• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Vanila ni Dhahabu ya Kijani Mkakati wa Kukomesha Wizi Mashambani Wasukwa Wezi na Walanguzi Kukiona Cha Moto – RC Gaguti

Posted on: April 15th, 2019

Dhahabu ya kijani (vanilla) Mkoani kagera sasa yawekewa mikakati imara ya kuwanufaisha wakulima na kuinua uchumi wa mkoa badala ya wananchi kutegemea mazao kama ndizi na kahawa tu ambayo yamekuwa yakilimwa kwa mazoea lakini bila kumnufaisha mkulima kulingana na anavyokuwa amewekeza hadi kuuza sokoni.

Mikakati hiyo imefikiwa baada  ya Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti kuitikia wito wa wakulima wa mazao ya vanilla, kakao, na chia na kufanya kikao nao katika Shule ya Sekondari KADEA Kanyigo Wilayani Missenyi na kusikia kilio chao cha wizi wa vanilla changa pamoja na marando yake.

Mara baada ya kutembelea na kukagua shamba la vanilla la Mwalimu Jovin Mbanga Mkuu wa Mkoa Gaguti alikutana na wakulima na kusikiliza kilio chao cha wizi wa vanilla changa na marando  katika mashamba yao ambapo wizi huo mara baada ya kufanyika vanilla hizo huuzwa nchi jirani ya Uganda.

Wakimweleza Mkuu wa Mkoa wakulima wa vanilla walisema kuwa changamoto kubwa ni wizi wa vanilla ambapo wanalazimika kulala mashambani wakilinda kila siku zisiibiwe. Wizi huo hufanywa na baadhi ya Watanzania wasiokuwa wazalendo wakishirikiana na wafanyabiashara kutoka nje nchi kwa kupewa  mitaji ya kununulia vanilla za wizi.

Pia wakulima hao mbale ya Mkuu wa Mkoa walitoa changamoto zao kuwa ni  kutokuwa na masoko rasmi ya kuuza vanilla zao mara baada ya kukomaa aidha, wanunuzi wanaojishughulisha na ununuzi wa vanilla kutosajiliwa na kutambulika Kiserikali ili mwananchi akiwa na vanilla zake aweze kuziuza katika soko na kwa mnunuzi maalum.

Baada ya Mkuu wa Mkoa Gaguti kusikiliza kwa makini malalamiko ya wakulima hao alitoa maelekeza mahususi kuhusu zao la vanilla katika Mkoa wa Kagera Kwanza; Aliagiza kuanzia tarehe ya kikao Aprili 15,2019 vanila itakuwa na muda maalum wa kuvunwa mashambani na kutakuwa na vituo maalum kama masoko ya kununulia vanilla hizo ambapo wafanyabiashara ni marufuku kwenda moja kwa moja kwa wakulima.

Akitoa ufafanuzi zaidi Mkuu wa Mkoa Gaguti alisema kwa mwananchi yeyoyote atakayekamatwa na vanilla kabla ya tarehe ya kuvunwa kutangazwa atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.

Pili; Wakulima wa Vanila wajiunge katika ushirika wa vyama vya msingi ambapo itakuwa rahisi katika kubainisha wezi, kuwa na soko la uhakika lakini pia kuuza vanilla ambazo tayari zimeongezwa thamani ili kupat bei nzuri zaidi na kuweka urahisi zaidi wa Serikali kuwasimamia kama ushirika kuliko mwananchi mmoja mmoja.

Tatu; Wafanyabiashara wote au makampuni yote yanayojihusisha na ununuaji wa vanilla wanatakiwa kujisajili na kupewa leseni ya kununua vanilla kuliko ilivyo sasa. Pia kwa Taasisi au Makampuni ambayo yanatoa ruzuku kwa wakulima wanunue vanilla kwa wakulima kulingana na bei ya soko na si kuwanyonya wakulima.

Aidha, Mkuu wa Mkoa alitoa rai kwa Watendaji wa Vijiji na Kata kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kikamilifu kama wanataka kuendelea kubaki kazini hasa jukumu la ulinzi na usalama kwa mfumo wa Nyumba Kumi Bora za Usalama ambapo wezi wa vanilla watabainika kirahisi kila eneo.

Mkuu wa Mkoa Gaguti pamoja na kufanya kikao na wakulima wa vanilla pia alichoma zana haramu katika mwalo wa Kabindi Kashenye Kanyigo Wilayani Missenyi na kutangaza rasmi kuwa mwaka huu wa 2019 atakikisha anatokomeza magendo yote iwe ya uvuvi, kahawa au vanilla na kuwataka wananchi wanaojishughulisha na biashara hiyo haramu kuacha mara moja.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Denice Mwila aliwataka wananchi wa Missenyi hasa Wakulima wa Vanila Kanyigio kubadilika kwani alisema kuwa wizi mwingine wa vanilla unatokea ndani ya familia na alitoa mfano kwa kusema kuwa unakuta shamba ni la baba na akitoka kwenda pengine Bukoba Mjini kufanya shughuli zake mama au mtoto anavuna vanilla haraha haraka na kuziuza lakini baba akirudi anaambiwa vanilla zimeibwa.

Katika kuchukua hatua kwa baadhi ya watuhumiwa ambao waliwahi kutajwa katika mikutano ya hadhara au kupigiwa kura Mkuu wa Mkoa alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Denice Mwila kuwa watu hao walipoti mara moja ofisini kwake na hatua zianze kuchuuliwa ambapo Mkuu huyo wa Wilaya alitekeleza agizo hilo mara moja kwa kuondoka na Mzee George Lubale aliwahi kutuhumiwa kujihusisha na wizi wa vanilla.

Vanila ni zao ambalo linaonekana kutaka kuukomboa mkoa wa Kagera, zao hili linalimwa katika sehemu yenye kivuli hasa kwenye migomba au kwenye miti na linahitaji mwanga sawa na kivuli asilimia 50% kwa 50%. Vanila inapandwa marando ambapo yanapandwa na kuwekewa mti aina ya jatrofa ili kukua kwa kupanda mti huo na mazao yake ni kama maharage. Bei kwa sasa sokoni tena kwa  vanila changa ni kati ya shilingi 20,000/= hadi 30,000/= kwa kilo moja.

Mwaka 2017/18 bei ya vanilla mkoani kagera ilifikia kati ya shilingi 100,000/= hadi 150,000/=  na siku za nyuma vanilla iliwahi kuzalishwa Mkoani Kagera hadi kufikia tani 103 lakini kwa sasa zinazalishwa tani 10 hadi 12 ambapo zao hili limekuwa likingiiza zaidi ya shilingi milioni 800,000/= Vanila inastawi au inalimwa na kukomaa kwa miezi tisa tu tayari unavuna na kuuaga umasikini milele badala ya kutegemea zao moja la kahawa.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.