• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Mawakala wa Kampuni Binafsi Wanaowapotosha Wakulima Vijijini Kuhusu Mfumo Serikali wa Ukusanyaji wa Kahawa Wakamatwe Mara Moja – RC Kagera

Posted on: July 21st, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti aagiza kukamatwa mara moja kwa Mawakala wawili wa Kampuni binafsi  wanaopita vijijini katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa kuwaposha na kuwalaghai wakulima wa kahawa wasikubaliane na mfumo wa Serikali wa kukusanya kahawa katika vyama vya msingi na kuiuza kwa mfumo wa ushirika ulionzishwa na Serikali.

Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa maelekezo hayo Julai 21, 2019 katika mkutano wa viongozi wa Vyama vya Msingi, Watendaji wa Kata na Viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika cha KDCU Limited Wilayani Karagwe mara baada ya kukagua viwanda vitatu  vya kukoboa kahawa vya Karim Amri, ASU Company Limited na KDCU Limited kuona namna vinavyoendelea kuchakata kahawa.

“Nimeona nije kujionea msimu unaendeleaje na kama kuna changamoto yoyote tuitatue kwa pamoja na si kusubiri msimu umeisha. Pia ninazo taarifa kuwa kuna mawakala wawili wa Kampuni binafsi wamekuwa wakipita vijijini kupotosha wakulima wasifuate mfumo wa Serikali ili baadae waje wanunue kahawa yao kwa bei ndogo tu namuagiza Kamanda Polisi Mkoa Mawakala hao wakamatwe mara moja.” Aliagiza Mkuu wa Mkoa Gaguti

Pia MMhe. Gaguti alisema kuwa maelekezo ya Serikali yapo wazi kuwa kama kuna mfanyabiashara yeyote anataka kununua kahawa awasiliane na ofisi yake lakini awe na bei inayomnufaisha mkulima. “Tayari tumepokea maombi kadhaa ya kununua kahawa kutoka kwa wanunuzi binafsi lakini maombi yote hayamnufaishi mkulima bei yao ipo chini sana hatuwezi kumruhusu mkulima anyonywe. Alisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti

Kuhusu bei kwamba wakulima wanapunjwa Mkuu wa Mkoa  Gaguti aliitolea ufafanuzi kuwa mpaka mkulima analipwa malipo ya kwanza tayari Vyama Vikuu vya Ushirika vinakuwa vimeondoa gharama za uchakataji kiasi cha shilingi 600  na kupelekea kilo moja kufika hadi 1700/= lakini bado bei katika soko la dunia ikitangazwa mkulima anaongezewa fedha nyingine wakati makato yote ya Serikali na gharama za uchakataji zinakuwa zimelipwa tayari.

Aidha, Mzee Thomas Kasimbazi  mkulima kutoka Chama cha Msingi Nyabwegira Kata Ndama aliiomba Serikali inapokuwa na mipango mizuri iwashirikihe wananchi ili waweze kuelewa hasa suala la mkulima kulipiwa benki ambapo mzee  Kasimbazi  alisema kuwa wazee wengi hawajui na hawaelewi kwanini wanalipiwa Benki baada ya kukusanya kahawa yao katika Vyama vya Msingi ambapo wakipata elimu wapo tayari kutoa ushirikianao kwani Serikali inalenga kulinda fedha zao ziwafikie walengwa moja kwa moja.

Akifafanua  Mkuu wa MkoaGaguti alisema kuwa tayari elimu inaendelea kutolewa chini ya uongozi wa  Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ikishirikiana na mitandao ya simu, TCRA, na Benki  zinazohusika katika malipo wanapita kwa wakulima na kuwaelimisha faida za kulipiwa benki pia Mkuu wa Mkoa Gaguti aliagiza Wakuu wa Wilaya kubaini maeneo yenye changamoto ya mitandao na wakulima wenye fedha chini ya Tshs 100,000/= kupelekewa fedha zao taslimu bila kuzipitisha benki.

Vyama Vikuu vya Ushirika Mkoani Kagera vya KCU 1990 LTD na KDCU LTD tayari vimekusanya kahawa kilo milioni 8.5 sawa na asilimia 20% ya malengo ya ukusanyaji katika msimu huu wa mwaka 2019/20 na jumla ya shilingi bilioni 6.2 tayari zimelipwa kwa wakulima aidha, KDCU LTD tayari kimekusanya kahawa ya maganda kilo milioni 5.8 na shilingi bilioni 5.3 zimelipwa kwa wakulima sawa na asilimia 15%  ya matarajio ya makusanyo.

Mnada wa kahawa katika msimu huu wa 2019/20 unatarajiwa kufanyika ndani ya wiki mbili kutoka sasa katika Manispaa ya Bukoba badala ya Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo baada ya mnada huo bei kamili ya kahawa itatangazwa rasmi ili mkulima ajue kwa kila kilo atauza kwa shilingi ngapi na kupatiwa malipo ya pili baada ya kulipwa shilingi 1100/= malipo ya awali.

Akimalizia mkutano wake Wilayani Karagwe  na viongozi mbalimbali wa vyama vya Msingi Mkuu wa Mkoa Gaguti aliwaeleza vingozi hao kuwa dhamira ya Serikali ni kulinda maslahi ya wakulima wa kahawa na si vinginevyo pia kuwahimiza wakulima kukubali mfumo wakulipiwa  benki kwa usalama wa fedha zao na wao wenyewe ikiwa ni pamoja na kudhibiti ubadhirifu wa baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi kutumia fedha za wakulima kwa matumizi yasiyokubalika.

Katika msimu huu wa mwaka 2019/20 Vyama Vikuu vyote vya Ushirika Mkoani Kagera vimekisia na vinatarajia kukusanya kahawa kilo milioni 52 ambapo msimu uliopita wa mwaka jana 2018/19 vyama hivyo vilikusanya kahawa kilo milioni 58.9

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.