• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Profesa Kamuzora Ahitimisha Wiki ya Utumishi wa Umma Kagera Kwa Kuwakumbusha Watumishi Wajibu Wao wa Kuchapa Kazi Kwa Uadilifu

Posted on: June 25th, 2019

Wiki ya Utumishi wa Umma Mkoani Kagera yahitimishwa na Katibu Tawala Mkoa Profesa Faustin Kamuzora ambaye ni msimamizi mkuu wa watumishi wa umma katika Idara na taasisi zote za umma mkoani humo ambapo alihitimisha kwa kuongea na watumishi hao katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera.

Profesa Kamuzora akiongea na watumishi hao kutoka Idara, Taasisi, Serikali za Mitaa na Serikali Kuu aliwakumbusha wajibu wao wa  kuwahudumia wananchi kwa kutumia muda mfupi sana lakini kutekeleza majukumu au shughuli nyingi za kuwaletea wananchi hao maendeleo.

“Sote tunajua kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imefanya uhakiki na kuwaondoa watumishi ambao walikuwa hawastahili kuwa watumishi wa umama na sisi tuliobaki tunatakiwa kuufurahia utumishi wa wetu kwani sasa Serikali imeanza kurekebisha maslahi yetu kwa kupandisha vyeo na kurekebisha miundo ili kila mtumishi apate anachostahili kulingana na miundo ya utumishi wa umma iliyopo.” Alisisitiza Profesa Kamuzora.

Kwa upande mwingine Profesa Kamuzora alitoa rai kwa Watumishi wa Umma mkoani Kagera kuhakikisha wanatumia fursa za uwepo wa Hifadhi za Taifa za Chato - Burigi, Ibanda na Rumanyika kuzitembelea hifadhi hizo ili kupumzisha akili lakini pia kuangalia fursa ambazo zinaweza kuingiza kipato kwao kuzichangamkia ili kujiongezea kipato kuliko kuacha na fursa hizo zinachukuliwa na watu toka nje ya mkoa wakati zipo wazi kwa kila mmoja.

Fursa ya pili alioingelea kwa watumishi Profesa Kamuzora ni kuhusu Bomba la mafuta kutoka Ohima nchini Uganda kwenda mkoani Tanga litakaloingilia  Mkoani Kagera kuhakikisha kila mtumishi anatimiza wajibu wake na kufanya kila liwezekanalo katika nafasi yake kutokwamisha bomba hilo kuanza kufanya kazi kama inavyotarajiwa kufanyika.

Tatu Profesa Kamuzora aliwakumbusha watumishi wa umma kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu 2019 lakini watumishi hao wanatakiwa kuzingatia kanuni na taratibu za utumishi wa Umma ambazo zinaelekeza namna mtumishi anavyoweza kushiriki katika Uchaguzi bila kuvunja sheria zilizowekwa.

Aidha, Profesa Kamuzora aliwataka viongozi wa taasisi, na mbalimbali za Serikali kuhakikisha wanatoa motisha kwa watumishi walio chini yao ili kuwatia moyo na morali wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mahala pa kazi na kufikia lengo la Serikali ya Awamu ya Tano la kuufikia Uchumi wa Kati.

Profesa Kamuzora aliendelea kusisitiza watumishi wa Umma wa Mkoa wa Kagera kuongeza jitihada za kutoa elimu ya lishe kwa wananchi kwani mkoa pamoja na kuwa na vyakula vingi lakini tatizo la udumavu bado lipo juu. Tatizo si vyakula bali elimu kwa wananchi kujua namna bora ya kula au kutumia vyakula vya aina mbalimbali walivyonavyo.

“Unaweza kuona kuwa kuna shida katika hili na sitaki kuamnini au kulilinganisha hili la udumavu na ninacotaka kukisema , juzi nilikwenda Mkoani Ruvuma kuona timu yetu ya Mkoa ya UMISETA inavyoshiriki mashindano lakini namba walioshika vijana wetu inaedana na namba ya udumavu katika mkoa wetu, sasa sisi kama watumishi wa umma tunalo jambo lakufanya inamaana kwenye ligi ya maendeleo kuna sehemu hatutimizi majukumu yetu ipasavyo.” Alikazia Profesa Kamuzora  

Naye Bw. Abbas Marikela Mkuu wa Hazina Ndogo Mkoani Kagera akitoa maoni yake katika kuhitimisha Wiki ya Utumishi wa Umma alitoa wito kwa Maafisa Utumishi katika Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali kutunza nyaraka za watumishi hasa wastaafu kwani wanapata shida sana wanapokutana na malezo tofauti na nyaraka zao walizonazo.

Bw. Abbas alitoa mfano kuwa watumishi wastaafu wengi unakuta hawapo katika masharti ya kudumu ya utumishi wa umma lakini wanakuwa hawajui na Maafisa Utumishi wao hawawaelezi jambo ambalo huleta usumbufu kwa mstaafu mwenyewe lakini pia na ofisi za hazina za mkoa kumbe kama Afisa Utumishi kama angetekeleza wajibu wake tatizo hilo lisingejitokeza.  

Mwisho katika kuhitimisha Wiki ya Utumishi wa Umma Mkoani Kagera iliyoanza Juni 19 hdai 25, 2019 watumishi wa umma walikumbushwa na kushuriwa kula vizuri, kupumzika kwa mda mrefu na kuomba ushari pale wanapokwazika au kukumbwa na matatizo kuliko kukaa kimya  kuwa ni tiba kwa kiwango kikubwa  kwa afya zao bila kusahau kufanya mazoezi ya mara kwa mara kuiweka miili yao imara.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.