• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Rais wa Burundi Mhe. Nkurunziza (Wakwanza Kushoto) Akiwa na Rais Magufuli Wilayani Ngara Mkoani Kagera Mbele ya Wananchi Kwenye Mkutano wa Hadhara.

Posted on: July 20th, 2017

Rais Magufuli Afanya Mazungumzo na Rais wa Burndi Nkurunziza na Kukubaliana Kufufua Fursa za Kiuchumi Kati ya Nchi Mbili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli afufua rasmi mazungumzo ya Kiuchumi na Nchi ya Burundi baada ya kukuta na Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunziza Wilayani Ngara Mkoani Kagera na kufanya naye mazungumzo ya kuanzisha ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na nchi ya Burundi.

Rais Dkt. Magufuli akiongea na wananchi baada ya kufanya mazungumzo na mgeni wake  Rais Nkurunziza alisema mwaka 2013 yalifanyika mazungumzo kati ya nchi za Tanzania na Burundi ambapo Mawaziri wa fedha wa nchi hizo  walikutanana na kuanzisha mazungumzo ya kibiashara kati ya nchi mbili ambapo kwasasa wamezungumza kufufua upya mazungumzo hayo ili kuanzisha ushirikiano wa kibiashara .

“Kwa takwimu za mwaka 2016 zinaonyesha kuwa biashara zilizokuwa zinafanyika kati ya Tanzania na Burundi zilikuwa zina thamani ya shilingi bilioni 116.5 ambazo biashara hizo ni kidogo sana ukilinganisha na watu milioni 50 Watanzania  na watu zaidi ya milioni 12 Warundi, kwahiyo kuna haja ya kukuza na kuimarsha biashara kati ya nchi zetu mbili.” Alifafanua Rais Dkt. John Magufuli.

Aidha, Rais Dkt. Magufuli alimpongeza Rais Nkurunziza kwa juhudi zake za kuendelea kuimarisha amani na usalama na kuwataka Wakimbizi kutoka nchi ya Burundi kurudi kwao kuijenga  nchi yao kwani tayari kuna amani na utulivu . Pia aliyakemea Mashirika ya kuwahudumia Wakimbizi kuacha kuwapotosha Wakimbizi hao kuwa kwao hakuna amani aidha, alisema kuwa tayari anajua kuwa Mashirika hayo ya Kimataifa yanatumia mwanya huo kuwatumia Wakimbizi kama Biashara.

Rais Dkt. Magufuli pia alimwagiza Waziri wa Mambo ya Ndani kuacha kutoa uraia kwa wakimbizi kuwa hicho kinaweza kuwa kivutio  kwa Wakimbizi kuendelea kuingia nchini Tanzania hata kama kwao hakuna vita.  Vilevile aliwataka Warundi kuishi kwa mshikamano kama Tanzania ambapo alisema kuwa hapo awali Tanzania ilikuwa na makabila 121 lakini kwa sasa kuna makabila 123 mawili yameongezeka  ambao ni Wahutu na Watutsi wapatao 200,000 waliopewa uraia  kuwa Watanzania.

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ya Tanzania Mwigulu Nchemba alipewa nafasi na Rais Dkt. Magufuli na  kusema kuwa kwasasa Wakimbizi kutoka nchi ya Burundi waliopo Tanzania ni 247,000 na tayari kuna Wakaimbizi 150,000 waliondoka kwa hiari yao na tayari wengine 5000 wamejiandikisha kurudi kwao kwa hiari.

Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Wilaya ya Ngara na Watanzania kwa ujumla aliishukuru nchi ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa pamoja na nchi yake ya Burundi. Pia alisema kuwa katika mazungumzo yake na Rais Dkt. Magufuli yamefungua mwanzo mpya  wa fursa za kibiashara baina ya nchi mbili.

Vile vile  Rais Nkurunziza alitoa wito kwa Watanzania kuanza kufanya biashara na nchi yake ya Burundi na alisema kuwa anaona kuwa hapo mbele mambo yatakuwa sawasawa  kati ya nchi hizi mbili na watoto wa nchi hizo mbili watakuwa na mambo mazuri hapo mbeleni.

Aidha, Rais Nkurunziza  alitoa wito kwa Wakimbizi Warundi walioko nchini Tanzania kurudi kwao Burundi kwenda kushirikiana kuijenga nchi yao kwani amani imerejea kwa sasa hakuna vita tena. “Nawaomba Warundi wenzangui walipo mrudi nyumbani ili tukaijenge nchi  yetu na kukuza uchumi na tuweze kunufaika kwa pamoja na watoto wetu.  Alisistiza Rais Pierre Nkurunziza.

Katika Hatua nyingine Rais Dkt.  John Pombe Magufuli aliwaeleza wananchi wa Wilaya ya Ngara na taifa  kwa ujumla kuwa Serikali yake inaendelea kuwaletea maendeleo katika Sekta mbalimbali, mfano Katika Afya Serikali tayari imenunua vitanda vyenye thamani ya  Bilioni 33 na itavigawa katika Hospitali zote za Serikali nchini.

Aidha,  Serikali imenunua vifaa vya mahabara na na kuvigawa katika shule 1900, na imetenga shilingi bilioni 483 kwaajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu. Vilevile  Serikali inatarajia kujenga upya barabara ya Nyanazi hadi Ngara ambayo ina mashimo mengi kwasasa na kujenga barabra ya Nyakahura Rulenge kilometa 92 kwa kiwango cha rami.

Katika Siku yake ya pili Rais Dkt. Magufuli Mkoani Kagera alimpokea kwa heshima zote za kitaifa Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunziza katika uwanja mpira wa Lemela Wilayani Ngara majira ya saa 5:00 asubuhi na Rais Nkurunziza alipigiwa mizinga ya heshima 21 na kukagua Gwaride. Aidha, baada ya kukamilisha ziara yake na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunziza alirudi nchini Burundi.

Katika Mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunziza Rais Dkt. Magufuli aliambata na Mawaziri wa Wizara za Mambo ya Ndani Mwiguru Nchemba, Wizara ya Fedha Dk. Philip Mpango, Wizara ya Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi, Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbalawa, na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Naibu Wazi Dkt. Suzan Kolimba  pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Kitaifa.

Rais Dkt. Magufuli amemaliza ziara yake ya siku mbili Mkoani Kagera na anatarajia kuelekea Mkoani Kigoma Juni 21, 2017 kuendelea na ziara yake ya kazi.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.