- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
“Kama kuna mwananchi, kundi la watu, baadhi ya wanachama wa Vyama vya Ushirika au kiongozi yeyote ana wazo la kukigawa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Karagwe na Kyerwa Development Co-operative Union Limited (KDCU LTD) ahame mara moja Mkoa wa Kagera au akafanye hivyo nje ya mkoa huu lakini sipo tayari kuona jambo hilo linatokea.” Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti akitoa onyo katika Mkutano Mkuu wa 32 wa KDCU LTD Kayanga Wilayani Karagwe.
Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa onyo hilo Machi 5, 2019 Wilayani Karagwe kwenye Mkutano Mkuu wa 32 wa KDCU LTD katika ukumbi wa CCM akiwa mgeni rasmi wakati akiongea na wajumbe wa Mkutano huo ambapo alisema kuwa tayari ameanza kusikia fununu za baadhi ya watu kutaka kukigawa chama cha KDCU LTD katika vyama viwili ambavyo vitawakilisha Wilaya za Karagwe na Kyerwa na kuonya kuwa jambo hilo haliwezi kutokea na halitakiwi kufikiriwa wala kujadiliwa.
Pia Mkuu wa Mkoa Gaguti alisistiza kuwa kwasasa anatamani Mkoa wa Kagera ungekuwa na Chama Kikuu cha Ushirka kimoja chenye nguvu na kuwahudumia wakulima lakini si kuwa na Vyama vya Ushirika vingi ambavyo vitauingiza mkoa katika migogoro na haviwezi kuwasaidia wakulima kuendeleza kilimo cha kahawa lakini pia kuwanufaisha wakulima na zao la kahawa ambalo linatakiwa kuwainua kiuchumi wananchi wa Kagera.
“Serikali itaendelea kuweka misingi na mikakati iliyo imara ili kuhakikisha kahawa inapata bei bora na fedha za wakulima kupatikana mapema ili mkulima asihangaike wakati tayari amekusanya kahawa yake katika Chama cha Msingi. Pia Serikali ingependa kuona zao la kahawa linaboreshwa zaidi na kuongeza uzalishaji mkoani Kagera kutoka uzalishaji wa sasa wa kilo milioni 58.9 hadi kilo milioni 100”. Alisistiza Mkuu wa Mkoa Gaguti
Katika hatua nyingine Mbunge wa Kyerwa Innocent Bilakwate akiongea na wajumbe wa Mkutano huo aliwaonya vionozi wa KDCU LTD kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa fedha za wakulima katika Vyama vya Msingi vya chama kikuu hicho kwani ambapo alisema alisema kuwa kwa utafiti wake baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wamehujumu au kutumia vibaya fedha za wakulima katika maeneo yao.
Jambo hilo lilimfanya Mkuu wa Mkoa Gaguti kuagiza Vyama vya Msingi vya Nyakatuntu, Kaina, na Kamuli kukamatwa mara moja na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa ubadhilifu wa fedha za wakulima na ifikapo Machi 6, 2019 saa 3:00 asubuhi awe amepata taarifa ni hatua gani zimechukuliwa kwa viongozi hao na kutoa rai kwa baadhi ya viongozi ambao wamejipanga kuhujumu mfumo wa ushirika kuwa Serikali itachukua hatua kali sana dhidi yao.
Katika msimu huu wa mwaka 2018/19 ulioanza mwezi Mei Mosi 2018 na utakamilika Aprili 30, 2019 Mkoa wa Kagera umekusanya na kuuza jumla ya kilo milioni 58.9 za kahawa na Chama Kikuu cha KDCU LTD kimekusanya asilimia 67% kahawa zote. Chama cha KDCU LTD kilikuwa kimeotea kukusanya tani elfu 40 na kufanikiwa kukusanya tani elfu 39 sawa na asilimia 98% na tayari chama hicho kimepata faida ya shilingi milioni 260.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.