• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Maafisa Elimu Nchini Waonywa Kutoiba Mitihani Vinginevyo Watafukuzwa Kazi na Kuchukuliwa Hatua za Kisheria – Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Posted on: October 9th, 2018

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akihitimisha ziara yake ya siku nne Mkoani Kagera iliyoanza Oktoba 6, 2018 na kuhitimishwa Oktoba 9, 2018 atoa onyo kali kwa Maafisa Elimu pamoja na Maafisa mbalimbali wa Serikali nchini wanaohusika na usimamizi wa mitihani ya Kitaifa kutojihusisha na vitendo vya kuiba  mitihani kwa ajili ya kuwatafutia majibu wanafunzi ili wafaulu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi Maafisa wote watakaojihusisha na njama za kuiba mitihani ili kuwafaulisha wanafunzi  badala ya kuwaandaa kwa kuwafundisha kwa bidii ili wafanye mtihani wenyewe bila kupewa majibu.

“Vitendo vya kuiba Mitihani na kuwapa wanafunzi ili wafaulu, kwanza ni kuwadumaza akili wanafunzi ili wasijishughulishe kutafuta majibu wenyewe, pili mnawaumiza wanafunzi wenyewe na wazazi wao kwa kitendo cha kurudia mitihani, Serikali haitavumilia vitendo hivyo itachukua hatua kwa yeyeyote atakayehusika, kamatulivyochukua hatua katika Wilaya za Chemba na Kondoa Mkoani Dodoma.” Alifafanua Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa onyo hilo akiwa katika Shule ya Msingi Nyakato Wilaya ya Bukoba mara baada ya kupokea mradi wa vyumba sita, ofisi mbili na matundu ya vyoo 16 kutoka kwa mwakilishi wa Balozi wa Japani  nchini Tanzania Bw. Katsutoshi Takeda katika Shule za Msingi Nyakato na Kashozi ambapo ujenzi huo uligharamiwa na nchi ya Japani kupitia Balozi wake nchini baada ya shule hizo kuharibiwa vibaya na Tetemeko la Ardhi lililotokea Septemba 10, 2016.

Baada ya Tetemeko la Ardhi kutokea mwaka 2016 nchi ya Japan kupitia Balozi wake nchini Tanzania ilitoa kiasi cha shilingi Milioni 228 kwa Halamshauri ya Wilaya Bukoba ili kurekebisha miundombinu iliyotajwa hapo juu katika Shule za Msingi Nyakato na Kashozi ili Wanafunzi warejee katika shule zao na kuendelea na masomo pamoja na Walimu kuendelea kutekeleza majukumu yao ya ufundishaji.

Mwakilishi wa Balozi wa Japani nchini Bw. Katsutoshi Takeda baada ya kukabidhi mradi huo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa baada ya nchi yake kutoa kiasi cha fedha Milioni 228 anafurahi kuona fedha hiyo imefanya kazi iliyokusudiwa na wanafunzi sasa wamerejea madarasani na wanaendelea na masomo yao.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kupokea mradi huo na kumkabidhi kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyakato kwa niaba ya Shule zote mbili Nyakato na Kashozi aliishukuru Serikali ya Japani kwa kuisaidia Seriakali ya Tanzania hasa Mkoa wa Kagera wakati ule wa matattizo ya Tetemeko na kurejesha miundombinu ya Shule hizo ili wanafunzi warejee madarasani na Walimu kutekeleza majukumu yao ya kufundisha.

Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwahakikishia Wananchi, Walimu na Wanafunzi waliohudhuria hafla fupi ya makabidhano kuwa Serikali itaendelea kuboresha Sekta ya Elimu nchini kuanzia ngazi ya Awali mpaka Vyuo Vikuu. Katika shule za Msingi Serikali inatoa shilingi bilioni 23.5 kila mwezi ili kugharamia elimu bila malipo  na watoto wameongezeka kutokana na kutokewepo na michango mbalimbali iliyokuwa inalipwa na wazazi hapo awali.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa wito kwa wazazi kuwaandaa watoto wao ikiwa ni pamoja kununua sare za shule, kufuatilia mienendo na maendeleo ya watoto wao shuleni kwa kushirikiana na walimu ili kujua kama watoto wao wanafika shule na wapatiwa elimu stahiki inayotakiwa kutolewa kwa mwanafunzi husika.

Serikali imeendelea kuboresha  Sekta ya Elimu kwa kulipa maslahi ya watumishi wa umma wakiwemo walimu na kuhakikisha yanapatikana kwa wakati. Pili kuajiri walimu  wa Shule za Sekondari 11,000 na Walimu wa Shule za Msingi 6,000 ambapo bado walimu wataendelea kuajiliwa ili kukidhi upungufu uliopo na utakaoendelea kujitokeza.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema pia Serikali mara baada ya kumaliza ujenzi wa maabara nchini sasa imetoa fedha za kujenga mabweni ili wanafunzi waweze kupata elimu na kulala shuleni. Pia Serikali imehakikisha upatikanaji wa vitabu katika shule za Sekondari  kutoka uwiano wa kitabu kimoja kwa Wananfunzi 15 hadi kitabu kimoja kwa Wanafunzi wawili na Shule za Msingi  kitabu kimo kwa Wanafunzi 8 hadi kitabu kimoja kwa Wanafunzi watano na mwelekeo ni kitabu kimoja kwa uwiano wa mwanafunzi mmoja.

Wanafunzi nchini wameaswa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuvitunza vitabu vinavyletwa na Serikali kwajili ya kuwasaidia katika masomo yao wasivichore michoro ya hovyo hovyo ndani au kukunja kurasa za vitabu hivyo na kupelekea uharibifu  jambo ambalo litavikosesha vizazi vijavyo kupata elimu kwa kusaidiwa na vitabu hivyo.

Pamoja na Waziri Mkuu Kupokea mradi wa Elimu Kutoka Ubalozi wa Japani katika Shule ya Msingi Nyakato lakini pia alitembelea kiwanda cha AMIMZA kinachosindika na kuongeza thamani ya zao la kahawa kilichopo Kibuye Manispaa ya Bukoba. Aidha, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea kituo cha Utafiti wa Kilimo Maruku ambapo alitoa wito kwa wakulima kupanda aina mpya ya mibuni inayozalisha kahawa kwa wingi na kuvumilia magonjwa inayozalishwa katika kituo hicho cha Utafiti Maruku.

Mwisho Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  alitembelea Shule ya Msingi Rweikiza yenye Mchepuo wa Kiingereza inayomilikiwa na Mbunge wa Bukoba Vijijini Jasson Rweikiza  na kumaliza ziara yake ya siku nne Mkoani Kagera kwa kufanya majumuisho katika ukumbi wa Hoteli ya ELCT Bukoba. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania alianza ziara yake Mkoani Kagera Oktoba 6, 2018 na kuhitimisha ziara hiyo Oktoba 9, 2018.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.