kesi kutoa ushahidi mahala papote walipo kwa njia ya Video Conference kuliko ilivyo sasa kuwa lazima shahidi afike mahakamani.

Faida nyingine zilizotajwa za kuanzisha TEHAMA katika Mahakama ni Mawakili kuwawakilisha wateja wao mahakamani bila wao kuwepo, kupunguza mianya ya rushwa Mahakamani. Hukumu, machapisho na sheria mbalimbali kupatikana kwa urahisi katika mitandao ili kuwasaidia Mawakili katika kuendesha mashauri Mahakani.

 Katika Hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society) Mkoa wa Kagera Wakili Aron Kabunga alishauri kuwa ili kuifanya Mahakama kuwa ya Kielektroniki lazima baadhi ya vifungu vya sheria virekebishwe ili kuruhusu matumizi ya TEHAMA kuwa na ufanisi katika Mahakama.

Vilevile Wakili Kabunga alisisitiza kuwa na tahadhari kubwa kuhusu madhara ya TEHAMA kama udukuzi wa nyaraka kwa njia za mitandao, Vifaa kama kompyuta kuingiliwa na wadudu (Virus) au wataalamu  na kuharibu mfumo mzima na kupelekea nyaraka muhimu kama hukumu au ushahidi kupotea au kubadilishwa kwa matakwa ya upande mmoja.

Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Sheria Mkoani Kagera yaliadhimishwa katika Viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba na Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.