- Home
- About Us
- Administration
- Districts
- District Councils
- Investment Opportunities
- Services
- Publications
- Media Center
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu mara baada ya kukamilisha majukumu yake ya Ukuu wa Mkoa hapo Jumatatu Agosti 6, 2018 kwa kukabidhi rasmi ofisi rasmi kwa mrithi wake Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti Jumanne Agosti 7, 2018 ametuaga na kuondoka rasmi kwenda kupumzika baada ya miaka 43 ya utumishi wa umma.
Baba Salum M. Kijuu kwaheri tunakutakia baraka, heri na fanaka na Mwenyezi Mungu akujalie maisha marefu wewe pamoja na familia yako. Imani yetu Wanakagera ni kuwa kwa kila ulichotoa kwaajili yetu Mungu atakulipa zaidi.
Mhe. Kijuu ulikuwa mlezi hasa sisi watumishi wa ofisi yako ulituongoza kwa kutuelekeza na kutufundisha kazi tutakumbuka daima. Uliwahudumia wananchi wote kila mmoja kutokana au kulingana na shida yake na kuhakikisha ufuatiliaji unafanyika mpaka mhusika shida yake inatatuliwa.
Mhe. Kijuu Wazee wanaolelewa katika Kituo cha Kiilima Halmashauri ya Wilaya Bukoba watakumbuka sana kwani kila wakati uliwapa kipaumbele sana kuhakikisha makazi yao yanaboreshwa na wanapata chakula kadri ya mahitaji yao, kauli yako kila mara ulisema lazima tuwaenzi wazee wetu kwani walitumikia taifa letu kwa uzalendo na kuwa kila mmoja anaelekea uzeeni. Kwaheri Mzee Kijuu.
Siyo Kituo cha Kiilima tu bali na Nyumba ya Wazee iliyopo katika Parokia ya Kashozi Jimbo Katoriki la Bukoba ulielekeza jengo lao lijengwe upya mara baada ya kwenda na kuliona kuwa lilikuwa halifai tena wazee kuishi baada ya kuathiriwa vibaya na Tetemeko la Septemba 10, 2016. Hukujali jengo linamilikiwa na nani bali tu kwasababu wanaishi wazee. Utakumbukwa sana na Wazeehao Mhe. Kijuu.
Nakumbuka kila mara katika ziara zako za kutembelea walengwa au wanufaika wa TASAF Awamu ya Tatu kila ulipomkuta mzee amefanya jambo la maendeleo kwa kutumia fedha za TASAFU ulitoa pochi yako na kumuongezeafedha na ulitoa mifano katika hotuba zako kuwa wazee wanafanya vizuri sana kwa kuzitumia fedha za TASAF. Tutakumuka Mhe. Kijuu.
Mwisho, uliyoyafanya ya kukumbuka ni mengi mno na si rahisi kuyataja yote na kuyamaliza bali tunakutakia mapumziko mema na sisi tunakuhaidi kuwa tutayaishi yale yote ulotuachia ili kukuenzi. Kweheri Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu Kagera kutabaki kuwa Nyumbani Kwako.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA
Telephone: 255 28 2220215/17
Mobile:
Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.