• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Picha ya Pamoja ya Wadau wa Chanjo MKoani Kagera Wakati wa Kikao cha Kujadili Chanjo Mpya ya Saratani ya Mlango wa Kizazi Kwa Akinamama

Posted on: April 18th, 2018

Wadau Mkoani Kagera Waweka Mikakati ya Kutoa Chanjo Mpya ya Saratani ya Mlango wa Kizazi Kwa Wasichana Waliotimiza Umri wa Miaka 14

Wadau wa wa Chanjo Mkoani Kagera wafanya kikiao cha kujadili namna bora ya kuanzisha na kutekeleza  kwa ufanisi  chanjo mpya ya Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wasichana wenye umri miaka 14 ambapo mkoa unatarajia kuchanja jumala ya wasichana 35,917 katika vituo vya kutolea huduma za Afya  1,182.

Akifungua kikao hicho  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawilo kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera  aliwasisitiza wajumbe wa kikao kuhakikisha wanawahamasisha wananchi hasa wazazi kuwaruhusu watoto wao wasichana wenye umri  wa miaka 14 kupata chanjo hiyo ambayo ni muhimu sana kwao na inatolewa bure bila malipo yoyote.

Mkuu wa Mkoa alisema kuwa  Saratani ya Mlango wa Kizazi ni ugonjwa wa kwanza Tanzania unaowaua akinamama wengi ukifuatiwa na Saratani ya Matiti, ambapo aliwasisitiza wajumbe wa kikao kuhakikisha wanawahamasisha wazazi katika maeneo yao  ili watoto wao wapate chanjo hiyo na kupunguza vifo kwa akina mama hapo mbeleni.

“Serikali ya mkoa imejipanga vizuri katika kutoa chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wasichana 35,917 katika mkoa wetu. Aidha, chanjo hiyo itatolewa katika vituo 1,182 vya kutolea huduma za afya vya Serikali na visivyokuwa vya Serikali pamoja na baadhi ya shule zitakazokuwa zimeainishwa,” Alitoa Msisitizo Mhe. Kinawilo.

Naye Dk.Siliacus Mtabuzi mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) akitoa salaam za Shirika hilo aliupongeza Mkoa wa Kagera kwa kufanya vizuri katika chanjo mbalimbali na kusema kuwa ni matarajio yake kuwa katika Chanjo hii mpya  ya Kizazi cha Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 24 Mkoa wa Kagera utafanya vizuri zaidi kwa kuwafikia walengwa wote.

Katika hatua nyingine Dk. Mtabuzi alisema kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kama mdau Mkuu wa Afya litaendelea kushirikiana kwa karibu sana na Mkoa wa Kagera ili kuhakikisha lengo la mkoa linafikiwa na wasichana wenye umri wa miaka 14 ambao ni akinamama wa kesho wasidhurike na Saratani ya Mlango wa Kizazi.

Mganaga Mkuu wa Mkoa Dk. Thomas Rutachunzibwa alifafanua namna chanjo hiyo itakvyotolewa katika Mkoa wa Kagera kwa kusema kuwa chanjo itaanza kutolewa tarehe 23 Aprili, 2018 na lengo likiwa ni kuwafikia wasichana 35,917 waliotimiza miaka 14 ambao walizaliwa kipindi cha Januari hadi Aprili 2004 na baada ya hapo zoezi litakuwa endelevu kwa wasichana watakaokuwa wanatimiza miaka 14 kila mwezi  watakuwa wanapewa chanjo hiyo.

Kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Luyango alitoa rai kwa wananchi ambao  watajaribu kupotosha utoaji wa chanjo hiyo kuwa Kamati za Ulinzi na Usalaama zitamshughulikia kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria mahala popote atakapokuwa.

Dalili za ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi ni kuishiwa damu, figo kushindwa kufanya kazi, kuvimba miguu, kutokwa na usaha wa rangi ya kahawia katika sehemu za siri za mwanamke. Aidha, visababishi vya ugonjwa huo ni kuanza mapenzi katika umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi, na kuvuta sigara.

Ili kujikinga na ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi ni muhimu sana wasichana wakazingatia kutojihusisha na visababishi vilivyotajwa hapao juu. Pia Katika Mkoa wa Kagera kuna vituo vipatavyo 56 vinavyohusika na uchunguzi wa awali wa ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi ambapo mkoa unatoa wito  kwaakina mama kuwahi mapema katika vituo hivyo pale wanapohisi dalili hizo ili kufanyiwa uchunguzi mapema.

Kikao cha wadau wa chanjo Mkoani Kagera kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Aprili 18, 2018 kiliwahusisha Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya, Waganga Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi  Watendaji wa Halmashauri, Maafisa Elimu wa Wilaya, Wadau wa Maendeleo wa Afya wa Mkoa wa Kagera, Wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na na Wataalamu wa Afya kutoka katika Halmashauri za Wilaya.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.