• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Uzinduzi wa Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) Mkoani Kagera

Posted on: July 13th, 2017

Vijiji 321 Mkoani Kagera Kunufaika na Nishati ya Umeme Baada ya Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III)  Kuzinduliwa Rasmi na Utagharimu Bilioni 45.43

Wananachi Mkoani Kagera wapata neema ya nishati ya umeme baada ya Serikali kuzindua  Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu  (REA III) utakaogharimu jumla ya  shilingi bilioni 45.43 na kuvinufaisha vijiji 321 ambavyo havikupata nishati ya umeme kwenye awamu ya kwanza na  ya pili.

Akizindua Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) Kijijini Rwabigaga Kata Kamuli Wilayani Kyerwa Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani alisema mradi huo wa Umeme vijijini Awamu ya Tatu  umelenga kuvifikia vijiji na vitongoji vyote na kila mwananchi ambaye hakupata umeme kwa awamu zilizopita.

“Mradi utavilenga vijiji vyote ambavyo havikufikiwa kabisa katika awamu ya kwanza na ya pili. Pili, mradi utavifikia vitongoji vyote ambavyo viliachwa kwenye vijiji katika awamu ya kwanza na ya pili. Tatu, mradi huo umelenga kufukisha umeme kwenye maeneo ambayo hayafikiki kirahisi kama visiwani ambapo Kagera visiwa 176 vitafikishiwa umeme wa jua.” Alisistiza Dkt Kalemani

Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) Mkoani Kagera  utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza jumla ya vijiji 141 vitafikishiwa umeme na kazi hiyo inaanza kuanzia sasa mpaka mwezi Machi 2019. Awamu ya pili itafuata mara baada ya awamu ya kwanza kukamilika na vijiji 180 katika awamu ya pili vitafikishiwa umeme na awamu hiyo itakamilika mwaka 2021.

Naibu Waziri Dkt. Kalemani alisema kuwa katika awamu ya tatu kila mwananchi atafikishiwa umeme katika nyumba yake bila kubagua aina ya nyumba hata iwe ya tembe  kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na umeme. 

Baada ya uzinduzi huo Naibu Waziri Dkt. Kalemani alimkabidhi Mkandarasi  ambaye ni NAKUROI CONSTRUCTIONS  COMPANY  LIMITED atakayetekeleza Mradi huo Mkoani Kagera  na kumwagiza ahakikishe anawaajili  Wakandarasi wadogo wadogo kutoka katika maeneo husika ili kupunguza gharama na kutoa ajira kwa wazawa wa maeneo husika.

Pili, aliwaagiza Shirika la TANESCO kuhakikisha wanafungua madawati katika Tarafa na kata kwa maeneo ambayo ofisi zao zipo mbali ili kuwaondolea wananchi usumbufu wa kulipia gharama za kuwekewa umeme. Aidha, aliagiza viongozi wote wa Serikali kushirikiana na Mkandarasi kuhakikisha Tasisi zote za Serikali zinafikiwa na umeme huo katika vijiji vitakavyotekelezewa mradi.

Kitaifa Mradi wa Umeme Vijijni Awamu ya Tatu (REA III) unatarajia  kutekelezwa kwenye vijiji 7,873 na tayari umezinduliwa katika Mikoa ya Simiyu na Kagera pia utazinduliwa katika Mkoa wa Geita. Aidha, kwa upande wa mkoa Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu kwaniaba ya wananchi alimshukuru Naibu Waziri Dkt. Kalemani kwa kuzindua mradi huo na alihaidi kumsimamia kikamilifu Mkandarasi ili utekelezwe na kukamilika kwa wakati.

Baada ya uzinduzi huo uliofanyika Julai 11, 2017 Mkoani Kagera wananchi waliaswa kutumia fursa hiyo ya kupata umeme kwa kujiajili kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kujipatia ajira ili wajiingizie kipato.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.