• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Kagera Kuibua Vipaji Vipya Katika Michezo Mbalimbali Umiseta 2019 Yafunguliwa Rasmi Kuunda Timu Bora ya Kunyakua Ushindi Kitaifa Mtwara.

Posted on: May 30th, 2019

Mashindano ya Michezo kwa wananfunzi wa shule za Sekondari UMISETA Mkoa Kagera yafunguliwa rasmi ili kuibua vipaji katika michezo mbalimbali na kuunda timu ya mkoa itakayokwenda kuuwakilisha mkoa katika mashindano hayo  ngazi ya Taifa mkoani Mtwara.

Akifungua mashindano hayo kwaniaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Bw. Isaya Tendega Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji aliwataka wananfunzi wanaounda kambi hiyo kucheza kwa nidhamu kubwa na kuonesha vipaji vyao wakifuata maekezo ya walimu wao ili kuunda timu imara na bora itakayoleta ushindani katika mashindano hayo Kitaifa.

Bw. Tendega aliwataka wanafunzi hao kuwa wazalendo, kwa kuwa wakakamavu, waadilifu kuwa na nidhamu pia uzalendo wanaposhiriki mashindano hayo kwani michezo si ugomvi bali ni upendo na kucheza kwa upendo ndipo kipaji cha mchezaji huonekana vyema zaidi. Pia aliwaasa waamuzi wa michezo yote kuamua bila upendeleo ili kupata vipaji vinavyolengwa vitakavyouwakilisha mkoa vyema kitaifa.

Aidha, katika hotuba yake Katibu Tawala wa Mkoa Profesa Faustin Kamzora aliwaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha idara za michezo katika Halmashauri zao zinawezeshwa kwa vifaa na fedha ili kuendeshea michezo na kukuza vipaji katika mkoa wa Kagera kwani hivi sasa michezo ni ajira.

“Michezo imewasaidia vijana wengi kuepukana na mdawa ya kulevya kama bangi, mirungi, cocaine na mengineyo lazima tuitilie mkazo sana ili vijana wetu wasiharibikiwe. Pili kumbukeni kuwa Michezo ni ajira mfano katika mkoa wetu tunaye mwamuzi wa mpira wa miguu tena mama anachezesha liku ligi kuu ya Tanzania ni kwasababu aliichukulia michezo kwa kipaumbele na amepata ajira ya kudumu sasa.” Alisisitiza Bw. Tendega kwaniaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera.

Aidha, Bw. Kepha Elias Afisa Michezo Mkoa wa Kagera ambaye ni meneja wa kambi ya UMISETA katika Shule ya Sekondari Nyakato Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba alisema kuwa kuna jumla ya wananfunzi wanamichezo 640  wavulana wakiwa 341 na wasichana 306  na wanamichezo hao wanashiriki katika michezo ya soka, fani za ndani, kwaya, mpira wa wavu, mpira wa pete, mpira wa mikono na riadha.

Naye Bw. Mbaraka Maya aliyemwakilisha Afisa Elimu Mkoa katika ufunguzi huo wa mashindano ya UMISETA mkoa wa Kagera alisema kuwa Maafisa Elimu wote wa Wilaya wapo katika kambi hiyo ya Shule ya Sekondari Nyakato kusimamia nidhamu ya wanafunzi wanamichezo ili kupata timu bora ya mashindano hayo itakayoleta changamoto katika michezo mbalimbali Kitafa mkoani Mtwara.

Ikumbukwe kuwa Mashindano ya michezo kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari UMISETA na Shule za Msingi UMITASHUMTA yaliwahi kusitishwa mwaka 2000 na Waziri aliyekuwa na dhamana ya Michezo wakati huo wa Awamu ya Tatu Mhe. Joseph Mungai na yalirejeshwa kwa majaribio mwaka 2007 na Mhe. Magreth Sitta akiwa waziri mwenye dhamana ya michezo wakati huo.

Mashindano hayo kwa shule za Sekondari UMISETA na Msingi UMITASHUMTA yaliporejeshwa tena mwaka 2007 na yalifanyika majaribio kwa Mikoa mitatu tu ya Dar es Salaam, Morogoro na Tanga na yalifanyikia Kibaha Mkoani Pwani. Aidha, Serikali iliamua kuyarejesha rasmi mashindano hayo mwaka 2009 kwa waraka namba 1 wa mwaka 2009.

Katika Mkoa wa Kagera Mashindano ya wanafunzi kwa shule za Sekondari UMISETA yanafanyika katika Shule ya Sekondari Nyakato Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ambapo yalianza Mei 25, 2019 na  yanatarajia kukamilika Juni 7, 2019.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.