• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Timu ya Wataalam Kutoka Nchini Iliyofika Mkoani Kagera Kukagua Eneo la Ujenzi wa Chuo cha Kisasa Cha VETA Kagera.

Posted on: April 6th, 2018

Timu ya Wataalam wa Ujenzi Kutoka Nchini China Yakagua Eneo la Ujenzi wa Chuo Cha Veta Kagera Ili Kuanza Ujenzi Mara Moja

Serikali ya Watu wa China yatuma  timu ya Wataalam  wa Usanifu wa Majengo na  ujenzi  kukagua na kujiridhisha na eneo lililotengwa na Serikali ya Mkoa wa Kagera kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Kisasa cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kinachotarajiwa kujengwa  kwa ufadhili wa Serikali ya Watu china Mkoani Kagera katika Kijiji cha Burugo  Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.

Timu hiyo ya Wataalamu kutoka katika Kampuni ya ujenzi ya “China Qiyuan Enginering Coorparation” ikiongozwa na Bw. Fang Ke Feng  walimueleza Mkuu wa Mkoa Kagera Ofisini kwake walipofika kumsalimia kuwa wamekuja kuona eneo la chuo cha VETA kitakapojengwa ili waweze kuchora michoro ya majengo inayoendana na eneo husika.

Baada ya kufika katika eneo la Burugo kitakapojengwa Chuo cha VETA Mkoa wa Kagera Wataalam hao kutoka nchini China  wakiongozwa na Msanifu Majengo Bw. Fang Ke Feng waliridhishwa na eneo hilo na kusema kuwa ni eneo zuri linalofaa kwa ujenzi na michoro wanayotarajia kuichora itaendana na eneo hilo.

“Tumeona eneo ni zuri sana, Serikali ya Mkoa imefanya kazi yake ya kufikisha miundombinu ya umeme na barabara katika eneo la ujenzi, pia tumeridhika na juhudi zinazoendelea kufanyika ili kuhakikisha maji yanapatikana katika eneo hili na jambo lakufurahisha Ziwa Victoria lipo karibu sana kwa upatikanaji wa maji katika ujenzi,” Alieleza Bw. Fang Ke Feng.

Vilevile kiongozi wa Timu hiyo ya wataalamu kutoka Nchini China Bw. Fang Ke Feng alisema kuwa baada ya kuona eneo husika sasa itachukua muda wa miezi miwili kabla ya ujenzi kuanza kutoka sasa ambapo watasanifu  michoro ya majengo na kuiwasilisha Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ili iidhinishwe na ujenzi utaanza mara moja.

Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bw. Enock Kayani alisema kuwa ujenzi wa chuo hicho utagharimu jumla ya Shilingi bilioni 22.4 pia katika awamu ya kwanza  chuo kitadahili wanafunzi 400 na awamu ya pili wanafunzi 400 na kukamilisha jumla ya wanafunzi 800 mara baada ya chuo hicho kuwa kimekamilika.

Pia Bw. Enock alisema kuwa tayari Serikali imeanza kuwaandaa wakufunzi  wa ufundi katika chuo cha VETA Morogoro ili kujiandaa mapema kwaajili ya kuwafundisha wanafunzi watakaodahiliwa katika chuo cha VETA Kagera. Pia alisistiza kuwa Walimu hao watapelekwa nchini china kujifunza zaidi kwani mara baada ya Chuo kukamilika kitakuwa na Mashine za kisasa zinazohitaji ujuzi zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu akiongelea ujio wa wataalam hao kutoka nchini China alisema amefurahishwa sana na ujio wao kwani uongozi wa mkoa na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakisubiri kwa hamu kubwa ujenzi wa chuo hicho kuanza na Serikali ya mkoa tayari imefanya majukumu yake ya kuhakikisha miundombinu ya umeme na barabara imefika katika eneo husika.

Mwenyekiti wa Kiji ji Burugo  Bw. Samson K. Simon akiongea na Timu ya Wataalamu kutoaka Nchini China Alisema kuwa imekuwa furaha kubwa kwake na wanakijiji wa Burugo kwani wamekuwa wakisubiria kwa hamu sana ujenzi wa chuo hicho kuanza na ni matarajio yao kuwa watapata ajira mbalimbali za kuinua vipato vyao pia ujenzi wa chuo hicho utainua sana uchumi wa kijiji chao.

Katika hatua nyingine Timu ya Wataalamu kutoka nchini China ilipata wasaa wa kutembela Shule ya Sekaondari Ihungo iliyopo Manispaa ya Bukoba inayojengwa upya na Serikali ya Tanzania mara baada ya kuharibiwa vibaya na Tetemeko la Ardhi lililotokea Septemba 10, 2016. Lengo la Timu hiyo kufanya ziara katika Shule ya Sekondari Ihungo ni kujionea ubora wa majengo yanayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.