• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Bw. Fred Kafeero Mwakilishi wa (FAO) nchini Tanzania Akitoa Hotuba Wakati wa Uzinduzi wa Kurejesha Hali za Wananchi Baada ya Tetemeko

Posted on: May 11th, 2017

Kaya Elfu Tano za Kagera Kunufaika na Mradi wa Kilimo na Ufugaji Ili Kurejesha Hali zao Katika Maisha ya Kawaida Baada ya Tetemeko

Kaya elfu tano (5000) za wananchi wa Mkoa wa Kagera zilizoathirika na Tetemeko la ardhi lililotokea mwaka jana Septemba 10, 2016 zatarajia kunufaika na mradi wa miaka miwili wenye thamani ya zaidi shilingi milioni 600 kupitia kilimo na ufugaji chini ya ufadhili wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO).

Mradi huo wa kurejesha hali za wananchi baada ya tetemeko chini ya ufadhili wa (FAO) ulizinduliwa rasmi Mkoani Kagera Mei 5, 2017 na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu pamoja na Mwakilishi wa (FAO) nchini Tanzania Bw. Fred Kafeero ikiwemo na wadau ambako mradi utatekelezwa.

Malengo ya mradi ni kuvisaidia vikundi vya wakulima hasa vijana na akina mama kupitia mfumo wa mashamba darasa na stadi za maisha. Kuwajengea uwezo wa matumizi ya mbinu na teknolojia zinazokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuongeza uzalishaji na kupunguza upotevu wa mazao kwa kulinda rasilimali ardhi na misitu.

Aidha, kuimarisha kilimo kinachozingatia lishe bora ili kupunguza utapiamlo hasa kwa wtoto wadogo na  kuwaelimisha wakulima na wafugaji namna bora ya kupata masoko ya mazao yao ili kujiongezea kipato.

Mwakilishi wa (FAO) nchini Tanzania Bw. Fred Kafeero alisema kuwa mradi huo utatekelezwa kwa kutumia raslimali zilizopo siyo kwamba utatekelezwa kama mradi mpya. “Tunalenga kutumia raslimali na njia ambazo tayari zilikuwepo awali mfano kutumia vikundi vya vijana na wakulima au wafugaji ambao tayari wapo ili kutekeleza mradi huu.” Alisistiza Bw. Kafeero

Bw. Kafeero alisema  kuwa mradi huo umekuja Kagera baada ya yeye kutembelea mkoani hapa mwaka jana Oktoba 16, 2017 akiwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charles Tizeba na kujionea hali ya ukame wa muda mrefu na madhara ya tetemeko jinsi vilivyoathiri uzalishaji wa chakula hasa zao la ndizi na kupelekea wananchi kukosa chakula na kipato kutokana na kutopata mavuno ya kutosha.

Katika ripoti ya utafiti wa Afya ya mwaka 2015/16 mkoa wa Kagera ulikuwa na asilimia 41.7% ya udumavu na kiwango kikubwa cha upungufu wa damu mwilini kwa watoto asilimia 39.1%  na akinamama asilimia 57.2% jambo ambalo lilionekana kuathiri matumizi ya lishe bora kwa ngazi ya kaya na kupelekea utapiamlo kwa watoto.  Pia majanga ya asili na ukosefu wa ujuzi katika kilimo kwa wakulima wadogo ni changamoto kubwa katika uzalishaji wa chakula na lishe bora kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu alilishukuru Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO)kupitia mwakilishi wake nchini Bw. Fred Kafeero kuleta mradi huo kwa wananchi wa Kagera hasa baada ya kupata majanga ya ukame na tetemeko. “Kwaniaba ya wananchi wangu nawashukuru sana kwani mradi huu utakuwa faraja kwa wananchi hasa baada ya kupata majanga ya asili.” Alisistiza Mhe. Kijuu.

Mkuu huyo wa Mkoa alitumia fursa hiyo kuwaagiza Watendaji na watekelezaji wa mradi huo kuhakikisha wantekeleza mradi huo kwa ufanisi mkubwa ambapo alisema kuwa Serikali imekuwa ikitekeleza miradi mingi lakini mwisho wa miradi hiyo hakuna tija kama inavyokuwa imetarajiwa hapo awali. Alisistiza kuona matokeo mazuri katika jamii na wananchi wenyewe mradi utakakokuwa unatekelezwa.

Mradi wa kurejesha hali za wananchi baada ya Tetemeko Kagera ambao utafadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) utatekelezwa katika Halmashauri za Wilaya za  tano ambazo ni Muleba, Kyerwa, Missenyi, Bukoba na Bukoba Manispaa.

Watekelezaji wakuu wa mradi huo ni Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kama mtekelezaji mkuu wa mradi kwaniaba ya Serikali, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera  kama msimamizi wa karibu wa mradi, Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) wafadhili wa mradi, na Halimashauri za Wilaya ambazo ndiyo wanaohusika moja kwa moja katika kutekeleza mradi huo.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.