• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Madini ya TIN Kuipaisha Wilaya Mpya ya Kyerwa Kiuchumi Nchini Yatachimbwa Hadi Miaka Hamsini Ijayo – Kassim Majaliwa Waziri Mkuu

Posted on: September 21st, 2021

“Wilaya ya Kyerwa ni kati ya Wilaya mpya nchini lakini naiona Wilaya hii kwa miaka michache ijayo mbele kidogo itakuwa na nguvu kubwa kiuchumi kutokana na raslimali zinazopatikana hapa, itaongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa katika mkoa wa Kagera  na nchini kwa ujumla kutokana na madini ya TIN yanayopatikana hapa pamoja na zao la kahawa, ndizi na mazao mengine.

Maneno ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi makao makuu ya Wilaya ya Kyerwa Rubwela Septemba 20, 2021 mara baada ya kutembelea kiwanda cha African Top Minerals Limited cha kuchenjua madini ya TIN yanaoyopatikana mkoani Kagera wilayani Kyerwa tu.

Ni baada ya kufurahishwa na  uwekezaji wa kiwanda hicho chenye thamani ya Shilingi bilioni nne ambacho kina uwezo wa kuchenjua  tani  10 kwa siku  na tani 250 kwa mwezi za madini ya  TIN. Waziri Mkuu  Kassim majaliwa alitoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa hiyo kwani madini ya TN Wilayani Kyerwa ni ya kutosha na  kutokana na utafiti uliofanyika mwaka 2017 na Taasisi ya Utafiti  wa  Madini Tanzania   iligundulika kuwa katika eneo moja tu kuna madini ya TIN tani milioni nne ambazo zinaweza kuchimbwa kwa miaka 40 hadi 50

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwepo kwa viwanda vya TIN Wilayani Kyerwa  vya Afican Top Minerals Limited na TANZA PLUS Limited vyenye u wezo wa kuchenjua tani 16 kwa siku na tani 450 za TIN kwa mwezi ni fursa kubwa kwa vijana kujiajili kwa  kuchimba madini hayo ambayo yamepanda bei mara baada ya wawekezaji hao wa viwanda kujenga viwanda hivyo na kuanza uchenjuaji Wilayani humo.

“Hii ni ajira vijana changamka unachimba mawe haya kilo moja unauza hapa hapa na bei imepanda baada viwanda hivi kuwa vimejengwa na kuhitaji mzigo wa kutosha ili vifanye kazi, mwaka 2019 madini haya ya TIN yalikuwa yanauzwa shilingi 6,000/- kwa kilo leo mwaka 2021 yanauzwa shilingi 34,000/- kwa kilo. Kyerwa tukitumia fursa hii wilaya itakuwa na maendeleo makubwa sana na itaongoza kwa uchumi mzuri mkoa wa  Kagera.” Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa akihutubia wananchi Wilayani Kyerwa.

TANESCO Waagizwa Kuachana na Wakandarasi Katika Ujenzi

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa  akiwa Wilayani Kyerwa alikataa kuzindua majengo ya ofisi za TANESCO wilaya yaliyojengwa na Mkandarasi  kwa gharama ya shilingi milioni 483,422,328.02 mara baada ya kusomewa taarifa amabyo ilitaja gharama za ujenzi wa kibanda cha mlinzi kugharimu shilingi milioni saba ambapo alisema kuwa angeweza kuchukua hatua lakini ni kutokana na majengo hayo kujengwa kwa kutumia Mkandarasi.

“Ningeweza kuchukua lakini  kwa kuwa mlitumia Mkandarasi basi nawaagiza kuacha mara moja mfumo huo na kwa majengo mnayoyajenga katika Wilaya 12  nchini  tumieni mfumo wa FORCE AKAUNTI. Haiwezekani  Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia Halmashauri za Wilaya tujenge  Vituo vya Afya  vyenye majengo matano kwa gharama ya shilingi milioni 500 halafu hapa mmejenga jengo moja uzio, kibanda cha mlinzi na stoo kwa gharama ya shilingi milioni 483,422,328.02.” Aliagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Serikali Kuuangalia Upya Mfumo wa Ushirika Mkoani Kagera 

Ni baada ya kutembelea kiwanda cha Ngara Coffee kilichopo Wilayani Ngara  ambacho hakifanyi kazi kutokana na kukosa malighafi ambayo ni kahawa, aidha malalamiko ya wananchi kuwa bei ya shilingi 1,300 ni ndogo ukilinganisha na mikoa mingine nchini. Baada ya kupokea malalamiko hayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwaeleza wananchi katika mikutano ya hadhara kuwa anakusudiwa kuunda timu ya wataalam kwenda mkoani Kagera kupitia upya mfumo wa Vyama vya Ushirika ili kuona namna ya kumnufaisha mkulima zaidi badala ya Vyama vya Ushirika.

  • TANESCO Waagizwa Kuachana na Wakandarasi Katika Ujenzi
  • Serikali Kuuangalia Upya Mfumo wa Ushirika  Kagera 

 "Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa atatuma timu ya  wataalam kufanyia kazi tatizo la bei ya kahawa, Kuhakiki Mali za Vyama vya Ushirika vinavyonunua na kuuza kahawa ya wakulima, kushughulika na  mfumo wa kununua na kuuza kahawa,  Kushughulikia  suala la bei ya kahawa mkoani Kagera kuwa ya chini, na Kwanini tozo ni nyingi zinafika hadi 12 badala ya tozo tano tu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa baada ya mradi wa kuzalisha umeme wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni 898 unaotekelezwa na nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi kukamilika Desemba 2021 na kuanza kuzalisha umeme Mkoa wa Kagera utaunganishwa kwenye gridi  ya taifa na matatizo ya umeme Kagera yatakuwa yamefikia mwisho.

Mwisho, Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa aliwataka viongozi wa Mkoa wa Kagera kusimamia ipasavyo miradi ya maendeleo hasa miradi inayolenga kutoa huduma kwa wananchi ambayo imetolewa fedha nyingi na Serikali, mfano ujenzi wa Hospitali za Wilaya na Vituo vya Afya ili miradi hiyo ijengwe kwa  ubora unaotakiwa  na ujenzi uendane na thamani ya fedha iliyotolewa.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.