• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Mche wa Zao la Vanilla

Posted on: May 2nd, 2017

Wakulima Wanuia Kulifanya Zao la Vanilla Kuwa Mbadala wa Kahawa na Chai na Kuinua Tena Uchumi wa Mkoa wa Kagera

Wananchi wa Mkoa wa Kagera wanuia kulifanya zao la Vanilla kuwa zao mbadala wa mazao ya biashara mkoani hapa ambapo mazao hayo ambayo ni Kahawa na Chai yalikuwa mazao makuu ya kibiasahara yaliyochangia katika kukuza uchumi wa Mkoa wa Kagera.

Zao la Vanilla huenda likawa zao mkombozi kwa wananchi wa mkoa huu baada ya kupata soko na kuwa na bei nzuri hasa katika soko la dunia jambo linalohamasisha kilimo chake ambapo kwa sasa vanilla mbichi inauzwa Shilingi 70,000/= hadi 100,000/= kwa kilo moja .

Mara baada ya Kuonekana kuwa zao la Vanilla linaweza kuwa mkombozi wa uchumi wa Mkoa wa Kagera uongozi wa mkoa uliamua kuitisha kikao cha wakulima na wadau wa Vanilla ili kuweka mikakati thabiti  wa jinsi ya kulifanya zao hilo kuwanufaisha wakulima na kukuza uchumi wa Mkoa wa Kagera.

Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa  wa Kagera alisema kutokana na zao la Kahawa na Chai kuanguka bei na kusababisha kuyumba kwa  uchaumi wa wananchi sasa zao la vanilla linaweza kuwa mkombozi na kuuinua mkoa wa Kagera kiuchumi tena.

Katika kikao hicho kilichoratibiwa na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Bw. Adam Swai alisema dhumuni kubwa ilikuwa ni kuwaleta pamoja wakulima, wanunuzi na wadau wote wa zao la vanilla ili kuweka mikakati ya pamoja kuhakikisha zao hilo linakuwa na mfumo rasmi hasa katika kautafuta masoko na jinsi ya kuwaendeleza wakulima ili wanufaike.

Wakulima na wadau wa vanilla walikubaliana kuwa sasa zao la vanilla lipewe kipaumble katika mkoa wa Kagera kama zao kuu la biashara. Pili, yaruhusiwe tu makampuni yaliyosajiliwa na kupata reseni za biashara za kununua vanilla. Tatu, bei ya vanilla itangazwe kwa maoteo mapema kulingana na maoteo ya soko la dunia na kama bei ya soko la duni ikiwa ubwa kuliko iliyotangazwa na makampuni hayo awali wakulima walipwe malipo ya pili.

Wanunuzi halali wa vanilla yaani Makampuni yalenge kumuendeleza mkulima na siyo kupatikana wakati tu wa ununuzi wa vanilla  ili kuhakikisha wakulima hao wananufaika na kilimo chao kuliko kuwaacha wanahaingaika na kupelekea kuuza vanilla zao kwa bei ndogo kwa kurubuniwa na wajanja wachache.

Aidha, Serikali iwadhibiti wanunuzi kutoka nchi jirani ambao wanawarubuni wakulima na kununua vanilla zao kwa bei ndogo na kukwepa kulipa ushuru na kodi na kupelekea kuikosesha Serikali mapato yake. Serikali ilitakiwa na wadau wa zao la vanilla kudhibiti magendo ya vanilla ili zao hilo lisije kuwa kama mazao ya kahawa yanayotoreshewa nchi jirani.

Katika hatua nyingine mwanzilishi wa kilimo cha vanilla na Meneja Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Wakulima(MAYAWA)  katika Mkoa wa Kagera Bw. Charles Kamando alisema zao la vanilla lilianza kulimwa mkoani Kagera kuanzia mwaka 1997 baada ya zao hilo kuletwa na vijana wawili kutoka Nchini Uganda waliokuwa wanafanya kazi katika shamba la Mzungu.

“Kilimo cha zao la Vanilla kilianza mwaka 1932 nchini Uganda lakini mwaka 1997 vijana wawili wa Kitanzania waliiba marando na kuja nayo Mkoani Kagera na ndipo hapo kilimo cha vanilla kilianza kwa shirika letu na tulianza kuwafundisha wakulima 85 na ndiyo mwanzo wa vanilla kuanza kulimwa Mkoani Kagera na nchini Tanzania.” Alitoa historia Bw. Kamando

Kwa sasa MAYAWA ndilo shilrika halali ambalo linajishughulisha na kuwafunza wakulima Mkoani Kagera kulima vanilla, kununua vanilla zinazozalishwa na wakulima, kuzikausha vanilla hizo kwa viwango vinavyohitajika na kutafuta masoko hasa katika soko la dunia. Kikao hicho kiliketi tarehe 28.04.2017 na vikao kama hivyo vitakuwa vinafanyika mara tatu kwa mwaka kila mwaka.

Zao la vanilla linatumika katika matumizi mbalimabli kama vinywaji, madawa ya binadamu, vyakula na vitafunwa pamoja na manukato mablimbali.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.