• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kulia Akimpoza Daktari Bingwa Kwa Kutoa Huduma Kwa Wananchi wa Kagera

Posted on: October 6th, 2017

Wananchi Wajitokeza Kwawingi Kunufaika na Huduma za Madaktari Bingwa Mkoani Kagera

Uongozi wa Mkoa wa Kagera wafanikisha zoezi la kutoa huduma ya afya ya Madaktari Bingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa mjini Bukoba na kuwahudumia wananchi 3146 waliokuwa na magonjwa yaliyowasumbua kwa muda mrefu na yalihitaji huduma za kibingwa.

Katika huduma hiyo iliyokuwa imekusudiwa kutolewa kwa siku saba kuanzia tarehe 18 hadi 24 Septemba, 2017  kutokana na wingi wa wananchi wenye matatizo iliongezwa siku hadi tarehe 28 Septemba, 2017 ambapo wananchi walikuwa na matatizo mablimbali ya kiafya 5700 walijitokeza kuhudumiwa.

Akitoa taarifa mara baada ya zoezi hilo Mganga  Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Kagera Dk. John Mwombeki alisema wananchi walijitokeza kwa wingi juu ya makadirio yao ya awali jambo ambalo lilipelekea baadhi ya wagonjwa zaidi ya 2000 waliojiandikisha kutowaona Madaktari Bingwa.

Dk. Mwombeki alisema kati ya wananchi 5700 waliojiandikisha ni 3146 walioonwa na Madaktari Bingwa na kuhudumiwa katika maganjwa ya Makoromeo, Sikio na Pua, Macho, Meno, Magonjwa ya wakinamama, Magonjwa ya ndani, Mifupa, Magonjwa ya watoto na Magonjwa ya mfumo wa mkojo kwa wanaume.

Aidha, kati ya wagonjwa 3146 walioonwa na Madaktari Bingwa  wagonjwa 446 walifanyiwa upasuaji mkubwa. Gharama za kuwaona Madaktari Bingwa hao ilikuwa ni Shilingi 5000 kujiandikisha na shilingi 30,000 kwa wagonjwa ambao walishauriwa kufanyiwa upasuaji.

Akizungumzia zoezi hilo lilivyofanikishwa  Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Thomas Rutachunzibwa alisema zoezi hilo lilifanikiwa kutokana na kufunga mfumo wa mapato katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera na kuanza kukusanya kiasi kikubwa cha fedha ambazo zilizopelekea kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi wa Mkoa wa Kagera.

Pia katika zoezi hilo lililofanyika kwa siku kumi kiasi cha shilingi milioni 34,886,338 taslimu zilikusanywa pamoja na wagonjwa 1,010  kati ya 3,146 walipata huduma za matibabu na kulipia huduma hizo kwa njia ya Bima ya Taifa (NHIF) na Bima za Mashirika mengine kama AAR, TANESCO, NSSF na STRATEGES.

Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Kamishina Diwani Athumani akizungumzia zoezi hilo alisema kuwa jukumu la Serikali ni Kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi, pia alisema kuwa  baada ya kupokea ombi la kuleta huduma za Madaktari  Bingwa Mkoani Kagera  kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa alihakikisha kuwa vifaa na miundombinu yote iliyohitajika inakamilika ili Madaktari Bingwa hao waweze kutekeleza majukumu yao ipasavo.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu mara baada ya kukagua zoezi hilo la Madaktari Bingwa wakiwahudumia wagonjwa alisema kuwa zoezi hilo linatakiwa kuwa endelevu ili wananchi waweze kuhudumiwa kwa gharama ndogo na uhuhitaji wa wananchi ni mkubwa sana.

“Zoezi hili linatakiwa kwenda mpaka katika ngazi ya Halmashauri za Wilaya kwasababu kuna wananchi wengi ambao hawakupata fursa ya kufika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera na wana matatizo makubwa kama tulivyoona hapa.” Alisistiza Mkuu wa Mkoa Kijuu.

Naye Jovinus Rweikiza  kutoka katika Kijiji cha Kasharu Bukoba Vijiji aliyefanyiwa upasuaji wa tezidume na Madaktari Bingwa hao akiwa wodini alitoa ushuhuda jinsi alivyokuwa amehangaika katika Hospitali mbalimbali ili aweze kupata huduma na kupewa rufaa za kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bugando lakini ilikuwa inashindikana kutokana na gharama kubwa za matibabu hayo.

Serikali ya Mkoa wa Kagera inatoa rai kwa wananchi waliokuwa wamejiandikisha na kulipa fedha zao ili kuonana na Madaktari bingwa lakini hawakufanikiwa kuonana nao kutokana na wingi wa wagonjwa na muda wao kuwa mfupi,  zoezi hilo litakapofanyika tena watapewa kipaumbele na kupewa huduma hiyo bila kulipia tena shilingi 5000 za kujiandikisha kwani tayari mafaili yao yapo.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.