• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Mkuu wa Mkoa Kagera Awashauri SUMA JKT Kutekeleza Miradi ya Serikali Kwa Gharama Ndogo na Kuikamilisha Kwa Wakati

Posted on: September 19th, 2019

Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli inafanya kazi usiku na mchana kuwahudumia wananchi wake hasa kusogezea karibu huduma za kijamii kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika mikoa, Wilaya hadi vijiji.

Katika kuhakikisha kuwa miradi ya kutolea huduma kwa wananchi inasimamiwa na kutekelezwa kwa viwango stahiki ili itoe huduma iliyokusudiwa pia Serikali imekuwa ikiboresha  mazingira ya watendaji wake wanaosimamia miradi hiyo ya maendeleo kwa kuwajengea miundombinu bora inayowawekea mazingira bora pia ya kutekeleza majukumu yao ikiwemo ofisi na makazi yao.

Miradi hiyo ya Serikali yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni mbili (2) katika Mkoa wa Kagera ni pamoja na ujenzi wa  Ofisi za Wakuu wa Wilaya mpya tatu za Biaharamulo, Muleba na Kyerwa, ujenzi wa nyumba ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Kyerwa, pia  ujenzi wa ofisi tano za Maafisa Tarafa katika Wilaya za Kyerwa, Biharamulo, Karagwe, Muleba na Bukoba vijijini.

Akikagua miradi ya ujenzi wa Ofisi za Wakuu wa Wilaya Biharamulo na Muleba Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti Septemba 18, 2019 aliridhishwa na viwango pia ubora wa majengo hayo mawili yanayoendelea kujengwa  na kampuni ya SUMA  JKT na kusema kuwa majengo hayo yanaonesha thamani halisi ya kiasi cha fedha zilizotumika.

Katika ukaguzi huo Mkuu wa Mkoa Gaguti alito wito kwa Kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT ihakikishe inaendela kutekeleza miradi yake kwa ubora unaotakiwa lakini pia ikamilishe miradi iliyopewa kwa wakati bila visingizio vyovyote vinavyoweza kuchelewesha miradi hiyo kukamilika kwa muda na wakati wakati uliopangwa au matarjio ya Serikali.

Pili, Mkuu wa Mkoa Gaguti aliishauri Kampuni hiyo ya SUMA JKT kuona namna bora ya kupunguza gharama zake za ujenzi na kutekeleza miradi mingi ya Serikali ikiwa yenye viwango kwasababu nayo pia ni Kampuni ya Serikali haitakiwi kutengeza faida kubwa katika miradi. Mhe. Gaguti aalitoa mfano wa ujenzi wa vituo vya afya na hospitali za wilaya zilizojengwa na fedha kidogo lakini kwa viwango na kukamilika kwa wakati.

“Mimi ni Mwananjeshi kama ninyi na hii Kampuni ya SUMA JKT ambayo na mimi ni mhusika lakini lazima sisi tuwe wa mfano kwa makampuni mengine, kwa kutekeleza miradi ya Serikali kwa gharama ndogo lakini yenye viwango na hapo tutapata kazi nyingi za Serikali na tukumbuke kuwa huo ni uzalendo tunatakiwa kutengeneza faida kidogo kwani hatufanyi biashara.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Serikali ya Awamu ya Tano tayari imetoa  fedha za ujenzi za ofisi za Wakuu wa Wilaya za Biharamulo shilingi milioni 295, Muleba shilingi milioni 690, Kyerwa shilingi milioni 541. Ujenzi wa nyumba ya Katibu Tawala Kyerwa shilingi milioni 159, ujenzi wa ofisi za Maafisa Tarafa tano shilingi milioni 326, ujenzi wa miundombinu hiyo upo katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji.

Aidha, katika mkoa wa Kagera Serikali imetoa fedha za kutekeleza pia miradi ya kutolea huduma za jamii na utekelezaji wake unaendelea, Serikali ilitoa shilingi bilioni 4.5 za ujenzi wa Hospitali za Wilaya za Bukoba (vijijni), Karagwe na Kyerwa tayari hospitali zimekamilika. Serikali ilitoa shilingi milioni 169 za upanuzi wa wodi ya wazazi na kujenga vyumba viwili vya upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera,  ujenzi upo katika hatua za mwisho kukamilika ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi akina mama wajawazito.

Vilevile katika kusogeza karibu huduma kwa wananchi Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ilitoa shilingi bilioni 5.9 za ujenzi wa vituo 14 vya afya katika mkoa wa kagera ambavyo vimejengwa na kukamilika na tayari vinatao huduma kwa wananchi wa Kagera. Wito kwa wananchi ni kuendelea kushirikiana na Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo pia kuitunza miradi hiyo ili idumu na kuendelea kutoa huduma stahiki.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.