• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoani Kagera - Karagwe

Posted on: March 9th, 2017

KAGERA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUWAINUA WAJANE NA KUWAHIMIZA WAJASILIAMALI KUFIKIA TANZANIA YA VIWANDA

Mkoa wa Kagera waadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kuwatia moyo na kuwahimiza  wanawake wanaojishughulisha katika shughuli za ujasiliamali kuongeza juhudi kufikia lengo la Serikali la Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Aidha, wanawake wenyewe wamehamasishana kuwasaidia wenzao ambao ni wajane na wenye matatizo hasa ya kukosa makazi kutokana na sababu mbalimbali.

Maadhimisho hayo yaliadhimishwa kimkoa Wilayani Karagwe katika Mji mdogo wa Kayanga na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambayo huadhimishwa  Machi, 8 kila mwaka.

Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa Kijuu alimtembelea Mama Cineth Patrick katika eneo la Omulushaka ambaye ni Fundi Seremala na anamiliki kiwanda cha kutengeneza samani za kisasa zikiwemo sofa. Mama Cineth ameajili vijana wakiwemo wasichana ambao ni mafundi aliowafundisha kazi yeye mwenyewe na anashirikiana nao kutengeneza samani katika kiwanda chake.

Mama Cineth anasema mara baada ya kuhitimu ufundi wa uselemala katika Chuo cha Ufundi Karagwemwaka 2014 aliamua kujiajili mwenyewe ambapo tayari amepata faida ya kazi yake kwani kwasasa anasomesha watoto wake watatu, amejenga nyumba ya kuishi na familia yake na ameweza kujenga vyumba vinne vya kupangisha  ili kuongeza kipato.

Mkuu wa Mkoa baada ya kutembelea na kukagua kiwanda pamoja na samani anazozitengeneza alimshukuru kwa kujituma kuliko hata wananume. Pia alimweleza kuwa viwanda vinavyohimizwa na Serikali kila siku vinaanzia katika viwanda vidogo vidogo na baadae vinakuwa vikubwa. Aidha alimsistiza kuongeza juhudi ili kiwanda chake siku moja kiwe kiwanda kikubwa zaidi ya kilivyo sasa na kutoa ajira zaidi.

Mara baada ya kumtembelea mama Cineth alimtembelea Mama Mjane ambaye nyumba yake ilingushwa na upepo mkali uliombatana na  mvua  tarehe 21/02/2017 na kumfanya mama huyo kukosa makazi na kuishi kwenye hema. Wanawake Wilayani Karagwe wakishirikiana na Mfuko wa Maafa wa Wilaya waliamua kumchangia mama huyo fedha na kuanza kumjengea upya nyumba yake.

Wakati alipofika kwa mama huyo mjane Juliana Novath Kayanga katika kitongoji cha Nsheshe Mkuu wa Mkoa alikuta ujenzi wa msingi unaendelea ambapo alimchangia bati ishirini ili kuunga mkono juhudi za akina mama kwa mama Juliana apate makazi imara ambapo nyumba yake ili ikamilike  itagharimu shilingi 8,700,000/=

Pamoja na michezo na ushuhuda wa akina mama wajasiliamali katika maadhimisho hayo pia wananchi mbalimbali walihamasishwa na kuchangia damu kwa ajili ya wahitaji ambao wapo katika Hospitali mbalimbali na wana uhitaji wa damu ili kunusuru maisha yao.

Katika hatua nyingine akiwahutubia wananchi waliohudhuria katika maadhimisho hayo Mhe. Kijuu aliwaasa wanawake kuchapa kazi kwa bidii kwani wao ni msingi wa mabadiliko ya uchumi kama kaulimbiu isemavyo. Pia aliagiza kila Wilaya kuhakikisha inapambana na wale wote wanaojihusha na madawa ya kulevya kuwakamata na kuwachukuila hatua kali za kisheria.

Kaulimbiu ya mwaka huu inasema “Tanzania ya Viwanda Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko ya Uchumi.” Maadhimisho ya Siku ya  Wanawake yalianza kuadhimishwa  tangu mwaka 1911 huko nchini Marekani, wanawake walipoandamana kudai haki zao na tangu haposiku hiyo  huadhimishwa kote duniana tarehe 8 Machi kila mwaka  ili kupima ufanisi wa  matamko mbalimbali ya wanawake duniani.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.