• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Mkoani Kagera Yaaswa Kutenda Haki Ili Yaaminiwe na Wananchi ni Baada ya Wajumbe Wake Wanne Kula Kiapo Mbele ya RC Gaguti

Posted on: April 12th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti awaapisha na kuwaasa wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Mkoani Kagera kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu, uadilifu pia kwa kutenda haki na kufuata sheria ili waweze kuaminika kwa wananchi wanaowahudumia.

Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema hayo April 12, 2019 wakati akiwaapisha wajumbe wanne wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya za Ngara na Karagwe ambapo aliwataka wajumbe hao kujikana wenyewe na kujitoa kikamilifu katika kazi zao ili kutenda haki kwa wananchi.

“Viongozi wengi wanaofanya  kazi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Mkoani Kagera wamekosa uhalali kwa wananchi wanaowahudumia kutokana na kutotenda haki, sasa nawaasa ninyi mlioapishwa kuhakikisha mnatekeleza kazi zenu kwa kutenda haki ili muweze kuwa halali kwa wananchi wenu.” Alisistiza Mkuu wa Mkoa Gaguti

Aidha, Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa katika Ofisi yake asilimia 80% hadi 90% ya malalamiko ya wananchi ni kuhusu migogoro ya ardhi, pia alisema kuwa hata katika ziara wilayani au viongozi wa Kitaifa wanapofika Mkoani Kagera malalamiko makubwa ya wananchi ni ya ardhi kutokana na Mabaraza ya ardhi na Nyumba ya Wilaya kutokutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Vilevile Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa wananchi wa Mkoa wa Kagera wamekuwa masikini kwa kupoteza fedha nyingi kwasababu ya kufuatilia kesi za ardhi katika Mahakama za chini hadi Mahakama za juu ambapo kama Mabaraza ya Ardhi na Nyumba yangekuwa yanatekeleza wajibu wake vizuri wananchi wasingekuwa wanapoteza fedha zao na muda kutafuta haki hadi Mahakama za juu.

Mwisho, Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa rai kwa Viongozi wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kutoa elimu kwa wananchi kuliko kujikita sana katika mashauri, pia alisisitiza Mabaraza ya  ngazi za chini mfano ya Vijiji na Kata kufanya kazi zake kupunguza migogoro ya ardhi jambo linalopelekea wananchi kujichukulia sheria mikononi kutokana kutoridhika na maamuzi yanayotolewa na kuufanya mkoa wa Kagera kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa mauaji na kujichukulia sheria mikononi.

Katika hatua nyingine Jaji Lucia Gamuya Kairo Jaji Mfawidhi wa Mhakama Kuu Kanda ya Bukoba aliwakumbusha wajumbe wanne walioapishwa kutekeleza majukumu yao kwa kutenda haki tena kwa uaminifu na uadilifu ili kutatua na kumaliza migogoro ya ardhi Mkoani Kagera

Jaji Kairo alisema kuwa Mabara ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya hayapo chini ya Mahakama lakini kwasababu yanashughulika na kutoa haki wananchi wanajua kuwa nayo ni sehemu ya Mahakama ambapo alisistiza kuwa kwa miaka minne aliyokaa Kagera ardhi imekuwa na malalamiko mengi na Mabaraza hayo yapo katika nafasi tatu za mwanzo kwa kulalamikiwa na wananchi katika kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Jaji Kairo alisema kuwa Rushwa inapofusha utoaji wa haki na kuwataka wajumbe wasijiingize katika vitendo vya rushwa na kuwakumbusha kuwa Haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyopotea na Haki iliyoharakishwa ni sawa na haki iliyopotea ambapo aliwataka wajumbe hao kutekeleza majukumu yao kwa ulinganifu bila kuchelewesha au kuwaisha haki katika maauzi yao.

Wajumbe walioapishwa na Mkuu wa Mkoa Gaguti Aprili 12, 2019 ni Bw. Charles Mbeikya na Bi Christina Mugasha Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Ngara, wengine ni Bw. Longino Frederick na Bi Lucletia Shubilo Saulo Balaza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Karagwe. Katika Mkoa wa Kagera Kuna jumla ya Mabaraza ya Ardhi na Nyumba manne katika Wilaya za Bukoba, Muleba, Karagwe na Ngara.

Aidha, wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba huchaguliwa kila baada ya kipindi cha miaka mitatu na Baraza moja linaweza kuwa na wajumbe sita hadi saba lakini Mwenyekiti wa Baraza anatakiwa kuwa na wajumbe wasiopungua wawili wakati akisikiliza na kuendesha mashauri.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.