• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Sipo Tayari Kuona Magendo ya Sukari Inaendelea Katika Mkoa wa Kagera Wakati Tunazalisha Sukari Katika Mkoa Wetu – RC Gaguti

Posted on: September 19th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti atembelea kiwanda cha Kagera Sukari kilichoko Wilayani Missenyi na kuhaidi kushughulikia masuala makuu matatu ambayo yanasababisha kiwanda hicho kuzalisha sukari ya kutosha lakini kwasasa inakosa soko kutokana na sukari kutoka nje ya nchi kuingizwa kimagendo katika masoko ndani ya nchi.

Akiwa kiwandani hapo Septemba 18, 2018 lengo likiwa ni  kutembelea kiwanda hicho na kuona changamoto ambazo zinasababisha sukari kukwama kwenda sokoni Mkuu wa Mkoa Gaguti baada ya kupokea taarifa ya kiwanda hicho iliyowasilishwa kwake na Meneja Mkuu wa Kiwanda Bw. Ashwin Rana alibainisha mambo makuu matatu ambayo alisema kuwa atayafanyia kazi ili kutatua changamoto ya sukari ya magendo kutoka nje ya nchi.

Kwanza, Magendo ya Sukari kutoka nje ya nchi, Mkuu wa Mkoa Gaguti akilitolea ufafanuzi suala hilo alisema kuwa hayupo tayari kuona suala hilo linaendelea katika Mkoa wa Kagera na atahakikisha anakomesha magendo ya sukari kwa njia yoyote ile ili kulinda soko la kiwanda cha Sukari Kagera. “Kwa kutumia Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi tutahakikisha suala hilo linakomeshwa mara moja.” Alifafanua Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Pili, Mkuu wa Mkoa Gaguti ili kutatua kero ya sukari kutoka Kiwanda cha Sukari Kagera kukosa soko na kupelekea kiwanda hicho kuwa na shehena kubwa ya sukari ambayo haitoki alitoa ushauri kwa uongozi na menejimenti ya kiwanda hicho kuangalia upya mfumo wao wa usambazaji wa sukari katika masoko kuwa rafiki kwa wafanyabiashara  na usiokuwa na mashariti magumu sana ili kuhakikisha sukari inasambaa kila kona kudhibiti sukari ya magendo kutoka nje ya nchi katika soko la ndani.

Tatu, Mkuu wa Mkoa Gaguti aliushauri pia Uongozi na Menejimenti ya kiwanda  cha Kagera kuangalia bei ya sukari yao  katika masoko ili kuendana na bei ya viwanda vingine vya nchini kiushindani jambo ambalo litapunguza ushindani wa wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kuingiza sukari ya magendo kutoka nje ya nchi au kuagiza sukari kutoka katika viwanda vya mikoa mingine wakati Kagera kunzalishwa sukari ya kutosha.

“Hivi karibuni natarajia kukutana na Wakuu wa Mkioa ya Kanda ya Ziwa Mkoani Shinyanga katika mambo muhimu nitakayozungumza nao mojawapo ni suala la kudhibiti magendo ya sukari na kuona namna bora ya kuhakikisha kiwanda cha Sukari Kagera kinasambaza sukari katika mikoa hiyo na kuweka mikakati endelevu ya kuvilinda viwanda vyetu vya ndani maana nimejionea shehena ya suakari ilivyo hapa ni ya kutosha.” Alisisitiza Mkuu wa Mkoa Gaguti

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti alipongeza juhudi za kiwanda hicho katika uwekezaji kwa kuweza kuzalisha hadi tani 75,000 za sukari kwa msimu wa mwaka 2017/2018 ulioishia mwezi Juni 2018. Pia alipongeza juhudi za kiwanda kuzalisha ajira 6,000 kwa wananchi wenye takribani familia 30,000. Aidha, alipongeza  huduma zinazotolewa pia kiwandani hapo kwa jamii mfano huduma za matibabu zinazotolewa bure kusaidia wafanyakazi na wananchi wanaozunguka kiwanda cha Sukari Kagera.

Kiwanda cha Sukari Kagera tangu kuanza uzalishaji wa sukari katika msimu wa mwaka huu 2018/2019 mwezi Julai tayari kimezalisha jumla ya tani 26,000 za sukari na matarajio ya uzalishaji kwa msimu mzima ni tani 84,000 za sukari. Aidha, tani 12,800 za sukari bado hazijaingia sokoni  na bado zipo katika kiwanda hicho kutokana na tatizo la sukari ya magendo katika masoko.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.