• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Naibu Waziri Dk. Faustine Ndungulile Akiongea na Mzee Anayeishi Katika Kituo cha Wazee Kiilima Wilayani Bukoba Mkoani Kagera

Posted on: February 23rd, 2018

Naibu Waziri Ndungulile Achangisha Zaidi ya Milioni 17 Kujenga Nyumba za Watumishi Kituo cha Wazee Kiilima Mkoani Kagera

Naibu Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia  Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndungulile afanikisha  kupatikana kwa zaidi ya  shilingi milioni 17 kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa  Nyumba ya Watumishi katika Kituo cha Wazee Kiilima Kata ya Nyakato Wilayani Bukoba Mkoani Kagera.

Katika Harambee hiyo iliyofanyika Februari 22, 2018 katika Kituo cha Wazee Kiilima Dk. Ndungulile akiwa  Mgeni Rasmi alichangisha fedha taslimu milioni 7,000,000/= na kiasi cha shilingi milioni 11 zikiwa ahadi kutoka kwa wadau mbalimbali pamoja ahadi za vifaa kama magodoro, saruji,  baiskeli za wazee na mabati.

Katika hotuba yake kwa wananchi na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee hiyo Naibu Waziri Dk. Ndungulile aliwasisitiza wananchi kuwa na moyo wa kujitolea kuchangia kituo hicho ili watumishi wanaowatunza wazee wapate mazingira mazuri ya kuishi baada ya kufanya kazi yao ya kuwahudumia wazee hao.

“Serikali itaendelea kuwaunga  mkono wananchi kwa kuleta fedha katika kituo hiki ili kikamilike ujenzi wake na Wazee wetu  waweze kuhudumiwa na watumishi  ambao watawaza ni wapi pa kuishi au kukaa salama mara baada ya kufanya kazi yao ya kuwahudumia Wazee wetu,” Alisisitiza Dk. Ndungulile.

Kituo cha Kutunza Wazee Kiilima ni kituo cha Serikali kilichopo chini ya Wizara ya  Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia  Wazee na Watoto.  Kituo Hicho kilijengwa upya na Serikali baada ya kuathiriwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea Septemba 10, 2016 Mkoani Kagera.

Majengo yaliyojengwa upya na Serikali ni pamoja na Mabweni mawili ya Wanaume na Wanawake, Jiko, stoo ya kutunzia chakula, Sehemu ya kulia chakula, sehemu ya kupumzikia wazee,  vyoo viwili vya wanawake na wanaume. Changamoto iliyokuwa imebaki ni nyumba za watumishi ambazo kwa sasa zina hali mbaya ya uchakavu na hazistahili tena kuishi watu.

Fedha zilizopatikana zinatarajiwa kujenga nyumba mbili za watumishi (Two in One) ili kutatua changamoto ya watumishi wanaoishi na kufanya kazi ya kuwahudumia wazee ili wapate mahali salama pa kuishi na kutimiza wajibu wao kikamilifu bila kuwa na changamoto za sehemu za kuishi.

Katika Hatua nyingine Naibu Waziri Dk. Ndungulile alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu kwa juhudi zake za kuipatia Bohari ya Dawa (MSD)  kiwanja cha kujenga Bohari ya dawa katika Manispaa ya Bukoba na Mkoani Kagera ili kurahisisha upatikanaji wa dawa zote hapa Kagera.

Pia Dk. Ndungulile alimuomba Mkuu wa Mkoa kuhamasisha wananchi kuitikia wito wa kuwapeleka watoto wa kike miaka 4 hadi 9 kwenda kwenye vituo vitakavyokuwa vimepangwa kupata chanjo ya kansa ya shingo na uzazi kwani imeonekana kuwa kuna ongezeko kubwa la Kansa ya Shingo na uzazi katika mkoa wa Kagera.

Akimshukuru Naibu Waziri kwa kuamua kufanya ziara ya kukagua shughuli za afya Mkoani Kagera Mkuu wa Mkoa Kijuu aliomba Wizara ya Afya kuangalia upya tatizo la ugonjwa wa Malaria katika Mkoa wa Kagera kwani pamoja na juhudi zote zinazofanyika laikini kiwango cha ugonjwa huo kinazidi kupanda ambapo Naibu Waziri Dk. Ndungulile alisema tayari Wizara imeliona hilo na linafanyiwa kazi.

Naibu Waziri Dk. Ndungulile akiwa Mkoani hapa katika ziara yake ya siku mbili alivitembelea pia vituo vya Afya Kabyaile Wilayani Missenyi, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera, Kituo cha Afya Kaigara na Kituo cha Afya Kimeya Wilayani Muleba ili kukagua huduma za Afya zinavyotolewa kwa wananchi na kuongea na watumishi katika maeneo hayo.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.