• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Mkuu wa Mkoa Awaagiza TRA Kutofunga Maduka ya Wafanyabiashara Mkoani Kagera Badala Yake Waelimishwe Ili Kulipa Kodi ya Serikali

Posted on: January 12th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti awaagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera (TRA) kuanzia Januari 11, 2019 kuacha tabia za kufunga biashara za wananchi kwasababu ya kodi badala yake wajikite katika kutoa elimu na kuwaelimisha wafanyabiashara kulipa kodi kwa utashi bila kushurutishwa pia waweke mkakati wa kuwapata walipakodi wapya.

Maagizo hayo yalitolewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti katika kikao cha Baraza la Wafanyabiashara kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Bukoba Januari 11, 2019 ambapo aliwaita wafanyabiashara hao kuwasikikiliza kero zao ili kuboresha ulipaji wa kodi katika Mkoa wa Kagera ikiwa ni pamoja na kufikia malengo ya ukusanyaji wa kodi kwa mwaka 2018/2019 kwa asilimia 100%.

Kabla ya Mkuu wa Mkoa kutoa maagizo hayo aliwapa nafasi wafanyabiashara kuchangia namna bora ya kuhakikisha kodi inakusanywa kwa asilimia 100% katika Mkoa wa Kagera na kuhakikisha wafanyabiashara wote wanafikiwa ili kodi rafiki ilipwe katika mazingira mazuri ya kufanya biashara bila bughudha zozote.

Wafanyabiashara waliopata nafasi ya kuchangia katika kikao hicho walilalamika juu ya utendaji kazi wa  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa wanakusanyatu kodi bila kutoa elimu na hawajengi mazingira mazuri yakuwasikiliza wafanyabiashara ili walipe kodi kwa utashi hasa katika Mkoa wa Kagera jambo ambalo limepelekea wafanayabisahara wengi kufunga biashara zao.

Mara baada ya kuwasikiliza Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa anataka katika Mkoa wa Kagera kuwe na mazingira mazuri ya wafanyabiashara kufanya biashara zao  na kulipa kodi bila kushurutishwa na kila mfanyabiashara atambuliwe ili kuwa na takwimu sahihi za wananchi wote wanaojishughulisha na biashara.

Mkuu wa Mkoa Gaguti alitoa siku kumi na nne kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwatumia Viongozi na Watendaji katika ngazi za Kata hadi Vijiji kuwatambua wafanyabiashara wote wawe wakubwa au wadogo ili kuwe na takwimu sahihi ya mkoa kuhusu wananchi wanaojishughulisha na biashara kwani  katika Mkoa wa Kagera ulipaji kodi ni asilimia 0.4% tu.

Aidha, Mkuu wa Mkoa Gaguti aliitaka TRA Mkoa wa Kagera kutanua wigo katika kukusanya kodi hasa kodi za majengo na ardhi. Pia aliwataka wafanyabiashara kuwa wakweli katika kutoa takwimu zao za biashara ili wasikwepe kodi na wala wasionewe. Mwisho Mhe. Gaguti aliitangaza tarehe 25 hadi 30 Machi, 2019 kuwa itakuwa wiki ya Kagera na kuwaomba wananchi katika Sekta zote kushiriki kuutangaza Mkoa wa Kagera katika wiki hiyo.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Prof. Faustine Kamuzora aliyehudhuria kikao hicho aliwahakikishia Wafanyabiashara kuwa sasa uongozi wa mkoa umejipanga kuondoa vikwazo vyote vinavyorudisha juhudi za wafanyabiashara kusonga mbele ambapo alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inataka kuona kila mwananchi anatajirika katika nchi yake mahali popote alipo.

Profesa Kamuzora alisema kuwa atahakikisha anaimarisha Mabaraza ya Wfananyabiashara ya Wilaya na Mkoa ili kuhakikisha Sekta binafsi inashirikiana na Serikali kikamilifu katika kuchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla

“Jana wakati nimefika hapa mkoani niwauliza wenzangu kuwa mkoa wetu hivi leo unacheza ngazi gani ya ligi nikaambiwa unacheza ndondo cup, wakati ule sisi Kagera ndiyo tulikuwa tunawika na kucheza Premiere League lakini sasa Ndondo? Hapana! Jambo hili inaenda mbali hadi kwenye maendeleo sisi hatutakiwi kuwa ndondo tunatakiwa Premiere.” Alisissitiza Katibu Tawala wa Mkoa Prof. Kamuzora

Mara baadaya kikao cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Kagera kumalizika Mkuu wa Mkoa na Ktibu Tawala wa Mkoa pamoja na viongozi wengine walitemblea baadhi ya Wafanyabiashara katika Mtaa wa One Way na Soko Kuu Manispaa ya Bukoba kusikiliza Changamoto wanazokumbana nazo ili kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara na kulipa kodi stahiki kwa utashi.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.