• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Operesheni Ondoa Mifugo Kagera Yasonga Mbele Sasa Ng’ombe Wasakwa Kwa Ndege Zisizokuwa na Rubani Kila Pembe ya Hifadhi

Posted on: April 8th, 2017

Operesheni Ondoa Mifugo Kagera Yasonga Mbele Sasa Ng’ombe Wasakwa Kwa Ndege Zisizokuwa na Rubani Kila Pembe ya Hifadhi

Operesheni ondoa mifugo katika Hifadhi za Misitu na Mapori ya Akiba Mkoani Kagera yaendelea kwa kasi ambapo tangu kuanza kwa operesheni hiyo Machi 31, 2017 hadi kufikia Aprili 7, 2107 tayari  mifugo 4489 imekamatwa na watuhumiwa wa makosa mbalimbali 115 wametiwa mbaloni.

Mifugo iliyokamatwa ni pamoja na Ng’ombe 4328, Mbuzi 125 na Kondoo 36. Pia watuhumiwa 115 waliokamatwa kwa makosa mbalimbali  Watanzania ni 109, Warundi 4 na Wanyarwanda 2. Aidha Ng’ombe 144, kondoo 17 na mbuzi 113 wametaifishwa na Serikali baada ya watuhumiwa kushindwa kesi zao na Mahakamani kuiamurisha Serikali kutaifisha mifugo hiyo.

Serikali ya Mkoa wa Kagera katika kuhakikisha zoezi la operesheni linafanikiwa kwa asilimia 100%  imeanza  kutumika ndege zisizotumia Rubani (Drones) pia na ndege zinazotumia Rubani ili kukagua maeneo yote ambayo siyo rahisi kuonwa au kufikika na vikosi vya nchi kavu ambako mifugo hufichwa na wavamizi na kuendesha shuguli za kinadamu.

Akirusha ndege isiyotumia Rubani katika kituo Kiteule cha Nyakanazi  Bw. Parmena Pallangyo Afisa Wanyamapori kutoka Pori la Akiba la Lwikwika Lumesule lililopo Wilayani Masasi Mkoani Mtwara alisema ndege hizo zina uwezo wa kusafiri zaidi ya Kilometa 10 kwa muda mfupi zikiwa zinapiga picha mnato na picha za video kwa kuonesha viwianishi (coordinates) za kila eneo kila kitu kilichopo ardhini.

“Badala ya kuangaingaka na kutumia rasilimali magari, mafuta au rasilimali watu kwenda kutafuta mifugo katika maeneo ambayo hatuna uhakika, tunazituma kwanza ndege hizi zinatuletea taarifa za picha na eneo walipo mifugo pia picha hizo zinakuwa na viwianishi (coordinates) ambazo zinatusaidia kujua eneo husika ndipo sasa vikosi vinaelekezwa eneo husika na kwa kutumia kifaa kiitwacho GPS huwawezesha  kukamata mifugo hiyo.” Alifafanua Bw. Parmena

Wafugaji na Wafanyabiashara wa Ng’ombe wasemaje?

Katika Mnada wa Ng’ombe wa Rusahunga ambao hufanyika kila siku ya Alhamisi kila wiki wanunuzi wa Ng’ombe wanasema kuwa kwasasa Ng’ombe wanapatikana kwa wingi katika Mnada. Bw. Sena Elias Magoma mnunuzi  aliseam kuwa kwa Ng’ombe aliyekuwa anauzwa bei ya shilingi 1,200,000/=  wiki mbili zilizopita kwasasa anauzwa bei ya shilingi 800,000/= hadi 700,000/= na aliyekuwa anauzwa shilingi 500,000/= kwasasa anauzwa shilingi 300,000/= hadi 250,000/=.

Naye Bw. Fikiri Matenya Mashine  ambaye ni mfugaji alisema kuwa katika mnada huo kwa sasa Ng’ombe ni wengi kiasi kwamba bei imeshuka sana na wafugaji wanawarudisha ng’ombe wao nyumbani kwakukosa soko. Akiulizwa sababu ya ngo’ombe kuwa wengi katika mnada huo wa Rusahunga kwasasa na bei kushuka alisema;

“Mimi nadhani kutokana na ‘parancha’  (akimaanisha operesheni) linaloendelea huko maporini ndiyo maana ng’ ombe wamekuwa wengi katika mnada na pengine matajiri wanasubiri mnada wa ng’ombe ambao Serikali imewakamata ili wawanunue kwenye mnada kwa bei ya chini sana. Lakini mimi naona Serikali imefanya jambo jema hawa Wafugaji kutoka nje ya nchi wanatunyanyasa sana kama watondoka mimi naamini kuwa malisho yatatutosha sisi wenyeji.” Alifafanua Bw. Mashine

Aidha, Afisa Mifugo anayesimamia Mnada wa Rusahunga Bw. Raphael Barakekenwa alisema kwa kipindi hiki cha operesheni mifugo hasa ng’ombe wamekuwa wengi mno kiasi kwamba wanakosa soko lakini Serikali kuu na Halmashauri zinapata mapato ya kutosha kutokana na wingi wa ng’ombe mnadani. Pia alitoa angalizo kuwa kwa wiki mbili au tatu zijazo huenda kukawa na uhaba mkubwa wa nyama sokoni kwasababu ng’ombe wengi kuondolewa maporini na kusafishwa kwenda mikoani na nje ya nchi.

Vilevile katika mnada huo Mwandishi wa habari hii alishuhudia malori mengi yakiwa yanapakia ng’ombe kwa wingi na kuondoka kuelekea mikoani pia ng’ombe wengi wakiwa katika eneo hilo la mnada wa Rusahunga wakisubiri kununuliwa aidha wafugaji wengine wakiamua kurudi nyumbani na ng’ombe wao waliokosa soko katika mnada huo.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.