• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Mkurugenzi Mkazi wa Umoja wa Maifa Akagua Miradi Inayofadhiliwa na Umoja Huo Mkoani Kagera

Posted on: March 13th, 2017

Umoja wa Mataifa kupitia Mkurugenzi wake Mkazi nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez umetembelea, kukagua na kuridhishwa na  utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na umoja huo Mkoani Kagera ambapo zaidi ya Dola za Kimarekani (618,000 USD) zimetolewa ili kufadhili na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama Elimu na Afya pia na miradi ya kijamii.

Bw. Alvaro Rodriguez ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Mashirika matatu ya Umoja wa Maifa nchini Tanzania (IOM, UNICEF na UNDP) aliwasili Mkoani Kagera Machi 13, 2017 na ujumbe wake ili kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo na Kijamii inayofadhiliwa na Umoja huo katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Miradi aliyoitembelea Bw. Rodriguez ni pamoja na mradi wa ujenzi wa vyoo, madarasa,  mabweni na jengo la utawala katika shule ya Msingi Mgeza Mseto Manispaa ya Bukoba ambapo mara baada ya kukamilika mradi utagharimu Dola za Kimarekani (318,000 USD) ambapo ujenzi wa vyoo umekamilika, madarasa mabweni na jengo la Utawala ujenzi upo katika hatua ya msingi.

Bw. Rodriguez akiongea na wanafunzi, walimu na wananchi waliofika kumpokea katika shule hiyo alisema kuwa amefurahishwa kufika katika shule hiyo na kujionea hali halisi ya watoto wenye ulemavu wa albinizimu na walemavu wengine aidha, alisema kuwa Umoja wa Mataifa uliamua kutoa fedha hizo ili kurejesha miundombinu ya shule hiyo baada ya kuharibiwa na Tetemeko la Ardhi lilitokea Septemba 10, 2016.

“Nilipokuwa Dar es Salaam niliambiwa na Waziri Profesa Joyce Ndalichako kuwa nikifika Kagera nitembelee Shule ya Msingi Mugeza Mseto pia nilipofika Kagera Mkuu wa Mkoa ameniambia nitembelee shule hii sasa nimejionea na kujua ni kwanini walinisistiza, shule inahitaji msaada mkubwa. Aidha, Umoja wa Mataifa unapenda kusaidia lakini Tanzania shule  za namna hii zipo nyingi na ndiyo maana tunasaidia kidogo kidogo ili kuongeza mahitaji muhimu.” Alisistiza Bw. Rodriguez

Pai Bw. Rodriguez alisema kuwa mara baada ya kujionea hali halisi ya shule hiyo ataendelea kushawishi wafadhili mbalimbali ili kuhakikisha shule hiyo yenye mahitaji maalum inapewa kipaumbele katika ufadhili. Vilevile aliiomba jamii kutowanyanyapaa watoto wenye ulemavu kwani ulemavu hauna ukabila, utaifa wala rangi ambapo alisema kuwa hata yeye watoto wake ni walemavu jambo ambalo alisema ulemavu hauna mzungu wala mweusi.

Umoja wa Maifa pia umetoa ufadhili dola za Kimarekani (250,000 USD) kwenye shule za Msingi 16 Katika Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ili kujenga vyoo na kuimarisha mifumo ya maji kwa ajili ya uboreshaji wa usafi na mazingira. Pia kukarabati miundombinu yote iliyoharibiwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea mwaka jana 2016.

Aidha, Umoja wa mataifa kupitia Shirika lake la (UNICEF) ulitoa ufadhili wa kujenga majiko sanifu katika jamii kwaajili ya kutunza mazingira kwa wananchi wa hali ya chini kwa kutumia nishati ya kuni kidogo. Pia kupitia shirika la (IOM) wananchi na kaya masikini waliokumbwa na Tetemeko  la Ardhi mwaka 2016 waligawiwa vifaa mbalimbali kama  ndoo, magodoro, blanketi, bati, vyandarua na vifaa vya kujengea makazi ya muda katika Halmashauri za Bukoba Manispaa, Bukoba na Missenyi.

Katika Hatua nyingine Bw. Rodriguez alikagua mradi uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa wa kufunga umeme wa jua katika Zahanati ya Bushasha Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Shule ya St. Mary Rubya Seminari Wilayani Muleba. Katika Shule ya Rubya Seminari ufungaji wa umeme wa jua uligharimu Dola za Kimarekani (50,000 USD) hadi kukamilika.

Akitoa maelezo ya Mradi huo Padre Malianus Rutagwerela ambaye ndiye Mkuu wa Seminari hiyo alisema kuwa mradi huo umeongeza nguvu ya mwanga katika shule hiyo na kuwa na umeme wa uhakika ikiwa ni pamoja na umeme wa TANESCO. Aidha aliushukuru umoja wa Mataifa kwa niaba ya uongozi wa Jimbo Katoliki la Bukoba kuwa mradi huo utaboresha zaidi elimu katika Seminari hiyo.

Naye Mkurugenzi Mkazi Bw. Rodriguez alifurahishwa sana na mradi huo ambao alishuhudia ukifanya kazi vizuri. “ Nimefurahishwa na mradi huu pia sisi kama Umoja wa Mataifa tutaendelea kuona jinsi ya kusaidia shule kama hizi ili Mapadre na Viongozi wa dini waendelee kuzalishwa katika shule kama hizi ili wasaidie kueneza neno la Mungu kuhusu upendo na kuondoa chuki kati ya Wanadamu. Alieleza Bw. Rodriguez

Mwisho, Bw. Rodriguez alisema kuwa amefurahishwa na utekelezaji wa miradi ambayo ipo chini ya Mashirika ya Umoja wa Maifa ambayo imetolewa ufadhili wa fedha na Umoja huo na kutekelezwa au inaendelea kutekelezwa Mkoani Kagera. Aidha,  alihaidi kuendelea kuushawishi Umoja huo na wafahili mbalimbali ili waendelee kuuangalia na kuufadhili Mkoa wa Kagera katika miradi mbalimbali ya maendeleao na Kijamii.

 

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.