• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Prof. Joyce Ndalichako Akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu Funguo za Majengo ya Shule ya Msingi Mgezo Mseto Yaliyojengwa na UNICEF

Posted on: February 15th, 2018

Waziri Ndalichako Akabidhiwa na Majengo na Shule na Unicef Awaagiza TBA Kulipa Madeni na Kumaliza Mradi wa Ihungo Sekondari

Katika Siku yake ya pili Mkoani Kagera Waziri Ndalichako  alipokea majengo yaliyojengwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF katika Shule ya Msingi Mgeza Mseto ambapo  pia alikabidhi majengo hayo kwa Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu naye pia aliyakabidhi majengo hayo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba.

Katika hafla hiyo fupi Prof. Ndalichako aliwashukuru UNICEF kwa kuitikia wito wake baada ya Tetemeko lililotokea Septemba 10, 2016 ambapo aliwaomba kutoa msaada katika Sekta ya Elimu kwani miundombinu mingi ilikuwa imeadhirika, na UNICEF walikubali kutoa milioni 700 kwaajili ya Shule ya Msingi Mugeza Mseto.

UNICEF imejenga Madarasa 3, Jengo 1 la kuwapumzisha wanafunzi watakaokuwa wanaumwa, Mabweni 4 yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 190, Vyoo 2. Pia wametekeleza mradi wa maji wenye thamani ya milioni 107 na kujenga matundu ya vyoo yenye thamani ya milioni 500 katika shule mbalimbali ndani ya Manispaa ya Bukoba.

Waziri Ndalichako pia aliwashukuru wadau wengine ambao walichangia katika Shule ya Msingi Mgeza Mseto. Wadau hao ni Rotary Club waliotoa milioni 80 kwaajili ya kununulia magodoro, makabati na mashuka kwa ajili ya watoto wenye ulemavu ambao wanalala katika mabweni yaliyojengwa na UNICEF.

Bi Cecilia Baldeh Mwakilishi wa UNICEF anayeshughulikia masuala ya elimu kwa Watoto aliyemwakilisha Mwakilishi Mkazi wa UNICEF Tanzania  akiongea na wanafunzi na wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo fupi alisema kuwa UNICEF iliguswa na uhuhitaji wa shule hiyo baada ya Tetemeko kutokea mwaka 2016 na ndiyo maana waliamua kutoa fedha ili kupunguza changamoto katika shule hiyo yenye mahitaji maalum.

Pia Bi Cecilia alisema kuwa anatambua kuwa bado kuna changamoto katika shule ambapo hakuna njia za kutembelea (walka way), usafiri wa wanafunzi, nyumba za watumishi wanaowalea watoto, uzio na vifaa vya michezo ambapo alitoa wito kwa mashirika ya Kimataifa kuguswa kuchangia ili watoto hao wenye uhuhitaji maalum waishi kwenye mazingira bora zaidi.

Shule ya Msingi Mgeza Mseto ilianza mwaka 1950 ikiwa Middle School na baadae ilibadilishwa kuwa shule watoto wenye mahitaji Maalum miaka ya 1960 katika shule hiyo kuna watoto wenye mahitaji maalum 150. Manispaa ya Bukoba inazo Shule zenye mahitaji maalum 3, Shule ya Msingi Tumaini, Shule ya Msingi Mgeza Viziwi na Shule ya Msingi Mgeza Mseto.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliwashukuru UNICEF pamoja na Waziri Ndalichako kwa ufadhili wao wa kuhakikisha miundombinu ya shule hiyo inaimarishwa na kuonesha moyo wa kusaidia mara baada ya Tetemeko kutokea mwaka 2016  ambapo alisema kuwa wananchi wa Kagera walifarijika na wataendelea kufarijika kwa kuona miundombinu ya shule zao inarejeshwa na inaimarishwa zaidi kuliko hata mwanzo.

Ihungo Sekondari, Mara baada ya Hafla ya Makabidhiano Shule ya Msingi Mugeza Mseto Waziri Ndalichako alitembelea Shule ya Sekondari Ihungo kuona maendeleo ya ujezi wa shule hiyo ambapo aliridhishwa sana na kiwango cha ujenzi wa shule hiyo na kuwapongeza wajenzi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kujenga shule hiyo kwa viwango vya hali ya juu sana.

Pamoja na pongezi hizo Waziri Ndalichako aliwataka TBA kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo mara moja ili wanafunzi waweze kurejea katika shule yao na kuendelea na masomo yao. Pia Waziri Ndalichako alisema kuwa Wizara yake tayari imetoa bilioni 9.13 kati ya bilioni 10.48 fedha za kutekeleza mradi mzima wa Ihungo Sekondari.

Waziri Ndalichako alisema hayo baada ya kupokea taarifa ya Meneja wa TBA Mkoa wa Kagera  Mhandisi Salum Chanzi kuhusu mradi huo na kusikia kuwa kuna wazabuni , vibarua na mafundi wanaodai fedha zao baada ya kutoa huduma za vifaa mbalimbali vya ujenzi na huduma katika ujenzi huo wa Ihungo.

Wizara yangu tayari imetoa kiasi kikubwa cha fedha  bilioni 9.13 na tumebaki tunadaiwa milioni 715 tu na fedha iliyobaki ni asilimia 5% itakayolipwa baada ya kujihakikishia kuwa kila kitu kimekamilika. Nawataka TBA kumaliza mradi pia kuhakikisha wanawalipa wanaowadai na siyo mapaka wamalize mradi kwani fedha wanayo wao, Alisistiza Prof. Ndalichako.

Shule Sekondari Nyakato, Waziri Ndalichako pia alipata wasaa wa kutembelea Shule ya Sekondari Nyakato kuona maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo  ambapo mjenzi ni SUMA JKT na ujenzi umefikia asilimia 60% kwa sasa baada ya kuanza Septemba 21, 2017 na unatarajia kukamilika Septemba 20, 2018.

Waziri Ndalichako aliwapongeza SUMA JKT kwa kujenga majengo ya shule hiyo kwa viwango lakini pia kwa kwenda na muda ambao ujenzi unatarajia kukamilika. Ujenzi wa Shule ya Sekondari Nyakato utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.2 Ikumbukwe kuwa Shule za Sekondari Ihungo na Nykato ziliathiriwa vibaya na Tetemeko la Ardhi mwaka 2016 na zinajengwa upya na Serikali.

Waziri Ndalichako pia alizitembelea Shule za Sekondari Omumwani Rugambwa na kuongea na wanafunzi na uongozi wa shule hizo huku akisistiza wanafunzi kuongeza bidii katika masomo yao.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.