• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu (Katikati) Akikagua Majengo ya Kituo cha Afya Nyakayanja Wilayani Karagwe

Posted on: February 7th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Akagua Miradi ya Afya Kuona Shilingi Bilioni 3.5 Fedha za Serikali Zinatumika Kama Ilivyokusudiwa

Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu afanya ziara katika Halmashauri za Wilaya nane   kukagua matumizi ya shilingi bilioni 3.5 fedha zilizotolewa na Serikali  kukarabati baadhi ya Vituo vya Afya Mkoani Kagera pia  kuwahamasisha wananchi kuendelea kuchangia gharama za ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya ambavyo havijakamilika katika maeneo yao kwa kushirikiana na Serikali.

Akiongea  na wananchi katika Kituo cha Afya Nyakanazi  Wilayani Biharamulo Mkuu wa Mkoa Kijuu alisema kuwa alifika  kituoni hapo pamoja na Vituo vingine vya Afya ambavyo vimepewa fedha na Serikali ili vikarabatiwe ili ajionee kama fedha hizo zinatumika ipasavyo ikiwa ni pamoja na michango ya wananchi  wa eneo husika na kuhakikisha ujenzi unakamilika ifikapo Machi 30, 2018.

Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 3.5 kwa vituo vinane katika Mkoa wa Kagera  ambapo awamu ya kwanza ilitolewa  shilingi milioni 500 kwa kila kituo Vituo vya Nyakanazi (Biharamulo) na Kayanga (Karagwe).  Awamu ya pili Serikali ilitoa  shilingi milioni 500 kituo cha Katoro (Bukoba) na  Vituo vya Kishanje (Bukoba), Mabawe na Murusagamba (Ngara), Kimea (Muleba), na Murongo (Kyerwa) vilipewa shilingi milioni 400 kila kimoja.

Akitoa ufafanuzi Mkuu wa Mkoa Kijuu kwenye Mikutano ya hadhara na wananchi alipotembelea na kukagua ukarabati  wa Vituo vilivyopata fedha kutoka Serikalini alisema kuwa Vituo hivyo vilipata fedha katika awamu ya kwanza kutokana na juhudi za wananchi wenyewe katika maeneo husika kuonesha juhudi katika uchangiaji wa ujenzi wa Vituo vyao vya Afya.

Mkuu wa Mkoa Kijuu aliwahamasisha wananchi katika maeneo mengine ambayo vituo vyao havijapata fedha kutoka Serikalini kuendelea kuchaangia ujenzi wa Vituo na Zahanati ili majengo na miundombinu yote inayotakiwa ikamilike, kupitia juhudi hizo za wananchi Serikali pia itaweza kuchangia fedha kwa maeneo yale ambayo wananchi wataonesha juhudi za kuchangia maendeleo yao.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa alisistiza mambo makuu manne kama ifuatavyo, Kwanza, Vituo vya Afya vilivyopata fedha za Serikali zitumike kwa kusimamiwa na Kamati za Vituo pia watumike mafundi wa eneo husika bila kuwatumia Wakandarasi na Wakandarasi washauri katika ujenzi  ili kuepuka gharama kubwa za ujenzi aidha, ujezi uzingatie viwango kwa usimamizi wa Wahandisi wa Halmashauri.

Pili, Mkuu wa Mkoa aliwaagiza Wakurugenzi  Watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanatenga na kuyapima  maeneo ya Vituo vya Afya na Zahanati kwa manufaa ya upanuzi wa baadae na kuondoa migogoro na wananchi jirani. Tatu, wananchi wanatakiwa kuendelea kujishughulisha na kilimo ili kujipatia chakutosha na kuchangia maendeleo yao kama ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya.

Nne, wananchi, Taasisi za Serikali na zisizokuwa za Serikali zinatakiwa kupanda miti ya matunda kuzunguka maeneo ya Taasisi hizo na wananchi  wapande miti ya matunda ya aina mbalimbali isiyopungua mitano kuzunguka kaya zao ili kupunguza tatizo la utapiamlo katika Mkoa wa Kagera ambalo linatokana na wananchi wa Kagera kutokula matunda na mchanganyiko sahihi wa vyakula.

Katika hatua nyingine kwenye ziara hiyo Mkuu wa Mkoa aliambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Thomas Rutachunzibwa ambaye alipata fursa ya kuwaelimisha wananchi juu ya miundombinu inayotakiwa katika Vituo vya Afya na Zahanati ambapo ili kituo cha Afya kiitwe Kituo cha Afya kinatakiwa kuwa na miundombinu ifuatayo:

Kituo cha Afya kilichokamilika na kuruhusiwa kutoa huduma kwa wananchi kinatakiwa kuwa na Jengo la Wagonjwa nje na wagonjwa wa ndani, Jengo la Maabara, Wodi ya akinamama, Jengo la upasuaji, Wodi nyingine za wagonjwa, Vyoo vya watumishi na wagonjwa, Nyumba za watumishi wawili, Kichomea taka, Maji ya kutosha, Nishati ya umeme na Nyumba ya kuhifadhia maiti.

Dk. Rutachunzibwa aliwakumbusha wananchi katika ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa kuwa kwa sasa Serikali imetoa ramani ya ujenzi wa Vituo vya Afya na Zahanati ambapo wananchi wanatakiwa kuzingatia ramani hizo wakati wa ujenzi ili majengo ya kutolea huduma za afya yakidhi viwango.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.