- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
Kampuni ya Kahama Fresh inayomiliki Kiwanda cha kusindika maziwa na shamba la mifugo imeunga mkono Programu ya BBT(Building Better Tomorrow) kwa kutoa ng'ombe wa maziwa (mitamba) watano (5) kwa kikundi cha vijana 17 ili kuwawezesha kujishughulisha na uzalishaji wa maziwa na kujiongezea kipato
Wakikbidhi ng’ombe hao katika shamba la mifugo la kampuni hiyo lililopo wilayani Karagwe, Mkoani Kagera, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalla Ulega amempongeza Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Bw. Josam Ntangeki kwa kuunga mkono kwa vitendo.
"Nampongeza Ndugu Josam kwa kuunga mkono Programu hii ya BBT kwa kuwakopesha ng'ombe wa maziwa vijana wetu kupitia mpango wa Kopa Ng'ombe Lipa Maziwa ili kuwawezesha vijana wetu kuzalisha maziwa kwa wingi na kuyapeleka katika viwanda vya uchakataji wa maziwa kikiwemocha Kahama Fresh", alisema Mhe. Ulega
Ameeleza kuwa programu hiyo ya BBT haiwezi kuendeshwa na Serikali pekee bila ya wadau wa maendeleo hivyo Kampuni ya Kahama Fresh wameonesha mfano na kuwahimiza wadau wengune kuendelea kujitokeza kuunga mkono Programu hiyo ili kwa pamoja kuleta mabadiliko katika sekta za uzalishaji
Aidha, Mhe. Ulega aliwakikishia wadau wote kuwa wataendelea kushirikiana nao ili programu hiyo ya BBT kielelezo cha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iweze kushamiri na vijana wengi waweze kupata fursa za kujiajiri
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw. Josam Ntangeki ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwapa fursa ya kuendesha shughuli zao huku akisema kuwa wametoa mitamba hiyo ili kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuwawezesha vijana kupata fursa mbalimbali za kujiajiri kupitia sekta za uzalishaji
Kahama imetoa ng'ombe hao kupitia programu Kopa Ng'ombe Lipa Maziwa unaotekelezwa na Shirika la kimataifa la Heifer International kupitia mradi wa kuboresha sekta ya maziwa (TI3P) kwa Kanda ya Ziwa na Zanzibar unaofadhiliwa na Taasisi ya Bill and Melinda Gates (BMGF) kupitia Benki ya Maendeleo ya kilimo nchini (TADB).
Tukio hilo la utoaji ng'ombe watano kwa vijana ni sehemu ya uzinduzi wa mpango wa ukopeshaji ng'ombe Mia Sita (600) watakaotolewa na TADB kupitia programu ya Kopa Ng'ombe Lipa Maziwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.