• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Rais John Magufuli (wa Nne Kutoka Mkono wa Kulia) Akikata Utepe Kuashiria Uzinduzi wa Barabara ya Kagoma Rusahunga Mjini Biharamulo

Posted on: July 19th, 2017

Rais Magufuli Azindua Rasmi Barabara ya Kagoma Rusahunga Mkoani Kagera

  • Atoa Siku 14 Kwa Wafanyabiashara wa Vituo vya Mafuta Nchini Kufunga Mashine EFD

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuri katika siku yake ya kwanza ziarani Mkoani Kagera azindua rasmi barabara ya Kagoma Rusahunga yenye Kilometa 154 ambayo imejengwa na kukamilika kwa kutumia fedha za ndani bila wafadhili ambapo jumla ya shilingi bilioni 190.4 zimetumika.

Akiongea na wananchi kabla ya uzinduzi wa barabara ya Kagoma Rusahunga Wilayani Biharamulo Rais Magufuli alisema barabara hiyo ilizinduliwa mwaka 2013 na Rais Jakaya Kikwete lakini wakati yeye akiwa Waziri wa Ujenzi na Serikali iliamua kujenga barabara hiyo kwa fedha zake za ndani baada ya miaka ya 1990 kumfukuza Mkandarasi ambaye hakukidhi viwango  na Kupelekea Benki ya Maendeleo ya Afrika kujiondoa katika ufadhili wa barabara hiyo baada ya Mkandarasi kufukuzwa.

Rais Magufuli aliwapongeza wananchi kwa kuitikia kulipa kodi na kusema kuwa hayo ndiyo matunda ya ulipajia kodi. “Kodi mnazolipa wananchi zinajenga barabara kama hizi ambazo zinafungua fursa za kukuza uchumi kwa wananchi na ndiyo maana nimekuwa nikisistiza sana wananchi kulipa kodi kwa hiari ili Serikali iweze kuwaletea maendeleo.” Alisistiza Rais Magufuli.

Ulipaji wa Kodi kwa Mashine za Kielekroniki

Rais Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya mafuta nchini kuhakikisha wanafunga Mashine za Kielekroniki (EFD)  katika vituo vyao, aidha, mfanyabiashara yeyote atakaye kiuka agizo hilo  Waziri wa Fedha na Waziri wa Viwanda wameagizwa kuchukua hatua za kuvifungia vituo hivyo mara moja na ikiwezekana visifunguliwe tena.

“Katika nchi hii tumekuwa tukiwatoza sana kodi wananchi wanyonge pamoja na wafanyakazi tu lakini wafanyabiashara wamekuwa wakifanya biashara bila kulipa kodi na kupata faida kubwa wakati wale wanaotakiwa kutozwa kodi tunawaacha tu. Jambo hili haliwezi kuendelea katika Serikali ya Awamu ya Tano.” Alikemea Rais Magufuli

Kodi za Kero kwa Wakulima 

Rais akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Biharamulo aliwaambia kuwa Serikali yake imeamua kuondoa kodi za kero kwa wananchi  wanaojishughulisha na kilimo ambapo tozo zaidi ya 80 zimefutwa  na mkulima anayesafirsha mazao yake yasiyozidi tani moja kutoka Halimashauri ya wilaya moja  kwenda nyingine hatakiwi kubugudhiwa na aina yoyote ya ushuru.

Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa Serikali imeamua kufuta kodi za kero kwa zao la kahawa ambao aliwaagiza Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya kusimamia wananchi wasibugudhiwe tena na kodi zenye kero. Katika mifugo Rais Magufuli alisema kuwa kwenye minada kumekuwa utozaji wa  ushuru wa hovyo hadi ushuru wa kwato ambapo aliagiza kuwa mifugo isiyofikia idadi ya mitano haitakiwi kutozwa ushuru.

Kuhusu Operesheni ya Mifugo Kagera

Rais magufuli aliwaambia wananchi kuwa operesheni iliyofanyika Mkoani Kagera kuondoa Mifugo katika Mapori ya Akiba, Vyanzo vya Maji na Misitu ya hifadhi aliagiza yeye Rais ifanyike kutokana na wafugaji kuvamia maeneo hayo ya hifadhi na kufanya uharibifu mkubwa  hasa katika Mapori ya Akiba ambapo wanyamapori walikuwa wametoweka kabisa.

“Serikali haiwezi kuvumilia vitendo hivyo,  wafugaji mnatakiwa kupunguza mifugo yenu kwa kuivuna na kufuga kisasa, hata mimi juzi nimevuna ng’ombe wangu na kuuza kwasababu nimeona siwezi tena kuwafuga wote. Kwanini nyinyi wafugaji msiwavune hao ng’ombe wenu mkajenga na nyumba? Mnawakaribisha wafugaji kutoka nje lakini kwao wanatunza mazingira yao, hatuwezi kuvumilia kadhia hiyo.”  Aliwaonya wafugaji Rais Magufuli.

Rais Magufuli alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Wakuu wa Wilaya kwa kutekeleza na kusimamia vizuri zoezi la Operesheni Ondoa Mifugo Kagera na kuwataka kuendelea kusimamia kwa karibu mifugo isirudi katika maeneo ya hifadhi pia aliagiza mtumishi wa idara ya Wanyamapori aliyekuwa amesimamishwa kazi kurudishwa kazini mara moja na kupandishwa cheo kwani alikuwa anatekeleza majukumu yake ipasavyo.

Wachimbaji wadogo

Rais magufuli aliwaambia wananchi kuwa wachimbaji wadogo wamekuwa wakinyanyaswa mara baada ya kugundua sehemu zenye madini kama dhahabu ambapo aliagiza Wizara ya Nishati na Madini kuhakikisha wachimbaji wanapewa leseni katika maeneo waliyoyagundua wao na kuacha kuwanyanyasa kwa kuwafukuza na kuwapa wawekezaji kutoka nje.

Afya na Elimu 

Rais Magufuli aliwaambia wananchi kuwa Serikali yake sasa imeongeza bajeti afya kutoka bilioni 31 hadi bilioni 250 na Serikali imeanza kununua dawa yenyewe ambapo bei za dawa zinatarajia kushuka zaidi kwani Serikali itakuwa inaziuza yenyewe kwa bei ndogo. Aidha, alisema Serikali inaendelea kutekeleza Elimu Bure kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli alitoa siku 10 kwa Mkandarasi anayetekeleza mradi wa Maji Biharamulo na Msimamizi wake Mamlaka ya Maji Saji na Maji Taka Bukoba (BUWASA) kuhakikisha maji yanaanza kutoka katika mji wa Biharamulo. Rais Magufuli ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya Ngara tarehe 20 Julai, 2017 ambapo anatarajia kuongea na wananchi katika mkutano wa hadhara

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.