• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Rais John Magufuli Akikagua Shehena ya Sukari Katika Kiwanda cha Kagera Sugar Missenyi Mkoani Kagera

Posted on: November 9th, 2017

Rais Magufuli Ardhishwa na Uwekezaji wa Kiwanda Cha Kagera Sukari Asema Serikali Itaendelea Kukiunga Mkono

Rais Magufuli akiendelea na ziara yake  Mkoani Kagera leo Novemba 8, 2017 katika siku ya tatu alitembelea Kiwanda cha Kagera Sukari kilichopo Wilayani Missenyi ambapo amempongeza mwekezaji wa kiwanda hicho Bw. Seif Seif  kwa kuwekeza mtaji mkubwa katika kiwanda hicho.

Akiwa katika kiwanda hicho Rais Magufuli alitembelea mashamba ya kiwanda na kujionea jinsi mashamba yanavyoandaliwa kisasa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu katika umwagiliaji na jinsi sukari inavyozalishwa aidha na kujionea shehena ya sukari ambayo tayari imezalishwa  tayari kuingizwa sokoni.

Aidha Rais Magufuli alipongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kutoa kipaumbele katika ajira kwa Watanzania wazalendo waliohitimu masomo yao katika Vyuo Vikuu vya hapa nchini na kuwaendeleza kielimu katika nchi za nje mara baada ya kuajiriwa katika kiwanda cha Kagera Sukari ili kupata ujuzi wa kilimo cha miwa ambapo hadi sasa kiwanda hicho kimeajiri wafanyakazi 5,000.

Hadi sasa Kiwanda cha Kagera Sukari kinazalisha tani 65,000 hadi tani 67,000 kwa mwaka ambapo Rais Magufuli alitoa maelekezo kiwanda hicho kizalishe tani 75,000 kufikia mwaka kesho 2018 na kuwahakikishia wenye viwanda vya sukari nchini kuwa soko la sukari lipo kubwa kwahiyo wanatakiwa kuzalisha zaidi.

“Kiwanda cha Mtibwa kinzalisha tani 30,000 TPC tani 100,000 Kilombero tani 109,000 Manyara tani 6,000 ukiunganisha na tani za Kagera Sukari kwaujumla  tani zinazozalishwa nchini ni 320,000 wakati mahitaji tani 450,000 na upungufu ni tani 130,000. Ukiangalia wingi wa watu Afrika Mashariki ni milioni 165 na nchi za SADC ni milioni 400 hilo ni soko kubwa la sukari,” Alibainisha Rais Magufuli.

Rais Magufuli aliwataka wenye viwanda kumhakikishia kuwa wanao uwezo wa kuzalisha sukari kwa kiwango chote cha mahitaji tani 450,000 ili Serikali ipige marufuku uingizwaji wa sukaria nchini ambapo alisema kuwa sukari hiyo inayoingizwa nchini wakati mwingine ni ya viwandani na wafanyabiashara waroho wanaiuza kama sukari ya matumiazi ya binadamu.

“Nawataka mnihakikishie kuwa mna uwezo wa kuzalisha sukari tani 450,000 na wakati mnapofunga viwanda kama kutakuwepo na upungufu nyie wenyewe muagize sukari toka nje hapo nitakuwa tayari kufuta uingizwaji Sukari nchini. Lakini sharti ni kwamba sukari toka nje muiagize nyinyi wenye viwanda na siyo kuwapa vibali wafanyabaiashara,” Alisistiza Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli aliwaagiza Mawaziri wa Kilimo, Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji kufanya upembuzi yakinifu katika viwanda vyote vinavyotumia sukari ili kujua matumizi halisi katika viwanda vyao na atakeyebainika anaagiza sukari ya viwandani zaidi ya matumizi yake afikishwe mahakamani kwa hatua za kisheria

Aidha Bw. Seif Seif kwaniaba ya Bodi ya Wakurugenzi wa Kiwanda cha Kagera Sukari na wafanyakazi wa Kiwanda hicho aliishukuru Serikali ya Rais magufuli kwa kuwapa ushirikiano katika kuendesha kilimo na kuzalisha sukari.

Aidha rais Magufuli alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano kuhakikisha wakandarasi wanakuwepo katika eneo linapotakiwa kujengwa daraja katika mto Kagera litakalozinganisha Wilaya za Karagwe na Missenyi ili kurahisisha usafirishaji wa miwa kutoka katika Wilaya ya Karagwe kuja kiwandani.

Raisi Magufuli alimalizia hotuba yake kwa wananchi na wafanyakazi wa Kiwanda cha Kagera Sukari kwa kuwaomba wawekezaji kuwekeza katika Mkoa wa Kagera na ili uwe Mkoa wa uwekezaji ambapo aliwataka Kagera Sukari kuanziasha Kiwanda kingine cha Kutengeneza pombe kali kutokana na morasisi na wananchi kuanzisha viwanda vidogovidogo kama vya senene na vinginevyo.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 Kupitia Miradi Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 23.8

    September 07, 2025
  • Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025 Kupitia Miradi Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 23.8

    September 07, 2025
  • Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera Yafungu Dawati Maalu la Uwezeshaji Wafanyabiashara

    September 03, 2025
  • Nsekela Stadium Yazinduliwa Rasmi Kyerwa - Kagera

    August 29, 2025
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.