- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Avikagua Vyama Vikuu Vya Ushirika Kuona Utayari wa Kukusanya Kahawa ya Wakulima Msimu Unapofunguliwa Juni Mosi 2018
Mkoa wa Kagera ukiwa mzalishaji mkubwa wa zao Kahawa nchini kwa zaidi ya asilimia 50 sasa wafanya maandalizi ya kufungua msimu wa mwaka huu 2018 wa ununuzi wa Kahawa kwa wakulima kupitia Vyama Vikuu vya Ushirika vya Kagera Cooperative Union 1990 Limited (KCU 1990 LTD) na Karagwe District Co operative Union Limited (KDCU LTD)
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu katika kuhakikisha agizo la Serikali la Wakulima kuuza Kahawa yao kupita Vyama vya Ushirika linatekelezwa kikamilifu amevitembelea Vyama Vikuu vya Ushirika vya KDCU Ltd na KCU 1990 LTD kuona maandalizi ya kupokea kahawa hasa maghara ya kuhifadhi kahawa hizo pamajoa na viwnda vya kukoboa kama vipo tayari kufanya kazi msimu unapofunguliwa Juni 1, 2018.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu alitembelea na kukagua mashine za kukoboa kahawa katika kiwanda cha BUKOP na maghara ya kuhifadhi kahawa kiwandani hapo na ghara la Kemondo la KCU 1990 Ltd. Katika Mashine ya kukoboa kahawa BUKOP Mkuu wa Mkoa alijonea ukarabati wa mashine zilizomo katika kiwanda hicho zikifanyiwa ukarabati ili kuanza msimu wa ukoboaji
Katika Wilaya ya Karagwe Mkuu wa Mkoa alitembelea maghara ya Chama Kikuu cha KDCU Ltd pamoja na mashine ya kukoboa kahawa iliyokuwa ikifanyiwa ukarabati ambapo alipewa taarifa ya kiwanda hicho kudaiwa fedha za Ankara ya umeme na TANESCO ambapo alisema kuwa tayari Kamati ya Ulinzi na Usalama inalifanyia kazi suala hilo ili msimu ukifunguliwa mashine hiyo iweze kukoboa kahawa.
Katika Wilaya ya Kyewa Mkuu wa Mkoa alitembelea na kukagua maghara ya vyama vya Msingi vya Iteera na Karongo na kuridhika na maandalizi ya maghara hayo kupokea kahawa kwa msimu huu wa mwaka 2018 unaotarajiwa kufunguliwa Juni 1, 2018.
Akiongea na viongozi wa Vyama hivyo Vikuu vya Ushirika Mkoani Kagera Mhe. Kijuu alisema kuwa ni lazima mkoa usimamie agizo la Serikali, na lengo kuu la Serikali ni kuhakikisha wakulima wa kahawa wananufaika na kilimo chao cha kahawa bila kunyonywa. Aidha, alisistiza kuwa wakulima watapewa malipo ya awali na baada ya kahawa kuuzwa watalipwa malipo ya pili kulingana na bei ya soko la dunia.
“Najua wakulima wengi wana mashaka na mfumo mpya wa uuzaji wa kahawa kutokana na makovu waliyoyapataa huko miaka ya nyuma lakini Serikali sasa imeamua kuhakikisha wananufaika na kahawa yao kupitia Vyama vya Ushirika na ndiyo maana nimeamua kufuatilia kwa karibu. Hapa namsafishia njia Mhe. Waziri Mkuu ambaye anatarajia kuja Kagera kuhakikisha mkulima ananufaika na Kahawa yake.” Alisistaiza Mhe. Kijuu.
Maagizo;
Mara baada ya kukagua maghara na viwanda vya kukoboa kahawa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu aliwaagiza Viongozi wa Vyama Vikuu vya Ushirika vya KCU Ltd na KDU Ltd kwanza kuhakikisha maghara yanasafishwa kwa kiwango cha kuridhisha ili kupokea kahawa ya wakulima. Pili kuhakikisha mizani yote inafanyiwa uhakiki na Wakala wa Vipimo kabla ya kuanza kukusanya kahawa ili mkulima asipunjwe katika vipimo.
Tatu, kukamilisha ukarabati wa mashine za kukoboa kahawa kwa wakati ili mara kahawa ikianza kukusanywa isikwame kukoborewa na kusababisha kucheleweshwa kwenda katika soko la mnada wa dunia na kuchelewesha malipo ya pili ya mkulima.
Nne, Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya kuhakikisha hakuna kahawa inauzwa “Obutura” wala kutoroshwa kwenda nchi jirani kwa wafanyabiashara wanaonunua kwa njia ya magendo bila kusajilijiwa kihalali kama Vyama vya Ushirika vinavyotambulika.
Chama Kikuu cha KCU 1990 Ltd kinatarajia kukusanya tani 5,000 na zaidi za kahawa maganda katika msimu huu wa mwaka 2018. Aidha, KDU Ltd inatarajia kukusanya kahawa ya wakulima kiasi cha tani 40,000 na asilimia 90 ya kahawa hiyo itakuwa Robusta na Arabika asilimia 10, pia katika kahawa hiyo kutakuwa na kahawa ya masoko maalum (Organic Coffee) tani 4,000.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.