• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Usichukulie Poa Nyumba ni Choo Kuzinduliwa Kanda ya Ziwa Mkoani Kagera Kupambwa na Mrisho Mpoto Pamoja na Fainali za JPM Bodaboda Cup 2019

Posted on: May 24th, 2019

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuzindua Kampeini ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira yenye kauli mbiu isemayo  “Usichukulie Poa, Nyumba ni Choo” katika mkoa wa Kagera Mei 25, 2019.

Akitoa ufafanuzi wa Kampeini ya “Usichukulie Poa, Nyumba ni Choo” Mkuu wa Mkoa Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti katika mkutano na vyombo vya habari alisema kuwa anaishukuru Serikali kuamua kufanya uzinduzi wa kampeini hiyo kwa  Kanda ya Ziwa katika Mkoa wa Kagera ili kuhamasisha wananchi kujenga vyoo bora katika ngazi ya kaya na taasisi.

Kabla ya Kampeini ya Usichukulie Poa, Nyumba ni Choo’ kuanza nchini mwaka 2012 katika mkoa wa Kagera asilimia 35 ya kaya hazikuwa na vyoo kabisa ambapo vyoo bora ilikuwa ni asilimia 20% tu. Lakini kutokana na juhudi za mkoa hasa kupitia idara ya Afya kuhamasisha wananchi  na kufanya ukaguzi wa kaya kwa kaya hadi sasa kaya zisizokuwa na vyoo zimepungua kutoka asilimia 35% hadi asilimia 5% tu.

Aidha, vyoo bora katika kaya mkoani Kagera vimeongezeka kutoka asilimia 20% hadi asilimia 55% na lengo ni kuhakikisha ifikapo Juni 2021 angalau asilimia 80% ya vyoo bora iwe imefikiwa katika . Vilevile Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa mkoa umejipanga katika kipindi cha miezi mitatu kufikia Agosti 2019 kila kaya lazima iwe na choo na kukitumia ili kuondoa asilimia 5% ya kaya ambazo hazina vyoo kabisa kwa sasa.

Pia kwa kunesha mfano Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kuwa uhamasishaji wa vyoo bora unajikita kwa wananchi tu lakini taasisi mbalimbali za Serikali na zisizokuwa za Serikali zinasaulika na kwa kulitambua hilo ndiyo maana yeye Mkuu wa Mkoa akishirikiana na wadau mbalimbali aliamua kujenga choo bora katika uwanja wa Kaitaba kuzikumbusha taasisi mbalimbali kuwa nazo zinatakiwa kuwa na vyoo bora katika maeneo yao.

Vilevile Mkuu wa Mkoa Gaguti  alikemea tabia ya kujisaidia ovyo ijulikanayo kama "kuchimba dawa" kwa wasafiri na madereva wa vyombo vya moto katika barabara kuu za Bukoba hadi nyakanazi na Bukoba hadi Mtukula kuwa kwa sasa hakuna haja ya kusingizia kuwa hakuna vyoo na kujisaidia hovyo na kuchafua mazingira wakati kuna maeneo yenye huduma za vyoo bora vya kujisaidia.

“Naagiza Wakuu wote wa Wilaya katika Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanasimamia uchafuzi huu wa mazingira ili kuzuia kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza kama kuhara na kuhara damu, kipindupindu na minyooo.” Aliagiza Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Naye Bw. Anyikite Mwakitalima mwakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika mkutano huo wa Mkuu wa Mkoa na Waandishi wa Habari alisema kuwa wakati kampeini ya “Usichukulie Poa, Nyumba ni Choo” inaanza mwaka 2012 kitaifa kaya ambazo hazikuwa na vyoo bora zilikuwa milioni 1.4 lakini hadi kufikia sasa kutokana na kampeini hiyo takwimu hizoo zimeshuka hadi kufikia kaya elfu 70,000 tu nchini.

Naye Msanii Maarufu wa kughani mashairi Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba alisema kuwa katika mkoa wa Kagera mkoa wenye watu wanaojipenda, mkoa wenye wasomi wa kutosha haamini kuwa asilimia 5% ya kaya hazina vyoo na kusisitiza kuwa pengine hizo ni takwimu za miaka mingi iliyopita. Mrisho Mpoto alisema kuwa labda angependa kuona mwenyewe kama ni kweli wakati akifanya uhamasishaji katika Wilaya zote za mkoa wa Kagera kwenye kampeini ya “Usichukulie Poa, Nyumba ni Choo”.

Kampeini ya “Usichukulie Poa, Nyumba ni Choo” itazinduliwa rasmi Mei 25, 2019 katika uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba ambapo uzinduzi huo utapambwa na Fainali ya mechi ya mpira wa miguu ya kombe la John Pombe Magufuli (JPM BODABODA CUP 2019) ambapo ligi hiyo iliyoanzishwa Machi 30, 2019 na kufadhiliwa na Mkuu wa Mkoa Gaguti na kuwahusisha vijana waendesha Bodaboda katika Manispaa ya Bukoba ili kuwaleta pamoja na kuwapa elimu juu ya ujasiliamali.

Katika Fainali hizo mshindi wa kwanza atanyakua zawadi ya shilingi milioni tatu pia na zawadi nyingine nyingi zitatolewa  kwa washiriki wananchi wa mkoa wa Kagera hasa Manispaa ya Bukoba wanakaribishwa kushiriki katika uzinduzi huo utakaopambwa pia Msanii Maarufu Mrisho Mpoto (Mjomba).

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.