• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government KAGERA REGIONAL WEBSITE

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections/Units
      • Sections
        • Management Monitoring and Ispection
        • Infrastructure
        • Education
          • Primary Education
          • Secondary Education
          • Adult Education
          • Higher Education
          • Sports
          • Youth
        • Health
          • Health
          • social welfare
        • Administration And HR
        • Planning & Coordination
          • Planning
          • Statistics
          • Community Development
          • TASAF
        • Economic and Production
          • Irrigation Farming
          • Commerce and Industries
          • Fishing
          • Livestock
          • Natural Resources, Tourism & Environment
          • Co operative
          • Agriculture
        • Investment Indusrty and Trade
      • Units
        • ICT
        • Legal Unit
        • Finance and Accounts
        • Internal Audit Unit
        • Procurement Unit
        • Government Communication
  • Districts
    • Bukoba
      • Bukoba Leaders
    • Biharamulo
      • Biharamulo Leaders
    • Karagwe
      • Karagwe Leaders
    • Kyerwa
      • Kyerwa Leaders
    • Missenyi
      • Missenyi Leaders
    • Muleba
      • Muleba Leaders
    • Ngara
      • Ngara Leaders
  • District Councils
    • Bukoba Municipal Council
    • Bukoba District Council
    • Biharamulo District Council
    • Karagwe District Council
    • Kyerwa District Council
    • Missenyi District Council
    • Muleba District Council
    • Ngara District Council
  • Investment Opportunities
    • Tourism Attractions
    • Farming Opportunities
    • Agricultural Opportunities
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • Water Services
    • Agricultural Services
    • Farming Services
  • Publications
    • By Laws
    • Client Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • News Letter
  • Media Center
    • Videos
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Viongozi wa Madhehebu ya Dini Kagera Wampongeza Rais Magufuli Wahaidi Kuendelea Kushirikiana na Serikali Kudumisha Amani na Utulivu

Posted on: January 17th, 2019

Viongozi wa Madhehebu ya Dini Mkoani Kagera waipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kuchukua hatua na maamuzi yanayolenga kumuinua mwananchi mnyonge ili afaidike na raslimali za nchi yake.

Viongozi hao wa Madhehebu ya Dini Mkoani wakizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ofisini kwake Januari 16, 2019 walimpongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini na yenye manufaa kwa umma mfano ununuzi wa ndege, ujenzi wa Reli ya Kisasa na ujenzi wa mradi wa umeme wa Stigler’s Gorge pamoja na miradi mingine mingi ya maendeleo ya wananchi.

Pia Akiongea kwa niaba yao Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoriki la Bukoba Methodius Kilaini alisema kuwa wanaipongeza Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli kwa kudumisha amani, utulivu na mshikamano kwa Watanzania na kuendelea kutekeleza shughuli mbalimbali ambazo zinalenga maslahi mapana ya wananchi.

Vilevile katika mazungumzo hayo Viongozi hao wa Madhehebu ya Dini walimweleza Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali ya mkoa katika kudumisha amani na utulivu kati wananchi wa Kagera ili kudumisha mshikamano kama ilivyo desturi yao. Pia wataendelea kuhamasisha wananchi kuchapa kazi kwa bidii kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa mkoa kama jina la Mwaka 2019 kwa lugha ya Kihaya linavyohimiza kila mwananchi kufanya kazi likimaniisha kuwa kila mmoja atakula kwa jasho lake “Biluga Omumpiita”.

Naye Mkuu wa Mkoa Mhe. Gaguti katika mazungumzo hayo aliwahakikishia Viongozi hao wa Madhehebu ya Dini kuwa yeye Binafsi kama Mkuu wa Mkoa wa Kagera pamoja na Serikali ya Mkoa wataendelea kushirikiana nao kwani wao ndiyo nguzo kuu ya amani katika mkoa lakini pia nguzo kuu ya maadili hasa kwa kuiunganisha Serikali na wananchi wake.

“Sisi Serikali tutaendelea kushirikiana na nyinyi kama ilivyo desturi ya Mkoa wetu wa Kagera na tunawategemea sana katika kuhakikisha mkoa wetu unaendelea kudumisha amani na utulivu kwani kila mara mnapokutana na waamini wenu mkahubiri juu ya amani na utulivu sisi kwetu kazi inakuwa ndogo. Pia mnapowahimiza wananchi wafanye kazi kwetu sisi Serikali inakuwa rahisi mnokuweka msukumo kwa wananchi.” Alisistiza Mhe. Gaguti

Katika mazungumzo hayo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Viongozi wa Madhehebu ya Dini waliokuwepo ni pamoja na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoriki la Bukoba Method Kilaini, Sheikh Aruna Kichwabuta Sheikh wa Mkoa wa Kagera na. Askofu Dkt. Abedinergo Keshomshahara wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania Dayosisi ya Kasikazini Magharibi.

Mkuu wa Mkoa akimalizia mazungumzo na Viongozi hao alitoa rai yake kuwa Mkoa wa Kagera kwa ukiongozwa na Kaulimbiu ya “Kazi, Amani na Maendeleo” umejipanga kwa mwaka huu wa 2019 kuwa ni mwaka wa kazi lakini pia ni mwaka wa wananchi wote hasa wanaojihusisha na biashara iwe kubwa au ndogo kulipa kodi, kodi ambayo ni rafiki ili kuhakikisha Kagera inarudi kwenye enzi zake za uchumi imara.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera Yaridhia Jimbo la Uchaguzi la Nkenge Kuitwa Jimbo la Uchaguzi Missenyi

    March 17, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Mwassa Awashukuru Wabunge Kupitisha Fedha za Miradi ya Mapinduzi ya Kiuchumi Kagera

    March 14, 2025
  • Viongozi wa Dini Wahimizwa Kudumisha Mshikamano Ili Kukuza Uchumi wa Mkoa wa Kagera – RC Mwassa

    March 14, 2025
  • TULIPE KODI-RC MWASSA

    October 07, 2023
  • View All

Video

KAGERA REGION DOCUMENTARY
More Videos

Quick Links

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Radio Stations in Kagera Region
  • Kagera Regional Commissioners Since Independence 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Related Links

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • National Bureau of Statistics (NBS)
  • Government of Tanzania Website
  • Open Data Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Postal Address: S.L.P 299 BUKOBA

    Telephone: 255 28 2220215/17

    Mobile:

    Email: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service
    • Hakimiliki

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.